JE WAJUA MWANAUME ANAHITAJI NINI ZAIDI KWA MWANAMKE……


JIUNGE NA GROUP LA WAKUBA HAPA 18+ HAPA


PATA GB 30 KILA MTANDAO BURE  HAPA


 KARIBUNI wasomaji wetu katika safu hii ya mahusiano ya kimapenzi inayowajia kila SIKU, ikilenga kujuzana hili au lile kuhusiana na suala zima la mapenzi.

Awali ya yote, nitoe pongezi za dhati kwa wote ambao wamekuwa wakichangia mada za safu hii, ikiwamo kuuliza maswali.Baada ya salamu hizo, tugeukie mada ya leo ambayo inasema: ‘Mwanamume anahitaji nini zaidi kwa mwanamke?”Umewahi kujiuliza mwanamume anahitaji nini zaidi kwa mwanamke? Wengi huamini kuwa mwanamume anahitaji tendo la ndoa zaidi kuliko kitu chochote. 

JIUNGE NA GROUP LA WAKUBA HAPA 18+ HAPA


PATA GB 30 KILA MTANDAO BURE  HAPA

Lakini ukweli ni kwamba, mwanamume anahitaji vitu vingine vingi zaidi kuliko suala la mapenzi kama ilivyozoeleka.

Kuna ndoa ngapi ziko mashakani hivi sasa japokuwa wanandoa hao wamekuwa wakishiriki tendo hilo mara kwa mara? Ni wangapi wamepoteza wachumba wao wapenzi ambao wamekuwa wakiwategemea na kuamini kuwa siku moja watafunga nao ndoa japokuwa wamekuwa wakishiriki tendo hilo mara kwa mara? Bila shaka ni wengi na pengine wewe ni mmojawapo.

Bila kupoteza wakati sasa tunakwenda moja kwa moja katika kufahamu anachohitaji zaidi mwanamume kutoka kwa mwanamke wake.

Busara; Ninaposema busara namaanisha kuwa uwe na busara hasa! Baadhi ya wanawake huamini kuwa silaha ya mwisho katika ndoa ni kumpa mpenzi wake tunda, hili halina ubaya wowote na ni kweli kuwa kumpa mumeo au mpenzi wako tunda ni silaha ya mwisho katika mahusiano na ndoa, lakini hiyo pekee haitoshi!Inawezekana mpenzi wako akawa na wakati mgumu wa msongo wa mawazo na wakati mwingine akawa na kisirani bila ya wewe kujua. 

Mumeo anaweza akawa amekuja nyumbani baada ya kutoka katika mihangaiko ya kutwa na bahati mbaya katika hali ya kawaida ikawa amekosana na watu au wafanyakazi wenzake.

Mara nyingi  wanaume wakiwa katika hali hii wanategemea zaidi  kutulizwa  na wake zao, ndio  maana anaporejea huja akiwa amekunja uso na wakati mwingine kuitikia salamu yako shingo  upande au anyamaze kabisa akitegemea  msaada mkubwa kutoka kwako.

Wanawakew wasiona busara huwakaripia na kuwaambia  kama ni hasira zao za  kazini waziache  huko huko, huu si ustaarabu! Huu ni wakati wako wa kuzungumza naye na kuwa mshauri wake mkubwa kwa kumpa faraja ya moyo na kumwondolea upweke alio nao.

Hakika wewe unaweza kuwa chanzo cha furaha kwa mumeo kwa kutumia busara yako vyema katika kumshauri mumeo. Wanaume wanahitaji sana busara ya mwanamke na kama ukiweza kuwa na busara katika kumtatulia matatizo yake hata kwa kumpa mawazo yako na kumpa moyo, ataona umuhimu wako na wakati mwingine kukushirikisha kila afanyalo kabla ya kulifanya hasa baada ya kuona kuwa anaishi na mwanamke mwenye busara.

Kujali; Imezoeleka kuwa mwanamume ni kichwa cha nyumba na yeye ndiye mwezeshaji wa kila kitu katika familia, hilo ni sawa na halina ubaya wowote, lakini kuna baadhi ya wanawake wanakosa busara ya kawaida kwa kufuja mali za mumewe kisa eti ameolewa.Mjali mumeo bwana, mume wako anahitaji ujali mali zake na fedha zake kwa ujumla. Kuna baadhi ya wanawake hutumia fedha hovyo kwa matumizi ya chakula na mahitaji mengine ya familia kwa kisingizio kuwa ni wajibu wa mwanamume kufanya kila kitu katika familia.

Maisha siku hizi yamekuwa magumu, mwanamume anapenda  kuwa na mwanamke ambaye anajua bajeti vizuri ili awe na uhakika kuwa hata kama siku akiwa hana fedha za kutosha, utaweza kutumia kiasi kidogo atakachokupatia.Siku hizi wanawake wengi ambao wameolewa nao hufanya kazi kwa minajili ya kujiongezea kipato, sasa kuna baadhi ya wanawake akipokea mshahara wake ni siri yake na hahitaji hata mumewe afahamu kuwa anapata kiasi gani. Wanawake wa aina hiyo mishahara yao huishia kununua vipodozi na nguo mbalimbali ili aweze kwenda na wakati huku akisahau  kabisa wajibu wake katika kumsaidia mumewe.

Huo si ustaarabu, unapokuwa unafanya kazi na mumeo pia anafanya kazi ni wajibu wenu kusaidiana kwa kila hali, unapopata mshahara wako ni vyema ukamshirikisha mumeo ili muweze kujua namna mtakavyotumia na si kubaki na mshahara wako wote bila ya kumshirikisha mumeo.Elewa kitu kimoja maisha ya siku hizi ni kusaidiana, hivyo ni wajibu wako wewe mwanamke kumsaidia mumeo kifedha kama unafanya kazi.

Mapenzi motomoto; Pamoja na yote hayo niliyokwishaeleza lakini pia mumeo anahitaji mapenzi motomoto kutoka kwako. Hakika hii ni mada kubwa sana lakini kama unahitaji kufahamu vizuri juu ya hili endelea kufuatilia ukurasa huu kila siku.Unatakiwa kuwa mtundu sana na mbunifu wa hali ya juu katika uwanja wa sita kwa sita. Uwe mpya kimapenzi kila siku ili mumeo awe mpofu asione wanawake wa nje kabisa. Jijengee utaratibu wa kusoma makala mbalimbali za mahusiano na vijarida vinavyochambua aina mbalimbali za  mapenzi na kuwa  bora katika mahusiano. 

Kwa kufanya hayo, mumeo atakuona mpya kila siku na hivyo uwezekano wa kukuacha kuwa mdogo.Nina imani somo limeeleweka sawasawa. Hadi wakati mwingine, nashukuru kwa kutumia muda wako kunisoma.

JIUNGE NA GROUP LA WAKUBA HAPA 18+ HAPA


PATA GB 30 KILA MTANDAO BURE  HAPA

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post