Uonapo unalisukuma sana penzi lako na wala haliendi ujue kwamba KUNA KIZUIZI MBELE..

HABARI NA MATUKIO: Harusi ya Jeremiah Mayeye na Lightness Mayeye
Wahenga na misemo yao "USIMLAZIMISHE NG'OMBE KUNYWA MAJI PENGINE AMETOSHEKA"
🤣🤣🤣🤣 Uonapo unalisukuma sana penzi lako na wala haliendi ujue kwamba KUNA KIZUIZI MBELE... Mimi na wewe hatujui, Mhusika ni yeye ndiye anatakiwa kusema kama amechoka anataka kupumzika ama KUACHA KABISAA! Mahusiano ni Faraja sasa kama hayaleti Faraja UNAYASUKUMASUKUMA ILI IWEJE? Mtu anayekupenda haambiwi MPENDE FULANI automatically yeye mwenyewe anaji -tune kukupenda💃
Sasa kama wewe ndiye unayeona unalilinda penzi kwamba usipojishusha ama kumbembeleza HAMUELEWANI unangojea Malaika waje kukuzindua usingizini? Mwenzangu pengine wewe ushajijua kwamba huyo ni ROHO YAKO sasa nisije kukushauri uondoke UKAKATA ROHO🤣🤣
Mapenzi hayako hivyoo, Mapenzi yanahitaji UWAJIBIKAJI kama hawajibiki kukupenda unadhani hana upendo? UPENDO kila kiumbe anao tatizo ni wapi AUPELEKE UPO HAPO?
Sasa wewe jipe muda wa kuja kupendwa na wakati tayari yupo anayependwa, Kuna wakati kama Bin adam unapashwa uichangamshe akili yako mwenyewe, Yaani Uko kwenye Mahusiano na Mtu ambaye hataki muwe na AMANI kila kukicha wewe ni mtu wa kulitetea penzi ili liendelee halafu unatoka mbele za wenZio unasema UNA MUME?
Mwana Mume unae sikatai ila sio MUME🙋🏻‍♂
Wanaume tulivyoumbwa Wallah ni watu wa kubembeleza Wake zetu sasa watafute wanawake wenzio waulize inakuwaje wao wanapata huduma ya MBEMBELEZO ili upime huyo wako na wa wenzio ukipata majibu CHUKUWA HATUA... Maamuzi magumu YANAUMA🔥But mbele yana neno AFADHALI.
Stress at your own risk💪🏽


0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post