UKWELI NI KWAMBA MWANAUME ANAWEZA KUBADILISHA DINI KWA AJILI YA MWANAMKE LAKINI MWANUME HUYO LAZIMA AWE HIVI KWANZA ...!

Mwanaume Ukiwa Unafanya Haya Usilalamike Mkeo/Mpenzi Akichepuka ...

NI KWAMBA; Mwanaume anaweza kubadilisha dini kwaajili ya mwanamke, lakini mwanaume huyo ni lazima awe amependa sana, ni wale wanaume ambao ukikohoa wanajamba, wale wanaume ambao hawaongei chochote na upendo wao unakua mwingi mpaka wakati mwingine unaboa, mwanaume wa namna hiyo huwezi kumfumania, narudia, ni ngumu sana kwa mwanaume wa namna hiyo kumfumania ukiangalia namna anavyokupenda.
Ninachotaka kusema hapa nikuwa, kama una mwanaume ni wa dini tofauti, na huna mpango wa kubadilisha dini kwaajili yake, kabla ya kubeba mimba yake, kabla ya kuendelea kupoteza muda wako basi achana na kuangalia maneno yake kuwa kakuahidi kwamba atakuoa, hapana, angalia matendo yake, je ni ya wale wanaume ambao wamechanganyikiwa juu yako au ni wale mabaharia ambao hata kujali hawajali.
Ni ngumu sana mwanaume kubadilisha dini kwasababu ya mwanamke, hata kama hajawahi kwenda Kanisani au Msikitini lakini kubadili dini ni ngumu. Ujinga ni kuwa utasoma hapa na utaenda kumuuliza tena, nasema ni ujinga kwani kama wewe ni msomeji wangu nilishasema acha kuamini mdomo wa mwanaume ambaye anafurahia kufanya ngono na wewe bali amini matendo yake, ukimuuliza atakupa jibvu unalotaka kusikia lakini matendo yake yatakuambia ukweli!


0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post