WANAUME TUNA KANUNI HII , HEBU SOMA HAPA - EDUSPORTSTZ

Latest

WANAUME TUNA KANUNI HII , HEBU SOMA HAPA

Wanaume wana kanuni moja, nataka nikukumbushe shuleni, kwa wale wahenga kama mimi na mliopitia shule za mchanganyiko nadhani mnajua hili, lakini kwa wale wa shule za siku hizi kiingereza kingi sijui hata kama mnafanya. Ukihamishiwa kwenye shule mpya wewe mgeni mgeni unahakikisha unatembea na ma slay quen wote kabla hawajakuzoea na kujua tabia zako. Lakini kama akija binti mgeni basi unakuta wanaume mnajipanga kila mmoja kuona kuwa ni nani wakwanza kumpata huyo binti.
Haimaanishi ni mzuri sana, mnampenda sana au chochote kile, lakini inamaanisha heshima tu kuwa mimi ndiyo wa kwanza. Hali hii ipo pia kazini, mwanaume kicheche mzuri akihamishiwa ofisini au hata mtaani, kitu cha kwanza nikuangalia wadada wazuri wote na kuhakikisha anatembea nao, nirahisi kwa wanawake kumkubali mtu mpya kwakua hawajamzoea na hawajajua tabia zake mbaya, mpaka wanstuka kashetembea na mtaa au ofisi nzima.
Hivyo kama uko ofisini kaja kijana hata mwezi hajamaliza kashaanza kukutongoza basi jua kuwa yuko kwenye huo wito wa kiuanaume, acha kudanganyika eti kakuona wewe sijui mzuri na ahadi zake nyingi. Hujiulizi kwani huko alikotoka hakukua na wanawake mpaka akuoe wewe? ishu iko hivi, kama wewe umempenda kweli, hembu mpe muda, mkatalie kwanza na muangalie, kama akiacha kutongoza wengine basi anaglai huyo kakupenda kidogo wewe, lakini kama ni wale wa wito basi ukimkataa atafuata mwingine, na mwingine na mwingine.
Lakini kuna wale akina dada mnafika sehemu, ofisi au mtaani mnaanza kujiona kuwa nyie ndiyo wanawake tu, unakuta ofisi nzima inakutongoza au kuna jamaa anakuja kwa kasi,a najifanya kukupenda, anataka hata kukuoa, anataka hata kutambulishwa kwenu, dada yangua cha ufala, huyo ndiyo yule ambaye kila msichana mpya akija ni lazima atembee naye kwa heshima ya ofisi na kizazi cha mafisi, hivyo usisherehekee na kudhani kuwa wasichana uliowakuta hawana mvuto hapana hata hao washapitiwa basi wanakuchoraa jinsi unavyojiozesha!




Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz