Sababu 11 Za Kufanya Mapenzi Na Rafiki Yako Wa Dhati

Sababu 11 Za Kufanya Mapenzi Na Rafiki Yako Wa Dhati
Sababu 11 Za Kufanya Mapenzi Na Rafiki Yako Wa Dhati


Kufanya mapenzi na rafiki yako si jambo la kawaida. Hii ni kwa sababu wengi huamini ya kuwa rafiki yako kimtazamo flani ni kama mtu wa karibu wa familia. Pia wengi huingiwa na mtizamo wa kuwa rafiki yako ni mtu ambaye yuko kwa ajili ya kusaidiana kimawazo na wala si kufikiria mambo na mapenzi nk.

Lakini kusema ukweli ni kuwa watu inafikia wakati flani wanavutiwa kimapenzi na rafiki zao, wanatamani kuwa nao maishani nk, lakini neno 'ni rafiki yangu' ndilo linalozuia wengi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na marafiki zao.

Pakua App MPYA ya 'EDUSPORTSTZ NEWS-(Lite Version)' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako Utasoma habari zote hata kama hauna MB

Well, ushawahi kwenda katika harusi na kuwasikia wanandoa wakisema ya kuwa "mchumba wangu alikuwa rafiki yangu wa dhati"? Neno hili linatumika kwingi na wanandoa wengi. Jambo hilo ndilo limenifanya nifunguke na kutoa sababu za kwanini unafaa kufanya mapenzi na rafiki yako.


Sababu kwa nini unafaa kufanya mapenzi na rafiki yako

1. Wao ndio wanaokujua vizuri

Hii ndio inaweza kuonekana sababu moja kuu lakini wengi huidharau. Kama una rafiki wa dhati ambaye amekuvutia na unahisi kumdate ama kumfanya mwenzi wako wa mapenzi, hakuna sababu ya kujizuia kutochukua hio nafasi. After all si ni kawaida mnaambiana kila kitu, ukweli? 

Ukweli ni kuwa rafiki yako anajua kuwa wewe ni bora zaidi kuliko yeyote hivyo kufanya mapenzi naye hakutasaidia kuwaunganisha kihisia pekee, bali pia kutakupa uhakika wa kufurahishwa na penzi lao kwani wanakujua ndani na nje. Hii ni sababu kuu ya kwako wewe kuchukua hatua ya kufanya mapenzi na rafiki yako.

2. Wanawajua familia na marafiki zako

Kumkaribisha mpenzi mpya kwa familia na marafiki zako kunaweza kuwa vigumu kwa mara ya kwanza. Lakini kwa rafiki yako wa dhati, ashazoea kukutana na familia yako na marafiki zako hivyo ni rahisi kuwatambulisha. Iwapo unatafuta mchumba wa kiurahisi, rafiki yako wa dhati ni rahisi kwani anayajua maisha yako ya nyumbani na mara nyingi kawaida amekubalika katika familia.

3. Wanaweza kuwa wamevutiwa kimapenzi na wewe

Kumwapproach mwanamke ambaye humjui kunahitaji kujiamini kwa hali ya juu. Lakini ukiwa na uzoefu wa kukaa na kuongea na mtu kwa muda mrefu inafikia wakati flani nyote wawili mnavutiana. Hivyo amini usiamini ukianza kumwapproach rafiki yako wa dhati na kumfungukia anaweza kukushangaza na jambo ambalo hukulitarajia. Hii ni kinyume na vile ambavyo unaweza kuwa wakati ambapo unaaproach mtu ambaye ni mgeni kwako.

4. Wanajua vitu unavyotaka...chumbani

Katika sababu zote za kufanya mapenzi na rafiki yako, hii ndio hafifu zaidi lakini ambayo inachangia pakubwa. Hebu fikiria wewe na rafiki yako mmekaa unamweleza chochote kile ambacho kinakuja akilini mwako. 

Bila shaka ushawahi kumwambia kuhusiana na deti yako ya mwisho ambayo ilienda vibaya ama kumwelezea jinsi ulivyombusu ex wako na ulipendezwa, mitindo ya mapenzi uliokuwa ukifanya na jirani yako wa chumbani nk. Kumwelezea haya yote bila shaka atakuwa amejenga taswira ya mambo ambayo unapenda na kutopenda ikija maswala ya chumbani, hivyo inatoa fursa kwake kujua mengi kama utachukua hatua ya kufanya mapenzi naye.

Pakua App MPYA ya 'EDUSPORTSTZ NEWS-(Lite Version)' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako Utasoma habari zote hata kama hauna MB

5. Hautakaa ungojee simu yake

Jambo zuri kuhusu rafiki yako wa dhati ni kuwa amejitolea kukupenda bila masharti yeyote. Hivyo hutakuwa na tashwishi ya kuwa hatokupigia simu baada ya nyinyi wawili kufanya mapenzi. Na iwapo kutatokea tatizo kuwa hakukupigia simu, bado kuna nafasi ya kwenu kurudiana kuwa marafiki.

6. Hawatakutumia

Mara nyingi katika mahusiano, kuna panda shuka nyingi za kawaida ambapo wapenzi wawili wanaachana kwa kuwa wanagundua mmoja alikuwa anamtumia mwenzake kimapenzi ama kumtumia kwa njia nyingine. Lakini ikija wakati wa kufanya mapenzi na rafiki yako, hauna tashwishi yeyote kwani unajua rafiki yako anakupenda na hayuko hapo kwa sababu ya kujiridhisha yeye mwenyewe. Mwanzo rafiki yako lengo lake kuu ni kukuridhisha wewe zaidi kujiliko, hivyo inatoa nafasi nzuri kwa wale ambao wamekuwa katika uhusiano wa kimapenzi ambayo imejawa na uchoyo mwingi.

7. Wanakupenda

Rafiki wako wa dhati anakupenda. Yeye ameshaona matatizo na furaha zote ambazo umepitia, wanajua tabia zako zote, aidha nzuri au mbaya. Hivyo kufanya mapenzi nao hakulipi pekee, bali pia kunaridhisha na kutimiza. Mwanzo unajenga ukanda wa faraja kwenu wawili hivyo hutakuwa na wasiwasi wowote katika mahusiano yenu.

9. Unaweza kurudi

Uzuri wa kuwa na uhusiano wa kimapenzi na rafiki yako ni kuwa iwapo itatokea wakati flani ambapo nyote wawili mumeona kuwa mahusiano yenu hayawezi kuchukua hatua nyingine, ama iwapo umepata mchumba ambaye umeona anafaa kuwa na mahusiano nawe basi unaweza kukatiza mahusiano ya kimapenzi na rafiki yako. Unaweza kukatiza mahusiano ya kimapenzi na rafiki yako na mkarudi kuwa marafiki wa kawaida bila kuwa na hisia zozote zile ilimradi nyote wawili mmepatana.

10. Unajiskia huru ukiwa naye

Rafiki yako wa dhati mmekua mkijuana kwa muda mrefu sana hivyo inamaanisha umemwelezea mengi kujihusu na anajua mengi kukuhusu. Hivyo kuwa naye unajiskia huru zaidi kuliko yeyote yule. Hauwezi kuingiwa na hisia za kujishuku wakati ambapo mnafanya yenu, hata kama ni mara yenu ya kwanza. 

11. Unaweza kuruka ile hatua ya kujuana

Kwa kuwa mumekuwa marafiki kwa muda mrefu, nyote wawili mkiingia katika mahusiano itakuwa haina haja ya kufuata mkondo wa kawaida wa kuapproach mwanamke na kumtoa deti. Hatua kama hizi mnaweza kuziruka na kuangalia mambo mengine. Ijapokuwa unaweza kutojua siri nyingine za rafiki yako, haina haja ya kufuata mikondo ya kawaida ya kuapproach mwanamke.

Kuna sababu nyingi za kwa nini unafaa kufanya mapenzi na rafiki yako, so chukua nafasi hii kujaribu labda unaweza kupata saprize ambayo hujawahi kuitarajia. Kuna ile hadithi ambayo imekuwa ikipitishwa kutoka kizazi kimoja hadi kingine eti kuwa na uhusiano na rafiki yako kunaharibu mahusiano. 

Ok, mwisho wa siku wewe ndie unayemjua rafiki yako vizuri na unajua vitu anavyopenda nk. Pia kuwa na mahusiano na rafiki yako ni salama zaidi kuliko yule ambaye umemtongoza kwa klabu.

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post