UKIMCHUKULIA POA MPENZI WAKO USIDHANI KAMA ATAKUVUMILIA SIKU ZOTE

*Ukimchukulia poa mpenzi wako usidhani kwamba atavumilia siku zote. Kuna wakati mpenzi wako anajiona kabisa hafurahii mahusiano sababu wewe umekua ukimuumiza kila mara na kibaya zaidi usaliti umekua ni sehemu ya maisha yako. Cha kushangaza na kusikitisha ni kwamba tunawasaliti wale tunaojua wanatupenda tukiwa na dhana potofu ya kwamba hawawezi kutuacha. Utamuumiza vya kutosha! Utamsababishia vidonda vya kila aina moyoni! Utamkejeli, kumdharau pamoja na kumshusha thamani yake lakini siku akisema imetosha basi ujue imetosha kweli. Tuache uovu kwa wanaotupenda na tuwe sababu ya furaha yao.*


0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post