Mwanaume anapomuona msichana yeyote,yeye kwa mda wote huwa anafikiria mapenzi tu,ni kweli kwamba wanaume huwa wanavutiwa sana na wasichana,lakini sasa:kabla ya kufanya naye mapenzi hakikisha kwamba unajibu haya maswali yake vizuri na kwa ufasaha zaidi.
Hii ndiyo listi ya maswali ya kujibu kabla hujampata kisawasawa:
Je anastahiri vya kutosha kuwa mke wako?
Je huyo ni msichana wa kuoa tu au ni wakufanya naye mapenzi tu?Hili Ni swali zuri sana la kuuliza kabla hujafanya naye mapenzi.Lazima ufahamu majibu kwanza na mambo mengine yatafuata baadae.
Vipi kama akipata mimba?
Hili ni swali KUBWA sana.Je utafanya nini?Je utapenda au utachukia? Je ni yeye ambaye unandoto za kuwa mama wa watoto wako?
Je utafanya nini baada ya kufanya naye mapenzi?
Je ulikuwa unahitaji mapenzi tu? Je utaendelea na uhusiano au utamuacha?
Je unampenda kweli?
Oh, labda unamtamani.Unatamani kumchezea tu.Je unampenda? Hicho ni kitu cha muhimu sana kufahamu.Kitendo cha kufahamu kwamba unampenda au humpendi huufanya mwili wako kuwa na amani katika mahusiano yako
Je unaweza kumsapoti mtoto?
Kama akipata mimba,unaweza kumhudumia mtoto? Ni kitendo kibaya sana kufahamu matokeo ya kufanya mapenzi harafu ushindwe kumhudumia mtoto wako uliye mpata.
Kama anafaa kwanini usimuoe?
Kama ni mzuri kitandani,kwanini asifae katika maisha kwanini usisubiri na mkafunga ndoa kanisani na kuoana kabisa?
Inahitajika ushujaa wa kutosha kabisa kuweza kujibu maswali haya.Mwanaume halisi huyajibu haya maswali kwa ufasaha zaidi.Hata kama majibu yote yasiwe mazuri,mwanaume wa kweli anaushujaa wa kuweza kujibu maswali hayo kwa ukamilifu kabisa.Weka mawazo haya hakilini usije ukafanya makosa na kuvuruga uhusiano wako.
Post a Comment