( Kujifahamu Mwenyewe ni Hekima ;
Na kuwatambua Wengine ni Uelewa zaidi )
Na kuwatambua Wengine ni Uelewa zaidi )
### 1. SANGUINE
Sanguine ni watu wachangamfu kupita kiasi, wacheshi, wawazi, wanaojichanganya na watu.
Sanguine ni watu wachangamfu kupita kiasi, wacheshi, wawazi, wanaojichanganya na watu.
SIFA ZAO KWA UJUMLA
1.Wanafanya marafiki kwa kwa haraka; wanapenda kujichanganya na kufamihana na watu; hupata marafiki haraka sana.
2.Ni wazungumzaji sana kuliko kusikiliza ( they are dominant in conversation)
2.Ni wepesi kwendana na mazingira.
3.Wana huruma, wepesi kulia na kusamehe.
4.Hawana utaratibu wa kufanya mambo ( Ni watu wasiokuwa na mpango kazi ).
5. Si watu wa kuaminika sana ( Ni wambea ) maana wanaweza kutoa siri za ndani kireja reja tu (kumwaga mtama kwenye kuku wengi ) sababu ya kupenda kuongea. Yaani sio watunza siri wazuri.
6. Hupenda burudani na raha, ucheshi na mitoko.
7. Hupenda kwenda na wakati (Fashions ) na mambo yenye umaarufu mkubwa.
8. Ni wasahaurifu.
9. Wanaishi kwa wakati uliopo; hawaogopi wakati ujao.
10. Ni watu wa 'misisimko'.
11. Hupenda kusifiwa na kujionesha
( mfano kuongea Kiswahili cha kisasa kutafuta kiki ) ; kutafuta umaarufu.
( mfano kuongea Kiswahili cha kisasa kutafuta kiki ) ; kutafuta umaarufu.
12. Pamoja na kufanya marafiki wengi kwa muda mfupi ( maana wanapenda kujichanganya na watu hata wasiofahamiana nao kwa karibu kwa sababu hujisikia raha sana kadri wanavyokutana na kujichanganya na watu wengi ) lakini pia hupoteza marafiki haraka.
13. Huepuka sana marafiki wanaowachosha ( wanao waboa ) au wasiokuwa wachangamfu.
14. Hushawishi wenzao na watu wengine kuungana katika mambo wanayopenda, hupenda kushawishi kwa kuwaambia wenzao, "....jamani nakuambia, hujui unachokikosa wewe "!.
15 . Ni wanadhifu hasa katika mavazi ( ni watu wanaopenda kutokelezea ) wanapenda sana kupiga pamba.
SIFA ZA KIROHO
• Wakarimu
• Wahamasishaji ( Washawishi )
• Wahamasishaji ( Washawishi )
UDHAIFU WA KIROHO
• Wanapenda misisimuko.
• Wanaona msamaha kwa uzembe.
• Wanaongoka kidogo sana.
• Wanaona msamaha kwa uzembe.
• Wanaongoka kidogo sana.
SIFA ZA KIAKILI
• Ni wagumu kuelewa 'especially deep concept '; Wapesi kusahau.
• Wanapungukiwa na utawala binafsi ( Self-control ).
• Ni watu wa misisimko.
• Hawafikii malengo yao ; Wanashindwa na magoli mafupi.
• Hawezi kuchanganua mambo kwa kina.
• Wanapungukiwa na utawala binafsi ( Self-control ).
• Ni watu wa misisimko.
• Hawafikii malengo yao ; Wanashindwa na magoli mafupi.
• Hawezi kuchanganua mambo kwa kina.
SIFA ZA KIJAMII
• Anafanya marafiki kwa urahisi.
• Ni wepesi kushiriki na wengine katika furaha na majonzi.
• Wanahuruma na ni wepesi kusamehe ( hawalipagi kisasi ; hawana mtima-nyongo )
• Ni wepesi kushiriki na wengine katika furaha na majonzi.
• Wanahuruma na ni wepesi kusamehe ( hawalipagi kisasi ; hawana mtima-nyongo )
UDHAIFU WAO MKUBWA
~ Si wasikivu na wanapenda sana kutawala mazungumzo.
~ Sanguine anapoteza muda mwingi kwa kuongea wakati ambapo angefanya kazi.
~ Sanguine anapoteza muda mwingi kwa kuongea wakati ambapo angefanya kazi.
KAZI WANAZOPENDELEA
• Sanaa / Uigizaji.
•Kupokea wageni ( reception )
• -'MC' ( Uzungumzaji wa hadhara )
• Kuhubiri
• Kutembelea na kuuguza wagonjwa.
•Kupokea wageni ( reception )
• -'MC' ( Uzungumzaji wa hadhara )
• Kuhubiri
• Kutembelea na kuuguza wagonjwa.
Mfano watu wa hulka hii ni, Mfalme Daudi - 2 SAMWELI 12 : 1-6., Miriamu dada yake Musa - KUTOKA 2 :3-7.
### 2. MELANCHOLIC
Ni watu wenye tabia ya kupenda kutenda jambo / mambo kwa ubora wa hali ya juu.( Perfectionistic )
Ni watu wenye tabia ya kupenda kutenda jambo / mambo kwa ubora wa hali ya juu.( Perfectionistic )
SIFA ZAO KWA UJUMLA.
1. Hupenda kufanya mambo kwa umakini sana. Mfano Luka ; mwandishi mmoja wa vitabu vya Injili - LUKA 1 " Inafaa nami pia, Mheshimiwa, baada ya kuchunguza kwa makini mambo yote tangu mwanzo, nikuandikie kwa mpango,- BHN
2. Wanauwezo mkubwa wa kufikiri na kuchambua mambo kwa kina ( wana high IQ ).
3. Hawapendi kujichanganya na watu na hutumia muda mwingi kukaa peke yao ; maana wakiwa peke yao huwa na amani zaidi na ndio huchaji sana akili zao.( Kuna watu wanaitwa great thinkers, wanaweza kutumia hata siku nzima, hajakutana na mtu, kajifungia chumbani peke yake ).
3. Ni watulivu na wakimya Lakini wakipata mtu wa kuzungumza naye katika mazingira tulivu huzungumza kweli kweli .(" ...kumbe ukimya si upumbavu ...na upole si umbu-mbumbu."
4. Melancholic hupenda kujifunza na kuelewa mambo mengi tena kwa kina hata mambo madogo madogo ili kuwa na maarifa zaidi badala ya kuwa wajinga.
Hawaridhiki wala kukubali mambo kirahisi rahisi tu kama wanavyoyaona. Ni wadadisi na huuliza maswali maalum ili wapate kuelewa vizuri.
Hawaridhiki wala kukubali mambo kirahisi rahisi tu kama wanavyoyaona. Ni wadadisi na huuliza maswali maalum ili wapate kuelewa vizuri.
5. Ni watata kwa sababu Mara nyingi hushikilia msimamo wao na mawazo yao wakiamini ndo sahihi, na hivyo basi hawayumbishwi kirahisi.
6. Ni watu wenye panic / hofu ; wanamihemko ya haraka ( emotionally are very sensitive ), wakimya wenye haya / aibu.
7. Hupenda kujenga hoja ili kufanya jambo fulani kwa ubora, lakini husononeka sana jambo hilo lisipotimia.
8. Hawapendi sifa za kijinga jinga ; huwa hawapendi mtu anayejipendekeza kuwasifia sifia.
" Ikawa alipokuwa akisema maneno hayo, mwanamke mmoja katika mkutano alipaza sauti yake , akamwambia, Heri tumbo lililokuzaa, na matiti uliyonyonya. Lakini yeye alisema," Afadhali ,heri walisikiao neno la Mungu na kulishika. - LUKA 11:27,28.
9. Hupendelea kuwa na marafiki wachache hasa wa daraja lao.
10. Hutafakari sana jambo kabla ya kulitenda na kuchukua hatua ; hawakurupuki.
11. Huwapa marafiki tahadhari.
12. Wanajihamini sana ; ila wana ukosefu wa kuamini wengine.
13. Wanapenda muziki na sanaa.
14. Wana vipawa ; wanakabiliana kwa akili sana.
15. Hupenda mambo yaliyofanywa kwa mpangilio nzuri.
16. Huwa na njozi tele za mafanikio, na hupenda kufanya mambo makubwa na yenye umaarufu duniani.
• ~ wanajichunguzaga sana kiasi cha kujiumiza.
A.SIFA ZAO ZA KIROHO.
• Wanachukia kinyongo na kulipiza kisasi.
• Huwa ni waongofu kweli kweli. e.g Mtume Paulo.
• Wengi ni wafia dini.
• Huwa ni waongofu kweli kweli. e.g Mtume Paulo.
• Wengi ni wafia dini.
B. UDHAIFU KIROHO.
• Ni wepesi kukosa matumaini kwa sababu wana hisia nyingi na mashaka. 1 Petro 1 :5-7.
C. SIFA KIAKILI
• Wana uwezo mkubwa wa kufikiri na kuchambua mambo.
• Wanapenda kufanya mambo kwa ubora hata kama ni dogo.
• Wanajua mipaka yao binafsi.
• Ni watu wenye misimamo isiyoyumbishwa kirahisi / sio bendera fuata upepo.
• Wanapenda kufanya mambo kwa ubora hata kama ni dogo.
• Wanajua mipaka yao binafsi.
• Ni watu wenye misimamo isiyoyumbishwa kirahisi / sio bendera fuata upepo.
D. UDHAIFU KIAKILI.
• Wanaweka viwango vya juu sana ambavyo hata wao wenyewe hawawezi kuvifikia ; na hupenda kujilaumu sana.
• Melancholic huwa anatafuta ukamilifu na kutoa hukumu ya kila kitu kulinga na mawazo yake mwenyewe.
• Wanajichunguzaga sana kiasi cha kujiumiza.
• Wanachoka kwa haraka.
• Huwa pia na mashaka kwa mema wanayoambiwa.

E.SIFA KIJAMII.
FAIDA.
• Ni watu wa kutegemewa katika mawazo na ubunifu wa mambo makubwa, maana wamejaa njozi.
• Ni marafiki wa kujitoa kafara.
• Ni wasiri na waaminifu.
• Ni watu wa kutegemewa katika mawazo na ubunifu wa mambo makubwa, maana wamejaa njozi.
• Ni marafiki wa kujitoa kafara.
• Ni wasiri na waaminifu.
UDHAIFU WAO KIJAMII
• Wanapenda kujitenga na wengine. " Kujitenga kwao wakati mwingine huwafanya wajihisi kutopendeza au kutothaminika mbele za watu ingawa huo sio ukweli."
• Wana hali ya kutoamini wenzao.
• Wana hali ya kutoamini wenzao.
KAZI WANAZOPENDA KUFANYA
# Wengi wao ni;
~ wanajimu
~ engineer
~ wanasaikoji
~ wanafalsafa
~ madaktari
~ wanajimu
~ engineer
~ wanasaikoji
~ wanafalsafa
~ madaktari
Mfano mwingine wa kundi hili ni YOHANA Mbatizaji " Yesu akamalizia kwa kusema, " Nawaambieni, kati ya binadamu wote hakuna aliye mkubwa zaidi kuliko Yohane Mbatizaji." .... LUKA 7:28. BHN
### 3. CHOLERIC
Tabia yao ni kupenda ukubwa ( dominant ) ,majivuno na kutumia mabavu / ubabe.
Tabia yao ni kupenda ukubwa ( dominant ) ,majivuno na kutumia mabavu / ubabe.
TABIA ZAO KWA UJULA
1. Hupenda kujikweza na tabia ya kujifanya kujua kila kitu zaidi ya wenzao.
Wengi wanyanyasaji na wanapenda kuburuza wenzao na baadhi yao wachache tu kama Mtume Petro ndo wanaweza kutetea watu wasiburuzwe. MATHAYO 17:24.
Wengi wanyanyasaji na wanapenda kuburuza wenzao na baadhi yao wachache tu kama Mtume Petro ndo wanaweza kutetea watu wasiburuzwe. MATHAYO 17:24.
" Kwa kawaida Petro alikuwa mwenye kimbelembele na mshupavu, na Shetani alikuwa ametumia sifa hizi
kumpindua ". - Tumaini la Vizazi vyote , Sura ya 85 ' Kando Ya Bahari Tena '.
kumpindua ". - Tumaini la Vizazi vyote , Sura ya 85 ' Kando Ya Bahari Tena '.
2. Choleric huwa anataka mapendekezo yake tu ndo yafanyiwe kazi. Analazimisha wengine kukubaliana mpango kazi wake. Ana magoli na kuyafikia.
3. Hawana huruma ni wakali ; wana hasira sana, wanachukia kwa kutoa machozi ; si mvumilvu kwa wanaoitilafiana naye ; hutunza chuki kwa muda mrefu ; si mwepesi kusamehe na wanapenda kulipiza kisasi.
4. Anawatumia watu kwa faida ; hajali mahitaji ya watu wengine. Ni wabinafsi.
5. CHOLERIC huwa na maoni ya hali ya juu sana ; hakatishwi tamaa kirahisi ( hayumbi-yumbi ), ni mtendaji hasa. Ni mwepesi na mjasiri wakati wa dharura.
6. Wengi ni shupavu na wenye chuki zisizo na sababu, huwakosoa wenzao kwa fujo, hupenda ligi ( mashindano ), hujiamini sana na kushughulikia tatizo kwa harara na fujo, na tabia yao ya kukosoa kusoa wenzao, pia ni watu wa kujihesabia haki.
7. Hupenda kuonesha wanavyotisha, yaani jinsi walivyo juu, ....." Mimi ndiye mwenyewe bhana," ...." Unanijua mimi",,,," Ujui kwamba Mimi ndo mwalimu mkuu wa shule",.
..
8. Wanapenda kujitambulisha au kutambumbulishwa kwa cheo ( sifa)
..
8. Wanapenda kujitambulisha au kutambumbulishwa kwa cheo ( sifa)
9. Wana lugha za amri ( command language ) / lugha za ubabe ; ni wagumu wa kutumia lugha ya kuomba na kusihi, neno naomba, tafadhali, samahani,pole ; kwao ni msamiati. ....
10... Ni wagumu kukubali makosa ( Hawapendi kujishusha ) ; wanaogopa kwamba itawashushia hadhi na heshima.....eti mkubwa huwa hajambi.
11. Wanapenda uongozi .
Ki ukweli tabia yao ya kupenda kutawala wenzao ndo huwafanya kuwa viongozi.
Ki ukweli tabia yao ya kupenda kutawala wenzao ndo huwafanya kuwa viongozi.
12. Wanapenda sana kuheshimiwa ; na yule asiyefanya hivyo huwekewa kisasi na kufikiriwa ni mpinzani.
Wanaweza kuwa marafiki wazuri ikiwa hautaingilia mambo yao, kinyume na hivyo wanaweza kuhakikisha wamekukomesha kwa namna yo yote ile.
Wanaweza kuwa marafiki wazuri ikiwa hautaingilia mambo yao, kinyume na hivyo wanaweza kuhakikisha wamekukomesha kwa namna yo yote ile.
*** Wanafaa sana kuwa viongozi hasa kuongoza mataifa ya watu wazembe na wavivu.***
Ushauri / MAONI
• Choleric aoane na PHLEGMATIC.
• Choleric aoane na PHLEGMATIC.
• Kama wewe ni Choleric avoid Over-Reaction because Overreacting it causes hardening to the brain arteries, leading to a decrease in mental power ".
BIBLIA Inasema ," Kwani hasira humwua mtu mpumbavu." - AYUBU 5:2
BIBLIA Inasema ," Kwani hasira humwua mtu mpumbavu." - AYUBU 5:2
• " Lakini nimekuombea wewe ili imani yako isitindike ; nawe utakapoongoka waimarishe ndugu zako." LUKA 22:32,
" Kabla ya kuanguka kwake, Petro alikuwa mara kwa mara anaongea pasipo uangalifu, kutokana na hisia za mvuto
wa wakati husika. Kila wakati alikuwa tayari kuwakosoa wengine, na kuonyesha mawazo yake, kabla ya kuwa na
hali ya kujifahamu kwa uwazi au kuelewa kitu cha kusema.
wa wakati husika. Kila wakati alikuwa tayari kuwakosoa wengine, na kuonyesha mawazo yake, kabla ya kuwa na
hali ya kujifahamu kwa uwazi au kuelewa kitu cha kusema.
Lakini Petro aliyekuwa ameongoka alikuwa tofauti
sana. Aliendelea kuwa na ari ile ile ya awali, lakini neema ya Kristo ilitawala ari hiyo. Hakuwa tena mtu wa
ushupavu wa msisimko, wa kujiamini binafsi, na wa kujiinua, bali mtulivu, (815) mwenye kujitawala, na
anayefundishika." - Tumaini LA Vizazi vyote , Sura Ya 85 , ' Kando Ya Bahari Tena ".

### 4. PHLEGMATIC
Ni watu wapole, wenye huruma, wataratibu na wanapenda amani.
Ni watu wapole, wenye huruma, wataratibu na wanapenda amani.
SIFA ZAO KWA UJUMLA.
1. Huogopa sana migogoro ; tena hawaianzishi ; ukiwalazimisha
kuingia kwenye migogoro basi uchanganyikiwa kabisa na utafuta njia ya kuepuka badala ya kutafuta ushindi.
Hawapendi Shari na mtu yeyote.
kuingia kwenye migogoro basi uchanganyikiwa kabisa na utafuta njia ya kuepuka badala ya kutafuta ushindi.
Hawapendi Shari na mtu yeyote.
2.Hujiheshimu sana na hupenda kufanya mambo kwa ufuata kanuni na utaratibu badala ya kujitia matatani.
Yaani kuliko kufanya jambo wakakosea kwao huona bora wasifanye kabisa.
Yaani kuliko kufanya jambo wakakosea kwao huona bora wasifanye kabisa.
3. Hupenda kuongozwa na Mara nyingi hutenda jambo vizuri zaidi pale wanapoagizwa kutenda hivyo.
4. Hawajiamini sana, hupenda wenzao ndo watoe uamuzi.
5. Si wajuaji Hawapendi kujikweza ; Hawapendi ubishi usio na maana ili kuepuka matokeo mabaya ya migogoro.
6. Si wabinafsi ( wanajali wengine ), SIKU zote huwaweka wenzao mbele . Hawajioni WAO ni bora kuliko wengine ; na hujitoa sana ( kujinyima )kwa ajili ya kuwapa furaha wengine.
7. Phlegmatic ana marafiki wengi ; ni mwaminifu na mptanishi (peace maker )
8. Ni wabahili.
9. Si wepesi wa wa hasira ( " Hasira hukaa kifuani mwa mpumbavu " MITHALI
10. Wepesi kuomba radhi ; hujlaumu kwa makosa wanayotenda, na hata kama kosa si lao, kwa kufanya hivyo hujisikia amani.
11. Anatoa ushauri anapoulizwa tu.
12. Ni nadhifu na hodari na wanatekekeleza ahadi zao .Si waongeaji sana. Hupenda sana kuongozana na marafiki zao
13. Kazi wanazopendelea kufanya ni mahakimu / majaji , wahasibu, wanadiplomasia, wapelelezi, ufundi
14. -Mapenzi (love affairs) si kitu kinachowaumiza sana (kundi linaloongoza kwa kuwa single ).
15 . Wao wanavurugu za chini-chini.(wengi wao wana mambo ya chini chini )
16. Hawapendi kutenda jambo kwa namna inayowaathiri wenzao; na hawapendi kuwaaibisha wenzao.
" Naye Yusufu, mumewe, kwa vile alivyokuwa mtu wa haki, asitake kumwaibisha, aliazimu kumwacha kwa siri ". MATHAYO 1:19
" Naye Yusufu, mumewe, kwa vile alivyokuwa mtu wa haki, asitake kumwaibisha, aliazimu kumwacha kwa siri ". MATHAYO 1:19
MAMBO MUHIMU UNAYOPASWA KUYAZINGATIA.
* Si tabia zote za kundi lazima ziangukie sehemu moja.*
-Kila mtu amezaliwa na tabia fulani zinazomfanya awe katika kundi fulani.
-Kujifahamu kundi lako kunakuwezesha kurekebisha madhaifu uliyonayo na kuimarisha mazuri
uliyonayo. Pia inakusaidia kuwatambua watu wengine hivyo kukupa namna bora ya kuishi naohasa katika namna ya kuvumiliana na kuchukuliana katika madhaifu.
uliyonayo. Pia inakusaidia kuwatambua watu wengine hivyo kukupa namna bora ya kuishi naohasa katika namna ya kuvumiliana na kuchukuliana katika madhaifu.
Prepared by Mr.Intelligent kwa kushirikiana Sifaely Mdungu, Oliver Webillo KUTOKA SDA KANA ( Idara ya vijana ) 2017-2018 Chini ya Eliya Kisika ( Master-guide ) ; pia shukurani kwa kitini cha Modesta Richard na January Ndagala ( 23/07/2017).
" Nayaweza mambo yote katika Yeye anitiaye nguvu ".
*** N.B ***
MUNGU YEYE AMEWAGROUP WANADAMU KATIKA MAKUNDI KUMI NA MBILI ( 12 ) YA TABIA ###
Mathayo 19:28.
MUNGU YEYE AMEWAGROUP WANADAMU KATIKA MAKUNDI KUMI NA MBILI ( 12 ) YA TABIA ###
Mathayo 19:28.
• Maana hata Jiji la Yerusalemu mpya lina milango 12 .
• Kila mwanadamu aliyekombolewa , ataingia kupitia mlango ulioandikwa jina linaloendana na tabia yake. UFUNUO 21: 3, 10, 12.
• Kila mwanadamu aliyekombolewa , ataingia kupitia mlango ulioandikwa jina linaloendana na tabia yake. UFUNUO 21: 3, 10, 12.
" Nikasikia sauti kubwa kutoka katika kile kiti cha enzi ikisema , Tazama , maskani ya Mungu ni pamoja na wanadamu , naye atafanya maskani yake pamoja nao ,......
" , .... akanionyesha ule mji mtakatifu , Yerusalemu , ukishuka kutoka mbinguni kwa Mwenyezi Mungu.
Fungu la 12 linasema , " ulikuwa na ukuta mkubwa , mrefu , wenye milango kumi na miwili , na katika ile milango malaika kumi na wawili ; na majina yameandikwa ambayo ni majina ya kabila kumi na mbili za Waisraeli . "

• Mfano ## Wale walio na tabia ya upole na uvumilivu kama Yusufu , wataingia ndani kupitia mlango wao. ## Wale waliokuwa na tabia ya uzinzi na wasio na msimamo kama Reubeni, nao watapitia mlango wao .
( kila mwadamu lazima uwe kwenye kundi mojawapo hapo juu, japo tulio wengi tuna'share' tabia )
### Sorry ; Wewe upo katika kundi gani ? %% Be blessed.
Post a Comment