UNAWEZA KUMFANYIA MWANAUME KILA KITU ANACHOKITAKA LAKINI BADO AKAKUACHA!


Unaweza kumfanyia mwanaume kila kitu anachokitaka lakini kama wewe hukujifanyia angalau kitu kimoja tu unachokitaka basi jua kuwa haitasaidia chochote. Asil
imia kubwa ya wanawake wanaoteseka katika ndoa ni wale wakuvumilia, anapigwa anavumilia, anapika na kupakua kila chakula anachotaka mwanaume, kwenye mapenzi anafanya kila staili na kila wakati anapotaka mwanaume, lakini utawasikia wanasema “Wanaume hawaridhiki!”
Husema hivi wakidhani tatizo ni wanaume, hapana tatizo ni wao wenyewe. Mapenzi ni kama chupa ya chai, kama iko tupu huwezi kumimina kikombe kikajaa, hembu kajaribu leo uone. Ili kikombe kijae nilazima wewe kwanza uweke kitu katika chupa hapa nikimaanisha ili mwanaume auone upendo wako na kuufurahia basi nilazima wewe ujipende kwanza ili uwe na chakumpa huwezi kumpa mtu kitu ambacho hata wewe huna.
Kama hujipendi umefikia hatua kila mtu anakuambia vumilia basi jua unamboa huyo mwanaume wako, hakuna kitu unachomfanyia ambacho atakifurahia kwakua huna furaha bali unamvumilia. Jifunnze kujipenda wewe mwenyewe kwanza, jaza chupa yako chai kwanza kabla ya kuamua kuwahudumia na watu wengine. Najua ushafanya kila kitu na huna furaha unajikaza tu hapo, hembu nikuulize kipi hujamfanyia mumeo kumridhisha?
Si anachelewa usiku unafungua na kumpashia chakula? Si anakupiga hata Polisi hupajui? Si michepuko yake inakupigia simu na unaona mpaka video za uchi na mapicha kibao na unaishia kuomba msamaha? Sasa bado hujajua tatizo ni nini? Unalia kwa ndani na yeye anaona hivyo unamboa ndiyo maana anaona raha zaidi kuwa huko nnje. Najua wote, mmefundishwa vumilia lakini kuvumilia bila upendo ni kazi bure, jifunze kujipenda? Ni lini ulikula chakula unachokitaka wewe! Nilini ulilala muda unaotaka wewe? Nilini ulijinunulia zawadi?
Ni lini ulijitoa out? Ni lini ulijiambia umependeza? Ni lini ulimuambia leo sisikii kufanya na sifanyi au ukamuambia leo nina nyege na wewe nakuhitaji? Ndiyo maana nakuambia kama huna furaha kabisa unaponunua Kitabu changu achana na sehemu nyingine soma sehemu ya NNE tu, ukishindwa nipigie! Kwa wale mnaokihitaji kinapatikana kwa elfu kumi tu, unalipia kwa M-Pesa No. 0742-381-155 au Tigo Pesa no. 0657-552-222 na unatumiwa kwa Whatsapp, E-mail au Facebook. Elfu kumi ni rahisi kuliko nauli ya kurudi kwenu huyo unayemvumilia akikuchoka.


0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post