SEHEMU 20 ZA MWANAUME AMBAZO WASICHANA WANAZIPENDA SANA.SOMA HAPA KIJANA NIKUJUZE.


Image may contain: 2 people, people smiling


Kutoka katika misuli ya mwili,kifua,unavyocheka hakili yako au kwa maana nyingine kujitambua,wasichana wanaelezea mambo ambayo wanapenda sana kutoka katika mwili wa mwanamme.

Kama ukimuangalia msichana machoni unapokuwa mtaani kwako,au kama mmetoka na msichana wako kwenda kwenye matembezi ya kimapenzi(out),au ukiwa umekaa na msichana au mpenzi ambaye mmeoana kwa muda mrefu,najua umekuwa ukijiuliza kwa muda mrefu sana kwamba mpenzi wako amekupendea nini na umemvutia kwa kitu gani kimuonekano mpaka akakubali kuwa mpenzi wako?

 Kutoka kwenye mwili wako mzima mpaka ndani ya suruali yako umekuwa ukijiuliza ni sehemu zipi wasichana hata kabla ya kuwa mpenzi wako huwa anapenda sehemu zipi?

 sehemu gani ambayo mwanamke au msichana wako huwa anachanganyikiwa sana mnapokuwa uso kwa uso,kifua kwa kifua au mkiwa kwenye mashuka? 

Haya ni maswali ambayo wanaume na wakaka wengi huwa wanajiuliza sana linapokuja swala la kumpenda msichana.

Kwa App ya Mapenzi; udaku na michezo»»BOFYA HAPA KUPAKUA APP ISIYOTUMIA DATA NYINGI

Tuliwauliza wasichana 25 kutoka katika historia tofauti ya maisha yao,sehemu walipozaliwa,na tofauti ya mitindo ya maisha yao kuelezea ni sehemu gani ambazo wasichana wanapenda sana kutoka kwa mwanaume.


Kwa mujibu wa mwanamke au msichana yeyote yule sehemu inayomvutia sana kwake inaweza kutokana na sehemu mbili ambazo ni moja ni;kuzaliwa na ya pili ni ile ambayo inatokana na mazoezi kama "Gym nk".Ndio unaweza ukashangaa lakini ndio hivyo wasichana walitupa maoni yao kulingana na kile wanachokipenda kutoka katika mwili wa mwanaume.


MSICHANA 1:


" Ninapenda sana muonekano wa TUMBO la mkaka hasa linapokuwa "FLAT " na sio kitambi"-Pilietta


MSICHANA 2:
"Ninapenda mwili wote wa mwanaume,lakini ukiniambia nichague sehemu ninayoipenda zaidi ni mi ninapenda MIKONO ILIYOJAA VIZURI na inapokuwa mizuri basi mimi nasikia raha"-Christina


MSICHANA WA 3:
"Mimi ninapenda mwanaume ALIYEJAA MIKONO vizuri,hasa hasa anapokuwa na mgongo mpana kwangu mimi nachanganyikiwa kabisa,huwa najihisi kuwa na amani na furaha sana ninapokuwa na mkaka mwenye mgongo mkubwa"-Sarah G


MSICNA WA 4:
"Mimi napenda mkaka mwenye VIGANJA VIKUBWA hali hii hunifanya nifikile kwamba mkaka huyu anaweza kufanya mambo vizuri kwa sababu ya kuwa na viganja imara na nguvu za kutosha."-Julia


MSICHANA WA 5:
"Mimi napenda mkaka mwenye TABASAMU ZURItabasamu huwa linanifanya moyo wangu unayeyuka kabisa kama barafu ndani ya maji ya moto"-Mariamu


MSICHANA WA 6:
"Mimi napenda mwanaume mwenye nguvu yaani aliyejaa mikono vizuri na mwenye mabega mapana na yaliyojaa vizuri,ili aweze kunibeba si unajua tena mambo ya mapenzi"-Lydia


MSICHANA WA 7:
"Mimi napenda mwanaume mwenye MACHO MAZURI macho mazuri hunifanya nichanganyikiwe kwa kumuangalia tu"-Anna


MSICHANA WA 8:
"Mimi napenda mwanaume mwenye MAKALIO MAKUBWA KIASI asiwe mwembamba sana,ninapenda makalio na sijui ni kwa nini nimejikuta ninapenda tu"-Sarah


MSICHANA WA 9:
"Mimi ninapenda wavulana wenye umbo la "V" katika matumbo yao na lazima mwanaume ninaye mpenda mimi awe ni mtu wa mazoezi"-Elizabeth


MSICHANA WA 10:
"Mimi napenda mkaka mwenye TABASAMU ZURI basi"-Recho


MSICHAN WA 11:
"Mimi ninapenda mwanaume mwenye Kifua kipana na kilicho jaa vizuri"-Fatumah


MSICHANA WA 12:
"Kwa upande wangu mimi ninapenda mwanaume mwenye mikono mikubwa ya kuweza kunibeba huku na kule kunapokuwa kwenye mambo yetu yale"-Mwajumah


MSICHANA WA 13:
"Mimi napenda mwanaume mwenye misuli imara sana na yenye nguvu kuanzia chini mpaka juu ila asikomae sana jamani"-Brigite


MSICHANA WA 14:
Msichana wa kumi na nne naye alisema kwamba anapenda sana wakaka wenye mikono mizuri


MSICHANA WA 15:
Msichana wa kumi na sita naye pia alisema kuwa anapenda wakaka wenye vifua vikubwa.


MSICHANA WA 16:

"Hahaha swali lahisi sana kwangu hilo,mimi napenda mkaka mwenye mikono mikubwa na iliyo jaa zuri na tumbo lililokaza vizuri".-Tunuh

Kwa App ya Mapenzi; udaku na michezo»»BOFYA HAPA KUPAKUA APP ISIYOTUMIA DATA NYINGI
MSICHANA WA 17:

"Mimi ninapenda sana wakaka wenye makalio makubwa kama vile wakaka wanavyopenda wasichana wenye makalio makubwa"-Vanessa.

MSICHANA WA 18:

"Mimi ninapenda wakaka wenye tabasamu zuri hasahasa anapokuwa na meno maeupee! yananivutia sana jamani"-Eliza J.B

MSICHANA WA 19:

"Mimi ninapenda sana mwanaume mrefu kwa sababu mimi ni msichana mrefu kidogo kwa hiyo huwa sipendi kumzidi urefu mpenzi wangu ndio maana napenda wakaka warefu"-Paulinah

MSICHANA WA 20:

"Mimi napenda mkaka awe na mwili msafi siangaliii kifua wala mikono wala nini,ila mimi napenda awe mtanashati"-Mwavua.

Kwa App ya Mapenzi; udaku na michezo»»BOFYA HAPA KUPAKUA APP ISIYOTUMIA DATA NYINGI
Previous Post Next Post