Mwaka jana wakati nanunua Kitabu chako nilikua ni mtu wa kupigwa tu kila siku, mume wangu alikua akinipiga kwa sababu za kijinga jinga. Hata nikipigiwa simu na mchepuko wake nikautuikanana alikua akija na kunipiga kwanini nataukana watu kwenye simu. Sikua na pakukimbilia, hakua akitaka nifanye kazi hivyo nilikua mtu wa kukaa nyumbani ingawa hata matumizi alikua hanipi.
Nakumbuka niliponunua Kitabu chako nilidhani kitanisaidia lakini hakikunisaidia, nilipoongea na wewe uliniambia mimi ndiyo natakiwa kubadilika na si mume wangu. Sikujua namna ya kubadilika ukaniambia kitu cha kwanza ni kukataa kupigwa, kwangu ilikua ngumu sana kwani nilikua namtegemea kwa kila kitu hivyo niliwaza nitafanya nini ili nisipigwe wakati hata ukimuangalia tu anaweza kusema umemuangalia vibaya.
Nilishashitaki kwa kila mtu lakini hakuna hata mmoja ambaye aliweza kunisaidia. Uliniambia naweza kwenda Polisi na kama ananitishia kuhusu watoto basi niwaambia huko huko kuwa anawatishia na watoto hivyo naogopa kuondoka. Nilikuongea na Mama yangu aliniambia kuwa unanidanganya huyo ni mume wangu siwezi kumpeleka hospitalini nivumilie. Lakini siku moja alinipiga akanivunja mfupa wa pua.
Alinifungia ndani tena chooni kwa siku mbili bila hata chakula. Nilipotoka sikusubiri kufia ndani, nilivizia ametoka na kwenda Polisi, niliwachukua wanangu wawili ambao nao huona Baba yao akinipiga na kuwaambia kuwa mume wangu ananipiga, sina pakwenda kwani nahofia uhai wangu. Yeye alikua ameenda kazini wakati hio na baada ya kuonekana kwenye hali ile walienda kumchukua kazini kwao.
Alikamatwa na kuwekwa ndani lakini lilipokuja suala la kufungua kesi nilijikuta naogopa, nilikataa kutoa ushirikiano kwani aliniomba sana msamaha. Nilikua naumia na kudhani kama kwakua kafikia hatua ile basi atabadilika, nilijikuta namsamehe, ndugu zake waliniomba msamaha na ndugu zangu walinisihi nisiendelee na kesi kwani nikijidhalilisha. Kweli yaliisha na tukarusi nyumbani, alibdilika kwa wiki moja kisha akaanza kurudia katika hali ileile.
Saa akiwa na hasira zaidi kuwa nimempeleka Polisi, kusema kweli nilichoka kupigwa, nyumbani hawakua na msaada wowote na mume wangu hakua akinijali tena. Nilipoongea na wewe uliniuliza kwani nina matatizo gani, si nina mikono miwili, mbona kuna watu wengi wanaishi wakiwa single mother. Kusema kweli Kaka ulinipa ujasiri, nilikua na kaakiba kidogo nikaenda kutafuta chumba cha elfu ishirini, nililipia miezi mitatu.
Siku moja alirudi nyumbani akiwa kalewa.alikua akitukana sana na ilionekana kuna kitu kilikua kinamchanganya. Sikumuuliza kwani nilijua ukimuuliza ni kipigo. Nilimtengea chakula, kikiwa mezani wakati anakula aliniambia nichamoto sana niende kumpoozea, wakati nasoge karudu na alipokua amekaaa, alichukua sahani ya chakula na kunirushia, kwa bahati niliiona hiyo sahani, niliikwepa. Ile sahani ilidondoka chini na kuvunjika, hapo ndipo nilikiona cha motro, alinivamia na kunipiga huku akinitukana.
Wakati akinitukana ni kama alikua anatukana mchepuko wake, kwania likua akiniambia wewe si uemamua kuondoka, nimekufanyia mambo kibao, nimekujengea lakini umeniacha, saa nakuua. Alinipiga sana, mwanangu mkubwa alitokeza kuamua lakinia limpiga mwanangu mpaka mtoto akazimia, hapo ndipo alishtuka, akatoka na kufuinga mlango kwa nnje ili tusitoke. Ilikua nmi usiku wakati huio nilikua sina simu kwani alishaninyang’anya, basi nilimuangalia mwanagu kazimia kwa masaa matatu, namwagia maji lakini hazinduki baadaye ndiyo akazinduka na tulikaa vile mpaka asubuhi, hakurudi nyumbani.
Asubuhi alikuja Mama yake, nadhania likuja kuangalia kama mtoto amekufa au la, alimuona yuko salama ndiyoa kmpigia simu mume wangu. Mume wangua lirudi na kujifanya kuomba msamaha huku akiniulaumu mimi kwa kumkairisha. niliamua yu kumuambia mume wangu nimechoka naondoka, hakuamini, alijaribu kunitishia watoto nikamuambia mimi sina shid ana hilo. Watoto wetu niwakubwa kidogo hivyo tunaweza kwenda polisi na ustawi wa jamii ili wao ndiyo waamue kama wanakaa na Mama yao au la. Alijua hatashinda na nilijua kabisa alikua hawataki, lengo lake lilikua ni kuniumiza tu ila sikua tayari kuendelea kuteseka kwasababu hiyo.
Niliondoka na watoto na kwenda kuishi nao, sikua na kazi yoyote ile ila nilipoongea na wewe uliniambia naweza kuanza kwa kuuza uji. Ulinishauri vizuri na kweli nilianza kuuza uji, kuna Kaka yangu mmoja niliongea naye akanipa kama laki moja. Hiyo ilinisaidia kununua vifaa na chakula cha watoto. Nilianza biashara ya uji, ukaniambia niuze pia na Karanga na kwakua nina muda nijifunze kupika Crips.
Nilifanya hivyo nikajifunza pia kupika Popcon kwakutumia jiko la mkaa. Taratibu maisha yangu yalianza kusimama, mume wangu hakua akihudumia watoto akiniambia kuwa hajawahi kunifukuza kama nimeshindwa kuwahudumia basi niwarudishe kwake. Sikuumizwa kwa hilo kwani angalau kipato nilikua nimekitapa. Nina miezi sita sasa tangu nitoke kwa mume wangu, ninafanya biashara kuanzia ya Vitafunywa, uji, Popcorn na kila kitu.
Pia nauza mashuka ya mitumba, nashukuru Mungu ninaweza kulipa kodi, sijapata kikubwa lakinia ngalau nina amani. Kila siku mume wangu ananisumbua kuhusu watoto lakini nimemuambaio kama anawahitaji tukamalizane kwenye sharia. Ananipiga,a natesa watoto na sipo tayari kuona akiniulia wanangu. Nilikua tayari kufa, nimeshazoea lakini nilpomuangalia mwanangu kwa masaa matatu amelala hanyanyuki nilijua ni wakati wa kuondoka kwani ataniua, nashukuru sana kitabu chako kinanisaidia, nina furaha na maisha yanaendelea.
MWISHO
Post a Comment