Mabinti wengi wameangukia kwenye matatizo kwa sababu ya mambo kama haya.
Fuatilia kisa cha Binti Morica.
Morica; Yaani naona uvivu leo kwenda shule, sijui kwanini. Na leo hesabu, nisivompenda yule mwalimu.
Mama; mwanangu haya maisha unatakiwa kukazana sana katika mambo matatu ninayo ona yatakusaidia.
Morica; Mama bhana najua unataka uanze kunipa semina, wakati mwingine semina zako zinakuwa ndefu.
Mama: Mtoto mwenye hekima humfurahisha baba yake, bali mwana mpumbavu ni mzigo wa mamaye. Unataka mimi ndo nichukue mzigo?
Morica; kwa hiyo Mama mimi ni mzigo? Mimi nishachoka na maneno na semi zako mama au unaniona mhuni?
Mama; Si hivyo mwanangu, jukumu langu ni kukuelimisha, ukiharibikiwa wewe wa kwanza kulaumiwa nitakuwa mimi na mimi sitaki kuaibika.
Morica; Sasa mimi nakuaibisha nini, au kisa nimesema sijisikii kwenda shule? Kwanza mafanikio hayapo kwenye shule. Mbona rafiki yangu mwajuma kafeli na ana salon kubwa ya kusuka?
Mama: Haya we jidanganye. Huyo Mwajuma unadhani katoa wapi hizo hela za kuanzisha salon? Halafu bahati ya mwenzako sio ya kulalia wahenga walisema mwanangu.
Ghafla sms inaingia kwenye simu ya Morica toka kwa mpenzi wake John fundi Magari.
John; Vipi Baby unakuja sasa hivi? Maana nishakununulia kiepe hapa, sosage. Fanya faster basi
Mama; Morica!!!! Vaa nguo uende shule sasa hivi!!!
Morica anamtumia John ujumbe mfupi…
Morica; Baby nakuja, Ila itabidi nimdanganye kuwa nipo kwenye siku zangu ili baadae nitoroke. Usijali baby. Nakupenda sana.
Morica alifanikiwa kutoroka na kwenda kwa mpenzi wake John akashinda huko hadi jioni wakala walivyoweza kula na wakati wakuondoka akafungasha chips kwenye mfuko.
Akawa mtoro shuleni, kila yakipikwa matembele kwao hawezi kula, anategemea John amtumie pesa ya chips na sausage ili aweze kula
Hadi anamaliza kidato cha nne Morica hakuwa mtu anayesikiliza ushauri wa Mama yake na tabia yake ilikuwa mwiba mtaa mzima. Kila akipewa pesa ya kufanya ujasiriamali na Mama yake alikula pesa yote.
Pesa alizokuwa akipewa na John yeye ndo akaonekana mrembo wa mtaa, kubadilisha nywele kila aina kupitia salon ya rafiki yake aitwae Mwajuma
John alikuwa akimtumia Morica kwa manufaa yake, pasipo Monica kujua kuwa alikuwa kaathirika na ugonjwa wa Ukimwi.
Siku moja John alimtamkia Morica kuwa hahitaji kuwa naye tena kwa kuwa alikuwa kamchoka na alihitaji kubadili mazingira.
Ikamuuma sana Monica, akakumbuka jinsi alivyo wanyanyasa kwa kuwatukana vijana wenye heshima zao mtaani kwa sababu ya John, alilia lakini aliamini atapata mpenzi mwingine si muda kwa sababu alikuwa mrembo kweli aliekimbiza mtaa mzima, na bado kulikuwa maombi ya posa ya kutosha.
Upole na ukaribu wa dini waliokuwa nao wazazi wake, uliwafanya vijana wengi wa kanisani wampaparikie lakini bado aliwajibu shiti.
Akajitokeza Kijana mmoja aliyekuwa akifanya kazi Mamlaka ya Mapato Tanzania, na bado alikuwa na maduka mengi Kariakoo, akampenda Morica na kuahidi kumwoa.
Maandalizi ya haraka yakaanza kufanyika, familia ikafurahia kuwa hakika Mungu ametujibu maombi yetu, binti yetu anaolewa na mtu mwenye hofu ya Mungu, mwenye uwezo wa kumpatia mahitaji muhimu.
Kila muda Mama Monica alimuita mwanae na kumwambia, najivunia kwa ajili yako mwanangu, ona ulivyoniheshimisha.
Ikafika hatua za karibu kufunga ndoa,
Mchungaji akawaita Morica na mumewe mtarajiwa Bw. Briton wakaanza safari ya kwenda kupima afya zao.
Muda wote Morica alikuwa mwenye furaha akiamini sasa ule ndio ulikuwa muda wake kumpelekea John gari yake akaitengeneze inapopata hitilafu.
Walipima na Daktari alitoa majibu kuwa mmojawapo wa wanandoa watarajiwa alikuwa tayari ameathirika ambaye ni Morica.
Mimi ninayeandika nikakumbuka ripoti zinazotolewa kwa sasa kuwa Tanzania ni moja ya nchi ambazo vijana wengi wanaongoza kujinyonga kutokana na masuala ya kimapenzi na mahusiano.
Nikiwa nawaza hayo bade ya saa tatu kupita nikasikia Morica amejinyonga baada ya kuipa fedheha familia yake kwa kugundulika kuishi na virusi vya Ukimwi.
Nikakumbuka alivyokuwa akijinadi pale mtaani, nikawaza hivi ile nguvu ya kujinadi angeitumia katika utafutaji asingefanikiwa? Ule muda aliotumia kushinda salon akijilemba angeutumia shambani asingevuna?
Nikagundua wasichana wengi wazuri wamesahau kuwa uzuri wao ni nguvu ya Mungu.
Wasichana wasiojitambua wamewekeza muda wao kwa ajili ya kuwafurahisha wapenzi wao kwa ajili ya vitu vinavyokuja kuwaliza huko baadae.
Kweli asiyefunzwa na Mamae hufunzwa na ulimwengu na mtoto mwenye hekima humfurahisha Babae ila mwana mpumbavu ni mzigo wa mamae.
U slay King na Uslay Queen haujawahi kumwacha mtu salama.
Post a Comment