Usijione kwa sababu Wewe ni Mtoto wa Kike ndio unastahili kuwa pangu pa Kavu, ACHA UJINGA. Usifanye KUOLEWA ndio SULUHISHO la Matatizo yako, ndio SULUHISHO la UCHUMI wako.
Kuna mabinti sijui ni Uchovu au kukata tamaa, utawakuta wanalia na kuomba “Bwana YESU nipe mume nataka kuolewa, anachana Nywele kwa Mtindo mbalimbali ili Vijana wamuone, huo ni UJINGA.
USIOLEWE ili UKATUNZWE, OLEWA ili Kutimiza MAKUSUDI YA MUNGU, HUOLEWI ili Mtu AKUTUNZE, Unaolewa kwa sababu unataka kutimiza RATIBA YA MUNGU, Sio Unaolewa kwa sababu unaona pale Nyumbani WAMEKUCHOKA au maisha ni magumu, HAPANA.
OLEWA kwa sababu UNATIMIZA Makusudi na Ratiba ya MUNGU kwani Yeye amesema si vema mtu awe peke yake.
Post a Comment