FAHAMU TATIZO LA MWANAMKE KUA NA UKE MKAVU NA MATIBABU YAKE.



Tatizo la uke mkavu lipo kwa baadhi ya wanawake japo sio wote, ni tatizo ambalo kimsingi linaweza kuleta msongo wa mawazo kwa wahusika, maumivu wakati wa tendo ndoa, kukosa hamu ya tendo la ndoa, au kuvunja mahusiano kabisa, kupata vidonda ukeni hata kuvuja damu.


Ni tatizo ambalo linaweza kua chanzo cha aibu kwa wanawake na kushindwa kujieleza tatizo hilo kwa wataalamu wa afya kwa kuogopa aibu.


Pakua App ya 'EDUSPORTSTZ (LITE VERSION)' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako Utasoma habari zote hata kama hauna MB


Kushuka kwa kiwango cha homoni ya oestrogen mwilini hasa mwanamke anapofikisha umri wa miaka 40 kwenda mbele ndio chanzo kikuu cha kukauka kwa uke na dalili hizo hua wazi kabisa mwanamke anapofikika menopause au mwisho wa kuona siku zake za mwezi lakini kuna vyanzo vingine kama


msongo wa mawazo


kunyonyesha


kuvuta sigara


baadhi ya magonjwa mfano hypothyrodism


mazoezi makali


uzazi


matibabu ya saratani


upasuaji wa kuondoa mayai ya mama.


baadhi ya dawa


kutokua na hisia na mwenza husika.


Nini cha kufanya?

ukipata tatizo hili unaweza ukamuona mtaalamu wa afya ambaye atakuchukua maelezo marefu na baadae atakupa suluhisho la matatizo yako kulingana na chanzo ambacho atakiona.


Lakini pia kwa wanawake ambao wanapata ukavu huu sababu ya umri basi kuna dawa mbalimbali za kupaka ambazo hua zina homoni ya oestrogen ndani yake ambayo huweza kusaidia tatizo hili, kumbuka tumia dawa tu ambayo imeelekezwa kwa kazi hii kwani baadhi ya dawa zimechanganywa na vitu mbalimbali kama perfume, na vitu asilia ambavyo sio salama kwa uke.

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post