Soma stori hii ujifunze kitu "Dada wa kazi akimweleza mume wangu siri hii, sina ndoa tena"

UTAMUZAIDIAPP

Mwaka jana mwishoni hubby na watoto walienda likizo kijijini kama utaratibu wa kila mwaka, nyumbani tukabaki mimi na msichana wa kazi, sikupewa likizo kazini, siku moja msichana wa kazi alinifuma na rafiki hapo nyumbani kwetu red handed na amelitumia suala hilo kama silaha dhidi yangu.

Kila Sunday huwa nampa ruhusa kwenda kanisani na nyumbani kusalimia, kwao ni hapa hapa mjini, huwa anaondoka asubuhi na kurudi jioni ya sa 6, hivyo rafiki yangu alinipigia simu kwamba tuonane hata kwa maongezi tu briefly, kwa kujua nipo alone home na kwamba ni maongezi mafupi nikamuomba rafiki aje nyumbani, kinyume na matarajio yetu tukashindwa kujizuia na kuanza romance ukumbini na baadae tukahamia bedroom kwa msichana wa kazi, niliona si vyema kutumia bedroom yangu.

Sijawahi kuelewa hadi leo kwanini huyu binti alirudi saa tisa badala ya jioni kama siku zote, ndani mwetu wote tulishagawana copy za funguo za geti dogo, hubby, mimi na hg, hivyo tukashtuka tu msichana wa kazi anafungua mlango na kuingia hivyo kutukuta kama tulivyozaliwa katikati ya suala lile.

Nilimgombeza sana kwa ukosefu wa adabu, maana badala ya kutoka nje akabaki humo anakodoa macho, then akatoka nje, nikajifunga khanga nikamfuata nikamuuliza kulikoni umerudi saa tisa? Hakujibu, hatukuongea kitu hadi kesho yake wakati naondoka kwenda kazini, nikaanza kumkaripia upya kuwa nisikie kasema chochote kwa mtu yeyote, cha kushangaza binti akaenda room na kurudi na begi lake kwamba anaondoka na atampigia simu daddy kumueleza alichoona, na hapo kanishikia kiuno, ikabidi nijishushe nimpigie magoti, nikambeleza sana na kumpa laki moja, akakubali kubaki.

Tangu hapo amekua mwiba mkali kwangu, mara leo aseme anataka smartphone namletea, kesho anataka laki, next day, laki mbili, vyote hivyo natoa kwa kuogopa kuvunja ndoa yangu, lakini zaidi ya yote, akimweleza hubby jambo hili ni wazi hata mimba hii anaweza kushtuka sio yake na ikawa shida kubwa kwangu.

Naombeni msaada kuhusu huyu msichana wa kazi nimfanyeje?
Nimechoka kuwa mtumwa, maana suala hili ni tangu December last year hadi sasa, utii wake umepungua sana, ni dharau tupu na nikimuona na wenzie wa hapa mtaani nakua na hofu sana kuwa atawapa umbea.

Sijawahi kuisaliti ndoa, safari hii ni huyu rafiki ndio alinirubuni tukaanzisha uhusiano huu, nilishindwa kukataa maana ndie mpenzi wangu wa kwanza na wa mwisho kabla sijaolewa sijui tulianzishaje suala hili.



0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post