UNAETEGEMEA KUOA AU KUOLEWA


1. Usioe au usiolewe kwa sababu rafiki zako wameoa au wameolewa.
🔥 Ndoa siyo mkumbo au mashindano.
2. Usioe au kuolewa kwa sababu ya umri kuwa mkubwa.
🔥Kinachoolewa au unacho oa siyo miaka ni wewe.
3. Usioe
au kuolewa kwa sababu ya Mali.
🔥Ndoa siyo Mali Bali ni maisha ya kiagano. Mali huisha na kupotea. Lakini Mali hutafutwa.
4. Usioe au kuolewa kwa sababu ya ukabila au ukoo.
🔥Huoi au huolewi na kabila wala ukoo .
5. Usioe au kuolewa kwa sababu ya elimu.
🔥Hauoi au huolewi na elimu, Bali mtu. Upo uwezekano MTU kuwa na elimu na asiye na maarifa vilevile.
6. Usioe au kuolewa kwa sababu ya huruma.
🔥Ndoa siyo kuhurumiana ni WITO. Mwenye huruma ni YESU peke yake.
7. Usioe au kuolewa kwa sababu ya kumpunguzia matatizo.
🔥Kama YESU asipo msaidia wewe ndiyo kabisa hutaweza kitu.
8. Usioe au kuolewa kwa sababu ujauzito.
🔥Ndoa ni ZAIDI ya ujauzito.
9. Usioe au kuolewa kwa sababu ya mlianguka katika zinaa.
🔥tubu anza upya na BWANA YESU.
Hakuna Amani kwa ndoa yenye msingi wa uasherati.
10. Usioe au kuolewa kwa sababu ya shinikizo la wazazi na rafiki.
🔥kumbuka ndoa utaiishi wewe na siyo wazazi au rafiki zako.
11. Usioe au kuolewa kwa sababu ya shamrashamra za harusi.😁
🔥Ndoa siyo maonesho kama ya sabasaba.
12. Usioe au kuolewa kwa sababu ya ugumu wa Maisha.
🔥ndoa siyo utapata nini bali unaenda kutoa nini na siyo kwenda kupunguza ukali na ugumu wa maisha.
13. Usioe au kuolewa kwa sababu ya kutaka kuleta heshima kwa wazazi.
🔥Ndoa siyo kuwaheshimisha wazazi au jamaa au wengine wanadai kusafisha nyota, Bali ni kibali kutoka kwa Mungu.
14. Usioe au kuolewa kwa sababu ya kufanya tendo la ndoa tu, ndoa ni ZAIDI ya hapo.
🔥 TENDO la Ndoa Kama ni wimbo basi ni korasi ila kuna beti kadhaa😁😁😁
15. Usioe au kuolewa kwa sababu ya hofu ya kumkosa huyo kijana au binti.
🔥Ni kosa la ufundi kukurupuka kuingia katika ndoa kwa kigezo cha hofu ya kumkosa huyo binti au kijana. Kama ni wako ni wako tu hata kama inakuaje.
kumbuka:
Mithali/Proverbs 19:14
[14]House and riches are the inheritance of fathers: and a prudent wife is from the LORD.
*Nyumba na mali ni urithi apatao mtu kwa babaye; Bali mke mwenye busara, hupewa na BWANA.*
Barikiwa na kipande hicho.
TUSIULIZANE LINI Kuoa au Kuolewa wakati kila mtu ana mipango yake na changamoto zake


0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post