Umemwangalia machoni na kumsoma lugha ya kimatendo na ishara ya mwili, ukamsogelea kwa mbwembwe huku ukijiamini na kumsalimia ukiwa unamchombeza kwa maneno mazuri ya hapa na pale na kuyafanya maongezi kukolea na kuzidi kuwa matamu, mwisho mkabadilishana namba za simu, baada ya hapo na muda kupita unajikuta ukiwaza uandikeje ujumbe mfupi wa meseji utakaomtumia huyu mrembo mliokutana kwa mara ya kwanza anaekugusa moyo ili umfanye aongezea mvuto zaidi kwako, umuandikie meseji gani kumchanganya zaidi kihisia, na ni nini cha kuandika kwenye meseji yako ya kwanza kwa huyu kimwana?.
Hakuna hisia nzuri kama ya kupata namba ya msichana uliyevutika naye, hii hisia inakuwa mahara pake na inasisimua zaidi iwapo msichana mwenyewe ndie aliyekupatia hio namba yake na ujumbe wako mfupi wa kwanza ndio utakaokupatia ufumbuzi kama ataendelea kuwa anakujibu meseji zako au vipi, na iwapo kama mvuto wake utaongezeka kwako au la, na kujibiwa kwa sms zako inategemea zaidi na jinsi na mazingira ya wewe ulivyoipata hio namba, iwapo hukuonyesha hisia wakati unaomba hio namba, na uliiomba hio namba kama rafiki, atakuchukulia kama rafiki daima na kubadilisha hio hali ya kundi alilokuweka kama rafiki ni ngumu mno hata kama unaujuzi wa hali ya juu kumrubuni kwa ujumbe fupi itakuwia vigumu kidogo kufanya hivyo, kwahiyo wakati wa mazungumzo hakikisha unaweka wazi japo bila kumweka wazi moja kwa moja, tumia maneno kumuelekeza uendako ila usiwe wazi ya kuwa unamtaka.
Iwapo namba hiyo umeipata kwa rafiki zake au watu wake wa karibu tegemea mambo kwenda kombo, ni mara chache sana na mara nyingi haiwezekani kuweza kumuhamasisha msichana kihisia wakati hujawahi kuongea naye na kwanza kile kitendo pekee cha wewe kutafuta namba yake kwa njia ya panya kunakufanya uonekane wa ajabu kwake kama mtu usiyejiamini mwenye wasiwasi na kutokuwa na msimamo wa kijisimamia mwenyewe hivyo unakuwa umejipotezea nafasi kwake na anakuwa hakupi uzito wowote ule ndani ya moyo wake.
Wanaume wengi huwa na hofu na kushindwa kutambua ni muda gani hasa ndo unaopaswa kuwa mwafaka kutuma ujumbe mfupi wa maneno kwa msichana waliovutika naye, maana huona iwapo wakiwahi kuutuma wataonekana kama malimbukeni na iwapo wakichelewa kuutuma itaonyesha kama hawakuvutiwa na huyo msichana hapo mwanzo na hivyo kumfanya msichana apate uwamuzi mbadala wa kuwatoa kichwani maana kwa muda waliochelewa kunaufanya mvuto wa msichana kupungua.
Ni vizuri zaidi na inaongeza mguso na mvuto wa msichana iwapo ukimtumia meseji mda kidogo mara baada ya kuonana kwenu, kupitisha muda kidogo kutasaidia kumpa nafasi ya kukuwaza na kumpa matamanio ya kujiuliza ni saa ngapi utapiga simu, kitendo hichi kitamfanya hausishe hisia zake na kumfanya aongeze mguso zaidi wa kihisia juu yako, hakikisha muda unaompa akufikilie usiwe mrefu sana na usizidi zaidi ya siku moja na nusu au atapata hisia mbaya na kuhisi labda hukuvutika na yeye kipindi mlipokua mnaongea pamoja na utamfanya apoteze ule mguso mliokua nao kwenye maongezi hapo kabla.
Wakati unamtumia ujumbe mfupi wa maneno, mkumbushe vitu vilivyokua vinamfurahisha wakati mlipokua mnazungumza kwa mara ya kwanza, hii itamkumbusha furaha aliyokua nayo pindi mlipokuwa pamoja, hakuna njia nzuri ya kumfanya akujibu meseji zako kama sio kumkumbusha nyie wawili mkikaa pamoja huwa kuna kitu kizuri kinaendelea baina yenu.
Kiumeni.com imekuandalia nini cha kuandika na mambo ya kuzingatia wakati wa kuiandika meseji yako ya kwanza.
- #1, Anza kwa kujitambulisha kwanza.
>> Mambo mtoto mdogo, bado unaendelea na soda zako mpaka jioni hii, siku yako inaendaje?, Hamis.
Hapa neno mtoto mdogo linakuwa kama jina lake la utani na kumfanya akukumbuke kwa urahisi zaidi, kuongeza jina la utani linakuwa linaleta hali flani ya ucheshi kwenye sentensi na kumfanya atabasamu wakati anaisoma hio meseji.
Hata ukitumia jina lake, tafuta namna utakavyoliita wewe ambavyo watu wengine hawamuiti hivyo,
Kama anaitwa Christine - Muite Tina
Francisca - Sisca,
Upendo - Love,
Angel - Malaika.
- #2, Usitume meseji ya kumkweza, jaribu kuwa tofauti na wanaume wengine.
- #3, Msifie.
- #4, Usitume meseji ndefu za kuchosha na kukatisha tamaa kusoma.
- #5, Kuwa mbunifu na usitabilike.
Jibu >> "Siku yangu ilikua tata, watu huwa hawaishi kunishangaza".
Hii itampa hamu zaidi ya kutaka kujua na kufanya maongezi yazidi kupendeza zaidi.
- #6, Usitume meseji nyingi kwa mkupuo.
- #7, Tumia alama za maneno.
- #8, Fanya utani.
- #9, Mkaribishe mahali ulipo ila usimwalike.
>> Nipo ziwani naangalia jua linavyozama, hali ya hewa imependeza kweli na anga limekua la manjano, natamani ungekuwepo!, baadae nitakutumia ujumbe nikifika nyumbani.
Mtamanishe mazingira uliyopo ila usimwambie njoo na kuonyesha hitaji la wewe kumtaka awepo mahali hapo, hii inamuongezea husuda ya kutaka kuwa sehemu ya maisha yako.
- #10, Wahi kuaga.
Post a Comment