NAOMBA ULITAMBUE HILI. - EDUSPORTSTZ

Latest

NAOMBA ULITAMBUE HILI.

Ziko nyakati watu huzipitia bila kujua maudhui ya mapito hayo... Kuna wakati Mtu hupitia Magumu hata akajikuta anakata tamaa ya kuishi, Akijitazama anadhani hawezi tena kuipata FURAHA maishani mwake😭
Kuna wakati Mtu anapitia FURAHA kiasi anakosa muda wa kutafakari juu ya ugumu wa maisha wanao pitia bin adam wengine.... MAISHA yanayolenga mahitaji ni sehemu ya mapokeo ya aina mbili;
KUPATA
KUKOSA
Na yote hayo yanayo matumaini kupitia MAANDIKO MATAKATIFU!
MAISHA yanayogusa Mahusiano ama ndoa yanakuwa na maana moja tu UPENDO WA DHATI... Kuendelea kuutaabisha moyo kwa mambo yanayoweza kusemekana kwamba KILA JAMBO NA WAKATI WAKE ni kosa, Kwanza naomba utambuwe jambo moja "FURAHA YA MUDA MCHACHE ISIKUFANYE UKASAHAU KILIO UMELIA KWA MUDA MREFU, MAMBO HUBADILIKA KAMA HUKUSIMAMIA MAAMUZI YAKO" Kuna wakati watu wanajikuta wameshikwa na shauku ya kuwa na mahusiano ama ndoa kukwepa aibu ama kwa sababu rafiki yake aliishakuwa na Mtu ama ndoa🙆🏿‍♂ Basi nae anajikuta anamshawishi mwenza wake WAOANE! Swala sio NDOA ila Swala ni JE UNAJUWA USIKU MMOJA TU BAADA YA NDOA NA MTU AMBAYE HAKUKUPENDA NI SAWA NA GHARIKA YA NUHU🚢?
Chukuwa tahadhali kabla ya kuzama penzini, Jaribu kuifikiria safari ya NDOA ina kiapo cha MPAKA kifo kiwatenganishe, Je utakapokuwa ushazama kwenye NDOA na mtu asiye sahihi utajinasuaje? Usiwe mwepesi kuitaka NDOA kabla ya kujua MWENZA WAKO ATASIMAMIAJE MISINGI YA NDOA TAJWA🙋🏻‍♂
JIAHIDI MWENYEWE:
Usiishi maisha ya kila mmoja umwambie vile unaumia juu ya Mapenzi, kwamba kuwa imara kiasi kwamba hakuna kitakachosumbua amani yako ya kwamba ULIISHAUMIZWA NA UNAHITAJIKA KUYAONDOKA MAISHA HAYO YA MATESO... Kuongea kwa AFYA kunatokana na jinsi ambavyo umeweza kumuondoka anayekutesa, Furaha iliyo kimaendeleo kwa kila mtu unaekutana nae inatokana na ukakamavu wako na JINSI ambavyo unaweza kukubari kwamba ULIYOPITIA YAMEKUJENGA! Kuwafanya marafiki zako wote kuhisi kuna kitu ndani yako ni kosa sana maana bin adam wanatabia ya kufurahia magumu ya wenzao, Kuangalia upande ng'aavu wa kila kitu na kuyafanya mashaka yako kuwa kweli kunakupa njia ya kuchagua kwa usahihi huko uendako, Kufikiria yaliyo bora tu yatakunyima kupata UTAMBUZI wa nyakati utakazokuwa unadanganya, kufanyia kazi yaliyo bora utajikuta unashindwa kujifunza kwa ULIYOPITIA! na kutegemea yaliyo bora tu utajitenga na kujifunza kwa mabaya ambayo ulisababisha mwenyewe, Kufurahia kuhusu mafanikio ya wenzako kama yako ni kujisahaulisha ya Kusahau makosa ya nyuma na kuweka mafanikio makubwa zaidi ya mbeleni. Kuvaa uchangamfu mda wote na kukipa kila kiumbe kinachoishi tabasamu kila unapokutana nacho ni busara maana unajitenga na msongo wa MAWAZO yasokupa taswira ya kuendelea, Kutoa mda mwingi kwa maendeleo yako binafsi na kwamba hauna mda wa kuwapinga wengine ni kuiruhusu akili yako iweze kupambania mateso yako, Kuwa mkubwa zaidi ya mashaka, mpole zaidi ya hasira, kuwa imara zaidi ya uoga, kuwa na furaha ili kuruhusu uwepo wa matatizo. Kujifikiria vizuri binafsi na kudhihirishia uhalisia huu kwa dunia, sio kwa maneno ya sauti ila kwa matendo makubwa. Kuishi kwa imani mpaka kwamba dunia yote iko upande wako ilihali kwamba wewe ni mkweli kwenye ubora uliopo ndani yako hivyo USIKUBARI KURUDISHWA NYUMA kwani kuja kuanza ni GHARAMA KUBWA.




Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz