Unaweza kuwa mwanaume bora kabisa lakini ukashindwa kuuthibitisha ubora wako kwa sababu umeshindwa kumhendo mwanamke ulie nae - EDUSPORTSTZ

Latest

Unaweza kuwa mwanaume bora kabisa lakini ukashindwa kuuthibitisha ubora wako kwa sababu umeshindwa kumhendo mwanamke ulie nae

Unaweza kuwa mwanaume bora kabisa lakini ukashindwa kuuthibitisha ubora wako kwa sababu umeshindwa kumhendo mwanamke ulie nae,na pia unaweza kuwa mwanamke bora kabisa lakini ukashindwa kuuthibitisha ubora wako kwa sababu tu umeshindwa kumhendo mwanaume ulie nae.
Labda nikuambie kitu kimoja rafiki yangu endapo kama watu wa nje na wanaokuzunguka wanakupa sifa kedekede kuwa wewe ni mwanaume au mwanamke bora kwa kila jambo na huku mkeo au mumeo anajutia uwepo wako ndani ya moyo wake kwa matendo yako machafu na mabaya unayomfanyia,basi wewe si bora hata kidogo.
Mwanaume au mwanamke ubora wake huanzia kwa yule anaeishi nae ndipo usambae kwa watu wa nje ndugu jamaa na marafiki au jamii inayomzunguka,huwezi kuwa bora ikiwa mkeo kila leo anatoa chozi na chanzo ni wewe,huwezi kuwa bora ikiwa mumeo hana amani hana furaha ikiwa chanzo ni wewe,badilika.
Mbundason

Image may contain: 1 person, standing




Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz