Unapokuwa kwenye mahusiano na mtu haya ndio mambo ya muhimu ya kuzingatia katika mapenzi yenu; Ijue vizuri familia ya mpenzi wako Unapokuwa na mpenzi na umempenda kwa moyo wote na una malengo naye ya kuwa mume na mke hapo baadae. Unapaswa kuijua vizuri familia ya mpenzi wako kuanzia baba, mama na familia kwa ujumla kama ana dada, kaka au wadogo zake.
Ni vizuri ukiwa unawatembelea kwenda kuwa salimia mara kwa mara ili kujenga mahusiano mazuri na familia ya mpenzi wako hata kama hawataki uolewe/kuoana na wewe utagundua dalili mapema kuliko kupoteza muda ya kuwa kwenye mahusiano na mtu ambaye familia yao haikutaki. Wajue marafiki wa karibu wa mpenzi wako Kujua marafiki wa mpenzi wako itakusaidia kumjua vizuri mpenzi wako kupitia marafiki wake wa karibu kwa kuangalia tabia za marafiki zake ambao muda wote wapo wote na kuwa siliana mara kwa mara. Ukiona mienendo ya marafiki zake sio mizuri basin a yeye atakuwa na chembe chembe za tabia kama zao maana kuna msemo unao sema “ukitembea na mwizi na wewe utakuwa mwizi ” kama tabia zao ni nzuri basin a yeye atakuwa mtu mzuri ingawa usimuamini mtu kwa asilimia zote.
Ujue nini anapenda na nini hapendi Ni vizuri ukimuuliza mpenzi wako anapenda nini katika maisha yake ya kila siku na nini hapendi itakusaidi kujua nini ukimfanyia atafurahi na nini ukimfanyia atakasirika hapo utakuwa makini ili msigombane mara kwa mara na mpenzi wako. Ujue anapo kasirika/furahaa anakuwaje Uwe nauwezo wa kumsoma mpenzai wako kipindi akiwa na furahaa anaonekanaje na akiwa amekasirika anakuwaje kwa sababbu anaweza kuwa amekasirika wewe unazidisha utani utashitukia kofi la uso.
Tuwe wachunguzi kwa wapenzi wetu ili kufikia ndoto zenu katika maisha. Ijue siku yake ya kuzaliwa Muulize mpenzi wako siku yake ya kuzaliwa na hakikisha huisahau au andika kwenye kitabu chako cha kumbukumbu ili siku ifikika unamkumbusha na kumnunulia zawadi. Wapenzi wengi wanajisahaulishaga kwa makusudi ili kuwa pima wapenzi wao kama wana kumbuka siku yake ya kuzaliwa ila wangine kweli wanasahau siku zao za kuzaliwa kutokana majukumu aliyonayo mpaka siku ya kuzaliwa inapita bila yeye kujua. Unaweza ongezea mambo mangine muhimu kwenye mahusiano….
Post a Comment