*VIJANA TUKUMBUSHANE JAMBO KIDOGO HAPA.*👇👇 - EDUSPORTSTZ

Latest

*VIJANA TUKUMBUSHANE JAMBO KIDOGO HAPA.*👇👇


Uchumba ni nini?
Uchumba ni hatua ya mpito kuelekea kuoana. Watu wawili wa jinsia tofauti wakikubaliana kuishi pamoja kama mume na mke katika siku za usoni huanzisha mahusiano yanayoitwa uchumba. *Uchumba si ndoa.*Katika uchumba mahusiano ni ya kirafiki yasiyohusisha kujamiiana. Uchumba ni hatua ya msingi ya ndoa. Makosa yakifanyika katika uchumba yanaathiri ndoa. Kwa hiyo ni muhimu kufanya maamuzi kwa makini katika uchumba. Huu ndiyo wakati ambao mtu huweza kudhani vyote ving’aavyo ni dhahabu wakati vipo vinavyong’aa ambavyo si dhahabu kabisa.*
*ZINGATIA HAYA HAPA:👇👇*
1.Ili umwite MTU mchumba wako lazima awe amefahamika nyumbani (pande zote mbili yaani kwa wazazi/ walezi) mtambulishane na kama utambulisho bado huyo ni rafiki bado, zingatia unaweza kuwa na marafiki hata 100 lakini mchumba ni 1 tu, hakuna wachumba zaidi ya 1) USISAHAU.
2. Tunajua wote ya kwamba ndoa ni MUNGU+MME+MKE!
Ndoa hujengwa na upendo, (Mme), Utii, (mke), Msamaha, pamoja na uvumilivu! N.k
3. MUDA WA UCHUMBA ni muda wa kumalizia mipango si muda wa kujuana tabia, (utakuwa umechelewa) muda wa kujuana tabia ni muda wa URAFIKI tena urafiki wa kawaida sababu binti ukisha mwambia tu nataka kukuoa kabla hujamfahamu vizuri zile tabia zake mbaya atazificha nawe utamuona ni mwema lakini ukisha muoa ndipo zinajitokeza na hapa ndipo migogoro huanza!(KWA UFUPI ANAFICHA MAKUCHA NDANI YAANI ANAKUWA MPOLE HUJAWI ONA) KUWA MAKINI, MUNGU KWANZA KWA KILA JAMBO INAPASWA IWE KAULI YAKO KATIKA VITENDO SIYO MANENO.
4. Ni vyema muwe marafiki sababu mkiwa marafiki atakua wazi (open) sana kwako hataweza kukuficha kitu si anajua wewe ni rafiki tu hivyo akiwa wazi ndio utajua tabia yake, bada ya hapo uamuzi ndo uchukuliwe kwa kadri ulivyoridhika nae!
Kamwe kijana asimchague binti kwasababu ya mwonekano wake wa nje Bali apendezwe na kuvutiwa na vyote alivyoona yani sura, umbo na tabia yake halisi yaani (si ya kuigiza kama walivyo wengi siku hizi) hivyo ukipenda, penda vyote usibague kimojawapo utapata tabu MAANA MAIGIZO YAMEZIDI KWA MABINTI WENGI LEO. Na msitumie macho ya kibinadamu tumieni macho ya rohoni ndio salama! ZINGATIA.
5. KUPIMA UVUMILIVU!
Ndoa ni kuvumiliana, kuchukuliana udhaifu sasa ni muhimu kujua kama mwenzako ana uvumilivu na kiasi? Ziko njia nyingi ila mimi nakupa rahisi na zisizo na madhara!
Mfano:
a) Kama mchumba wako anapendelea chips mayai, piza, baga, chips kuku n.k akija aidha kujitambulisha nyumbani siku hiyo mpikie Ugali tena wa dona na matembele, uone atalipokeaje hilo? Wapo wengi huringa wakisema hawali ugali wengine husema makoromeo yanauma kumeza ugali utawajua tu kwa matendo yao. Hata kama hujampikia unaweza pia kumuuliza vyakula anavyopenda UTAMSIKIA TU.
b) Kama una gari siku moja liache gari nyumbani na mtembee kwa mguu uone je atavumilia hata hali ikija kubadilika mkiwa katika ndoa? Wapo wadada hata kutembea 2Km hawawezi kabisa yaani akijitahidi mita 100 anataka bodaboda chunga sana KIJANA japo pia wapo VIJANA WAVIVU pia hata nao kutembea hawawezi siju nani atamwongoza mwenzake.
c) Wakati mwingine unaweza usitimize ahadi uliyomwahidi kwamba utamfanyia jambo zuri mwambie mpenzi samahani nilitamani kufanya hivyo lakini imeshindikana! Je atakudharau kwamba umeshindwaje kutenda? HILO NALO LITAZAME VYEMA KATIKA UVUMILIVU MAANA KUVUMILIA NI KUJIKANA NAFSI.
d) Kama ni mambo ya pesa alikuomba mwambie mpenzi leo Sina nimejitahid lakini sijafanikiwa kupata imeshindikana uone atalichukuliaje hilo? Hata mkiwa kwenye ndoa siku umekosa je atakutia MOYO? Je, anajua kama kuna kukosa na kupata na siku ukikosa atakuvumilia? Maana wapo MABINTI wao ukiwaahidi anajua ni kupata tu hilo la upande wa pili haelewi ukimwona wa hivyo chukua TAHADHARI mapema.
Wakati mwingine unaweza kumpa pesa uone vitu atakavyonunua ni vya bei gani ndogo na kubwa au kubwa tu. Kutumia pesa vizuri ni jambo la msingi kasivyo utaoa mfujaji wa mali nyumbani.
Kamwe mwanadamu hawezi kujua tabia ya mwanadamu mwenzake kwa 100% isipokua Mungu pekee, lakini zipo zile zinazoonekana na tunazoweza kuzijua ni vyema kuzijua sababu ukijua tabia Ya mchumba wako, itakusaidia wewe kuishi nae vyema kwa Amani na Furaha
Ndoa ni *UVUMILIVU* sababu hakuna alie mkamilifu kati ya wawili hao!
Kumbuka👇👇
*Nyumba na mali ni urithi apatao mtu kwa babaye; Bali mke mwenye busara, mtu hupewa na Bwana.*
Mithali 19:14
*Bwana wa Baraka nyingi akubariki unapojifunza kwa jili ya Utukufu wa Jina Lake.*
🙏🙏🙏🙏
TAFAKARI NJEMA.




Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz