👹SUMU INAYOUWA WANAUME.👿


Kuna Dada aliyechoshwa na maisha ya ndoa hata ikamlazimu kutaka kumuua mumewe.
Asubuhi moja alimkimbilia Mama yake na kumshirikisha azma yake ya kuchoshwa na manyanyaso ya mmewe, na mpango wake wakutaka kumuua. Lakini alihofia mkono wa sheria endapo akimuua aweza ozea gerezani, akahitaji ushauri wa mama yake.
Akasema "Tafadhali mama nisaidie kwa jambo hili". Mama yake akamjibu hivi; Sawa nitakusaidia binti yangu umuue mumeo bila kushtukiwa na yeyote.

Mama-- Niahidi kwamba utaushika ushauri wangu bila ulegevu. Binti akamuahidi mama yake "Nitazingatia mama". Mama yake akafurahia ila akamuonya kwamba jambo hili lina ugumu wake, Je? Utapambana kiujasiri hata utakapofanikisha kumuua, hivyo zingatia haya;-
(1)... Lazima uweke amani ya kweli na mumeo, ili atakapokufa watu wasikustukie kama umehusika.
(2)...Unatakiwa ujirembe na uwe msafi ili kumvutia na mwonekano wako uonekane kama dogodogo yaani msichana mbichi mbichi.
(3)....Unatakiwa umjali sana na uwe mwenye kumwelewa ili msigongane kimawazo.
(4)....Uwe mvumilivu, msikivu, mwenye mapenzi ya dhati, usiwe na wivu wa hasara hasara, umuheshimu sana na kumtii.
(5).....Tumia pesa kwa ajili yake na usichukizwe akikupatia pesa ndogo kwa matumizi yako, umshukuru kwa unyenyekevu.
(6)......Usiinue sauti yako unaposema nae, wala usimkosoe kwa dharau, bali zingatia maneno yawe ya amani na ucheshi yakijawa na penzi la kweli. Ili akifa wasikushuku.

Je. Utayafanya hayo? Mama akamuuliza binti yake.
Mama yake akampatia Unga unga fulani ambayo ndio sumu. Akamwambia "Tia hii sumu ndani ya chakula chake; Nayo itamuua pole pole na atakufa siku ya 90.
Baada ya siku 30 kupita binti alirejea kwa mama yake kumpa mrejesho wa kazi yake ya kumuua mmewe.
"Mamaaa mamaa tafadhali nimebadilisha mawazo SITOMUUA TENA MUME WANGU. Yaani amebadilika ananipenda kuliko, ananijali sana mamaaa, tafadhali nisaidie dawa ya kuiondoa sumu, akalia. Huyu ni mpenzi wangu chaguo la moyo wangu nisaidie mamaaaa".
Mama akamjibu binti yake; "Usiogope binti yangu, Ule unga unga haukuwa sumu, ila nilikupatia maziwa ya unga tu, sio sumu".
Ukweli ni kwamba wewe (binti) yangu ndiye ulikuwa sumu halisi ukimuua mmeo kwa tabia zako mbaya. Ulikuwa ukimuuwa taratibu.
Hivyo ulipoanza kumuenzi,kumfurahisha, kumpenda na kumtii mumeo ndipo ulianza kumtibia.
Wanaume sio dhaifu bali mahusiano yetu yanapopunguka ndiyo huwafadhaisha na kuanza kututesa.
Unaweza kumteka myo mumeo kwa Kumheshimu bila kinyongo, kumpenda kwa dhati, kumtii bila kumkosoa kwa kiburi Kiukweli 100% atakuwa wako.😅😂👂
.


0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post