Wanaume kaka zangu na shemeji zangu na wanangu wa kiroho nataka leo nizungumze na nyie. MWANAMKE NI MWANAMKE TU


Narudia MWANAMKE NI MWANAMKE TU
Hata awe Raisi
Awe Waziri
Awe na pesa za dunia nzima
Awe na influence kama zote
Awe na ujasiri na nguvu kama simba
Awe na PHd na amesoma mpaka mwisho wa vitabu
MWANAMKE NI MWANAMKE TU
:
Akipendwa
Akithaminiwa
Akitunzwa
Ukimjali
Ukiheshimu hisia zake
ANATULIA TULI, Analegea kabisa, hafurukuti, atakubeba hata mgongoni ukitaka.
Ukiona mwanamke anafanyiwa haya yote na bado haeleweki jua ana mapepo au ana shida kichwani au hakukupenda in the first place. Lakini any average woman ukimfanyia hayo aisee utafurahi. Njia rahisi ya kumshusha na kumnyenyekeza mwanamke ni KUMPENDA. Sio kumpiga wala kumnyanyasa wala kumpelekesha kibabe.
:
Mimi sio mwanamke wa mchezo mchezo lakini kwa yule Baba sikohoi. Mimi ni mwanamke ninayeweza kusimama kwa ujasiri nikasema Mwanamke anayependwa:
ANACHANUA
ANAKUA NA ADABU
NI RAHISI KUSUBMIT
ANAKUA NA AFYA YA MWILI NA AKILI
*Mpaka Leo bado napewa hela ya sokoni
*Mpaka leo bado napewa hela ya saluni
*Mpaka leo bado ananunua nguo za ndani na nguo nyingine
*Mpaka Leo bado nabebewa pochi
*Akipata nafasi anatupikia na kusaidia kazi
*Mpaka leo bado nashikwa mkono kuvushwa barabara. Kwake mimi sio mke tu, ni mtoto wake.
*Mpaka leo bado naambiwa I LOVE YOU mara nyingi sana kwa siku (hii ni dawa aisee)
*Mpaka leo bado hafanyi chochote bila kujua opinion yangu
*Nalindwa sana.
*Natetewa sana
*Narekebishwa kwa upendo kama binadamu sio kwa vipigo na matusi
*Nasamehewa kila siku
*Ananiamini na amenipa uhuru na nafasi ya kufanya Mungu alichonijalia kufanya bila masharti
*Napewa nafasi ya kuchangia maamuzi yote na vingine siwezi kuandika.
👇
Ninafanya kazi, nina uwezo wa kununua nguo yangu ya bei yoyote, nina uwezo wa kwenda saluni yoyote lakini hata siku moja:
*Sijawahi kuambiwa nitoe hesabu ya matumizi ya hela yangu
*Sijawahi kuhitaji hela nikaambiwa na wewe si unapata tumia zako
*Sijawahi kuambiwa jambo fulani na fulani ni jukumu lako kwa sababu na wewe unaingiza pesa.
👇
NA KWA SABABU NINAJISIKIA NIKO KWENYE MIKONO SALAMA
*Simuachii majukumu yote, ninamuhurumia na sitaki achoke. Najigawiaga mwenyewe cha kufanya ndani ya nyumba
*Natoaga ripoti zote mwenyewe tu bila kuulizwa
*Kujishusha na kuomba msamaha ni jambo rahisi
*Siwezi kuona jambo la Mume wangu nikakunja mikono tu, nitalipigania mpaka lifanikiwe hata kama sijaombwa
*Ninampenda mpaka sijielewi. Kama kuna mtu siwezi kuvumilia nikimuona hana furaha ni Mume wangu. Nitapigana kufa na kupona na chochote kinachomyima furaha
👇
HEBU MPENDE MKEO, MPENDE KWA LUGHA YAKE ANAYOELEWA, PANDA MBEGU NJEMA KWENYE MAISHA YAKE, YAANI MAVUNO NI MARA MIA YA ULICHOPANDA!
Thumbs up to my Husband Pastor Nick Shaboka Jr.


0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post