1. KUBALI KOSA: Usiendelee kumzungusha Wife wakati unajua umemkosea 🤫🤫.
2. OMBA MSAMAHA: Omba msamaha kwa kumaanisha hadi Wife ajue unajutia kosa 🙏🏽🙏🏽.
3. USIRUDIE KOSA LILELILE: Kurudia kosa moja kila wakati inamaanisha hakuna toba ya kweli 🙄🙄.
4. USIJARIBU KUJITETEA KWA KUMKUMBUSHA WIFE MAKOSA YAKE: Hata kama Wife alishawahi kukukosea na ukamsamehe; usilete hiyo mada hapo Brother! Wewe kuwa MPOLE tu ndugu yangu, shughulikia AGENDA iliyopo mezani 🤐🤐.
5. KIPINDI CHA TOBA MFANYIE WIFE VITU ANAPENDAGA: Wewe unajua anachopenda Wife wako; fanya kwa bidii kama sehemu ya toba. Mfano kumpikia (kama unajua lakini), outing, kusafisha nyumba, kumsaidia watoto, nk!! Mara nyingine ni ngumu kufanya haya mambo ila jitahidi iwe ENDELEVU 🌷🌷.
6. MWAMBIE WIFE AKUOMBEE: Yani akikubali KUKUOMBEA baassiiii; umesamehewa kabisaaa 😊😊. Unajua mtu hawezi kukuombea kwa MUNGU pasipo kukusamehe kwanza 👌👌.
✨NB:
📌 UKIKAA VIBAYA NA WIFE KILA KITU KINAGOMA!
📌 Happy WIFE... Happy LIFE!!
1 PETRO 3:7; “Kadhalika ninyi WANAUME, kaeni na WAKE ZENU kwa AKILI; na kumpa mke HESHIMA, kama chombo kisicho na nguvu; maana wao pia ni warithi wa neema ya uzima, ili MAOMBI yenu YASIZUILIWE na chochote.”
Post a Comment