Najua si kila mwanaume ambaye anajua namna ya kuongea au vitu vya kumfanyia mwanamke mpaka kumfanya kuwa na furaha, kumfanya kuchanganyikiwa juu yako. Wanaume wengi wanaamini katika kutoa pesa, kweli wanawake wanapenda pesa, lakini kama unataka mwanamke wako, kukuona mtamu, kuchanganyikiwa juu yako na kila wakati kutaka kuwa karibu na wewe basi mbinu hizi zitaweza kukusaidia sana.
(1) Msifie kitu cha tofauti kabisa na mazoea; Amezoea kuambiwa kuwa amependea, ni mzuri, anajua kufanya kitu flani, hivyo ni vitu ambavyo hata Mama yake, marafiki zake na ndugu zake humuambia, wewe kuwa tofauti, msifie kitu ambcho kinamfanya ajue kuwa unamjua zaidi, kitu ambacho kinamfanya ajione wa maana zaidi.
Mfano msifie namna ambavyo unapenda ufanyaji wake wa kazi, jinsi alivyo na mzuka wa mapendeleo au naman anavyokupa changamoto ya kufanikiwa zaidi. unaweza sema, “Napenda jinsi unavyojituma… unajau nikiwa na wewe akili yangu inachangamka sana… utafika mbali Baby unajituma sana…” angalie uwezo wake na msifie, mfanya ajihisi bora na sifia kitofauti kabisa.
(2) Ulizia kuhusu Familia yake na maisha yake; Wakatio mwingine wanaume tunakua wabianafsi sana, kutaka kuzungumziwa kuhusu sisi tu, unataka kuzungumzia kuhusu Mama yako anasema nini, Mama yako anataka nini na vitu kama hivyo. Humuulizii kuhusu Mama yake, kwao vipi alikuambia kuwa Mama yake anaumwa huulizii. Akija kwako unajalia kufanyie yale unayotaka wewe, huulizii yeye anataka nini?
Kila wakati unazungumzia familia yako na ndoto zako tu. Ni kama yeye hana maisha unataka aishi maisha yako tu, hiyo si sawa, ukitaka kumchanganya mwanamke, ulizia kuhusu familia yake, wanaendeleaje, wakoje, hata kama husiadii, msikilize kuhusu maisha yake, muonyeshe kuwa, kile anachokiwaza kina maana na yeye ana maana kwako.
(3) Msikilize na onyesha kuwa unasikiliza; Ndiyo wanawake wanapenda kusikilizwa hata kwenye vitu ambavyo sisi wanaume tunaona kama ni vya kiuuzi. Kama mwanaume wake ni lazima wewe ndiyo uwe msikilizaji wake wakwanza, uwe kam shoga yake, kwamba akiwa na kitu, kakwazwa, kakwama au hata ana kaumbea kapya huko basi awaze kukuambia wewe kwanza kuliko mtu mwingine.
Msikilize zaidi anapokua na shida, mawazo, hata kama humsaidii lakini ile kuonyesha kujali, ukamuacha akatoa dukuduku lake inampa ahueni na inaongeza mapenzi sana. Sikiliza kakuambia nini, shauri, na baadaye ulizia kafikia wapi, tafuta namna ya kumsaidia, usimkatishe katishe, onyesha kujali na si kupuuzia kila anapoongea, hata kama ni ujinga, acha kukosoa kwa dharau mrekebishe kwa upendo. “Baby mbona ni hivi na vile… Baby hapo naona kama umekosea, ilikua hivi na vile….”
(4) Muambie na muonyeshe hisia zako; Wanaume mara nyingi si watu wa kuongea kuhusu hisia zetu, tunaona kama ni udhaifu, unakuta mwanaume anampenda mwanamke, kachanganyikiwa kabisa juu yake lakini ni ngumu kumuambia kuwa nakupenda, nimeumia, nimekereka au nafurahia nikiwa na wewe. Tunapenda kimya kimya na wakati mwingine unakuta mtu anampenda mwanamke lakini hamuambii.
Kuna wanawake wengi wanchepuka, wanachana na na watu wao kwakua tu wanaamini hawapendwi kumbe wanapendwa ila hawajaambiwa. Mwanaume, muambie mwanamke wako unavyohisi, muambie unavyompendda, unavyomfurahia, akikufanyia kitu kizuri shukuru na onyesha hisia zako, kwamba kama unampenda mfanyie vitu vya upendo, mtoe out, mpe zawada, mfanye ajisikie anapendwa ili asiutafute upendo huko nnje.
(5) Fanya kile anachotaka kukifanya; Kimakuzi wanawake wamelelewa kumridhisha mwanaume, kwamba kufanya kila kitu ambacho wanaamini wanaume wao wanataka kufanya. Kwa mfano mdogo, hata kwenye chakula, unakuta mwanamke anapika chakula kile ambacho mume wake anapenda hata kama yeye hakipendi au hakifurahii. Anaweza kucheka kumbe amecheka ili ufurahi, kama mwanaume unatakiwa kumjua mwenza wako na mara moja moja kufanya kile kitu anchotaka yeye hata kama wewe hukitaki bila kulalamika.
Unajua anapenda kuangalia Tamthilia, wewe inakuboa, basi angalia na acha kuangalia mpira siku hiyo afurahi. Anapenda kufuarilia kitu flani, kifuatilie ili muwe na stori za kuongea, unajua anapenda chakula flani, basi muambie apike na kula ili nayyee afuirahi. Wanawake wanajitoa sana mpaka wanajisahau, kwa maana hiyo kama usipokua makini anaweza asiwe na furaha kwa kukufurahisha wewe kila siku.
(6) Kua makini na vitu vidogo vidogo na saidia kazi za nyumbani bila kuambiwa; Wanawake wanafurahia zaidi kufanyiwa vitu vidogo vidogo kuliko vikubwa, vizawadi, mnunulie vizawadi, karanga, pipi, chocolate na vitu vingine vingine, kumbuka siku yake ya kuzaliwa, siku ambayo mlikutana, mpe zawadi, sifia kucha zake, sifia nywele zake na vitu vingine ambaviyo kikawaida havionekani onekani.
Msaidie vikazi vizofo bila kuambiwa, amemaliza kupika osha vyomvbo, toa nguo zake siku moja kafue, siku moja amka na safisha nyumba, hata kama hutafanya vizuri kama yeye, hata kama atalalamika kuwa hukufanya vizuri ila jua kafurahia, anafurajia kuwa na mtu ambaye anamfanyia hivyo.
(7) Muonyeshe mahaba Mbele za watu bila kulazimishiwa; Mnatembea mbele za watu mshike mkono, tafuta sababu za kumgusa mwili wake mbele za watu, mshuke kiono, unaweza kumtania hata kwa kumtekenyetyekenya na mazingira yakiruhusu mbusu mbele za watu. Kwa kifupi onyesha mbele za watu kuwa unampenda, yaani humuonei aibu, unamfurahia na hujali kama watu wanawaona au la, wanawake hawependi kupendwa tu bali wanapenda kuonyeshwa kuwa wanapendwa na watu wajue kuwa wanapendwa.
(8) Mnong’oneze mambo ya kimahaba; Mko mbele za wtau, mmekaa, mlikua mnafanya kitu cha maana au mnasikiliza kitu cha maana, akiwa hana hili wala lile, mvute, inama sikioni kisha mnong’oneze kitu cha kipuuzi. “Baby unajua nasikiliza hapa lakini najaribu kukumbuka hivi asubuhi ulivaa chupi ya rangi gani… HIvi unajua hapa wakizima taa tunaweza tukamza… kwanini tusiingie kwenye gari tukapiga hata kimoja tu hivi, nina hamu na wewe….” Muangalie usoni kisha mcheke kwa pamoja.
(9) Msaidie kukua, mshirikishe katika mambo yako; Acha kjuwa mtu wa kumkosoa, kila akikosea kidogo unamdhihaki na kumfanya kuonekana kuwa hana akili. Mara nyingi wanaume tunajiona tuna akili sana kuliko wanawake, hatuheshimu mawazo yao, hatutaki kuwasikiliza na kila kitu tunachoongea sisi ndiyo tunataka kiwe. Kuna wakati kweli tunakua sawa lakini si kila wakati. Kama unataka mwanamke wako kuwa na furaha basi hakikisha kuwa unamsikiliza, msaidie kukua na mshirikishe katika mambo yako.
Mwanamke si adui na mwanamke wako si mshindani wako, mnajenga nyumba moija, hakuan haja ya kushindana na kama unataka kuonekana kuwa wewe ndiyo mwenye akili zaidi basi ni ngumu kufanikiwa. Kuwa na furaha hakikisha mwanamke wako ana furaha, msiadie kukua, kibiashara au kiajiri kama umemzidi, msikilize na shirikiana naye, ni rahisi kufanikiwa mkifanya pamoja kuliko ukifanya peke yako.
Post a Comment