FANYA MAMBO HAYA KWA MTOTO WA KIKE NA UUTEKE MOYO WAKE

FANYA MAMBO HAYA KWA MTOTO WA KIKE NA UUTEKE MOYO WAKE

MTENDEE UUNGWANA, UKARIMU Ili kuhakikisha unaiteka roho ya msichana kwa jinsi hii, jitahidi kuwa mtu wa mahaba, badala ya kuonekana kuwa na tamaa ya kumwingilia kimwili. Pia mshike mkono wake kwa jinsi isiyoonesha tamaa bali upendo, mfungulie mlango wa nyumba na gari, mwandalie kiti mfikapo mahali na mkataka kukaa na kwa ujumla mfanyie ukarimu na uungwana.

Pakua App ya 'EDUSPORTSTZ NEWS' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako Utasoma habari zote hata kama hauna MB

MCHUKULIE WA THAMANI Pia katika vitendo vyako, mfanye msichana adhani unamchukulia kuwa wa thamani na wa maana sana . Unapompeleka nyumbani kwako, mathalani, mbusu mkononi au shavuni (akiwa tayari) wakati wa kuagana naye, huku ukimwahidi kuwa utampigia simu. Msichana atashangaa na kujiona wa thamani kubwa kwako, kwani umemtendea kama mtu muhimu kwako.

MTENDEE KAMA MALKIA Ikitokea ukatoka na msichana huyo mara nyingine, au akakutembelea nyumbani kwako, endelea kumchukulia kama binti mfalme au binti malkia.
Katika zama hizi za kupungua kwa upendo katika jamii, wanawake wana kiu ya mahaba na mwanaume anayefahamu jinsi ya kutoa mahaba ni mtu adimu kwa watu wa jinsia ya kike.

 USIHARAKIE NGONO Katika siku za kwanza, hakikisha kuwa huwi na haraka ya kutaka ngono, kwani ukivuta subira, msichana mwenyewe atakuonesha kwa ishara kuwa yuko tayari kwa ngono. Vuta subira, kwani kabla hujakata tamaa na kujiona unachelewa kuonja asali, tayari msichana huyo ataanza kuanguka penzini na wewe kwani wewe ni mwanaume unayemheshimu na kumtendea kwa ukarimu, mahaba na heshima.

Soma Zaidi>>>Kazi Ya Shanga/Cheni za Kiunoni Kwenye TENDO La Ndoa

Hakika hata yule mwanamke anayedhaniwa kuwa malaya au changudoa hupenda kutendewa hivi na mwanaume. Kwa hiyo kwa ujumla, kabla ya kufikia mahali ukajidhania kufanikiwa katika medani ya utongozaji na ukampata mwanamke wa kukufaa, unapaswa kufahamu ni nini hasa wanawake hutaka kutoka kwa wanaume na jinsi ya kujipatia nafasi katika moyo wake na baadaye kuuteka.

SIFIA UZURI WAKE Mwambie msichana huyo kuwa ni mzuri, na kwamba ni mtu wa kufaa kuwa naye maishani – mtu anayefaa kuwa mama wa watoto wako. Wanawake hupenda sifa kama hizo hasa kama watahisi kuwa mwanaume amezitoa kwa dhati na si kwa kutania au kudhihaki, au kumvalisha kilemba cha ukoka. Hapa inambidi mwanaume kuwa makini, asije akatia chumvi sana , akashtukiwa.

ACHANA NA WANAWAKE WENGINE Jambo lingine la muhimu ni kuhakikisha kuwa unapokuwa unamfuatilia mwanamke mmoja huwi na tamaa ya kuwafuatilia wengine wengi. Hakikisha kuwa msichana unayemfukuzia anahisi kuwa umeweka akili yako yote kwake. Hata hivyo, hakikisha kuwa hufikii mahali ukawa kama mjinga kwa ajili ya kutaka kumfurahisha, kwani hakika hutamfurahisha kwa kufanya hivyo bali unaweza kumkosa.

Na kama baada ya kumtendea ukarimu na kumheshimu bado ataonekana akiendelea kuambatana na wanaume wengine au kuzungumzia wapenzi wake wa zamani, achana naye kwanza, kwani huyo hajakuheshimu.

MFANYE KUWA RAFIKI Lakini kuna ushauri mkubwa zaidi anaoweza kupewa mwanaume, hasa kijana, kuhusiana na wanawake. Ukiutekeleza ushauri huu basi karibu kila mwanamke utakayekutana naye atakupenda na inaweza hata ikadhaniwa kuwa unatumia dawa. Ushauri wenyewe ni kwamba jitahidi kumfanyia urafiki mwanamke unayetoka naye.

Mpe nafasi ya kujisikia huru na salama awapo na wewe na utabaini muda si mrefu kuwa umekuwa mmoja wa wanaume wanaopendwa zaidi katika sayari hii kwani wanawake wengi ( kama si wote) watakupenda. Hii itatokana na ukweli kuwa kila msichana utakayetoka naye, hata katika hali isiyokuwa ya kimapenzi, atawaeleza marafiki zake kuhusiana na tabia yako na kila mmoja atatamani kutoka na wewe kwani unafahamu jinsi ya kumkuna mwanamke pale panapomwasha, kwa matendo yako.

Soma Zaidi>>>Sababu Zinazopelekea Mwanamke Kutokuolewa Kabisa

Inaaminika kuwa kitu ambacho humfanya mwanamke ampende sana mumewe au bwana wake, au mwanaume mwingine yeyote, ni ule ukweli kuwa mwanaume huyo amemwonesha urafiki mkubwa. Rafiki ni mtu ambaye mnajuana, kupendana na kuaminiana na mara nyingine huweza kuitwa maswahiba au wandani. Ni mwanamke mjinga tu asiyeweza kumpenda mtu aliyemwonesha sifa hizi.

USIJILAZIMISHE KUMPENDA Jambo la msingi kabla ya kutekeleza yote yaliyobainishwa hapo juu ni kujihakikisha wewe mwenyewe kwanza kuwa mwanamke mwenyewe unampenda kwa dhati na si kwamba amekulazimisha mwenyewe kwa kukuganda. 

Hakikisha kuwa hujilazimishi kuambatana na mwanamke ambaye rohoni mwako huhisi kumpenda. Kama msichana atakujia na kukwambia kuwa anakupenda lakini wewe ukawa huhisi mapenzi kwake, kuwa mkweli na kumwambia kuwa hauko tayari kuambatana naye. Wanawake pia humpenda mwanaume aliye muwazi na mkweli.

HAKIKISHA ANAKUPENDA KWELI Sasa baada ya jitihada zote za kumwingiza ‘line’ mwanamke ambaye una uhakika kuwa unampenda, unaweza ukajikuta katika mtihani mwingine: hujui kama mwanamke unayemfukuzia amekupenda kwa dhati au la. Hupaswi kuwa na wasiwasi kuhusiana na hili pia.

Hebu tuangalie dalili kadhaa za mwanamke ambaye hakupendi. Kwanza, kama mwanamke hakupendi, hata baada ya kumwonesha kila dalili kuwa unamjali na umemfanya swahiba wako, utabaini kuwa kila unapotaka kumkaribia yeye anasogea, au anakukwepa. Mwanamke huyu pia utamwona akionekana kama mtu aliyekerwa na jambo kila unapokutana naye, ataepusha macho yake kukutana na yako, atakunja mikono yake kifuani mwake kuepuka kukushika mkononi mnapokutana na atajitahidi kufunga miguu yake unapozungumza naye. Pia mwanamke huyu ukiwa naye anaonekana kutojali na kama ana simu atakuwa anatuma au kupokea ujumbe wakati wewe ukimweleza jambo. 

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post