Ndoa ni ya watu wawili, narudia ndoa ni ya watu wawili, lakini kuna familia nyingine mwanamke ukiolewa basi kila mtu anadhani kuwa yeye ndiyo mume wako ana haki ya kukupangia kila kitu. Ni nadara sana kukuta masehemeji wana midomo, lakini ni jambo la kawaida kukuta mawifi wana midomo mpaka unahisi kama mnashea mume. Wanakua na visirani, wanajifanya kujua kila kitu, wanaongea na kama Kaka yao naye ni wale wanaume wakimya ambao hawajui kuongea au anawasilikiza sana ndugu zake basi utachanganyikiwa katika hiyo ndoa, sasa ngoja nikudokeze kidogo namna ya kuishi na hawa watu.
(1) Wengi wamedoda wana matatizo yao; Mwanamke mwenye furaha katika mahusiano yake, ambaye ana mwanaume wake anampa raha kwanza hatakua na muda wa kufuatilia matatizo ya Kaka yake. Ukiona wifi yako kila siku kukukosoa, kila siku kukulalamikia, anajifanya anampenda Kaka yake utadhani ndiyo alimtoa bikra basi jua kuwa hana furaha. Anaweza kuwa anapigwa kila siku na bwana wake, au hata bwana mwenyewe hana anadanga tu, wengi unekuta kashazalishwa hapo nyumbani na hana harufu ya ndoa.
(2) Hajawahi kuhongwa hata pesa ya Pedi hivyo akiona Kaka yake anavyokuhudumia basi anachanganyikiwa na kuona wivu. Kwa maana hiyo mtu wa namna hiyo mjue tu kuwa ana matatizo, badala ya kumuangalia kwa hasira, badala ya kumuonea wivu au kudhani yeye ana nafuu muangalie kama mgonjwa, muonee huruma kuwa anatamani vitu unavyopata lakini ndiyo hivyo ataishia tu kuangalia. Usione anacheka kila siku, nikuambie mtu mwenye furaha hawezi kuingilia ndoa ya Kaka yake, sanasana ukilalamika wewe kuwa Kaka yeka anakunyanyasa ndiyo ataingilia.
(3) Huyo ni shangazi tu wala asikutishie; Wadada wengi wanajiona kama wamiliki wa mali za Kaka yao, wanajiona kuwa Kaka yao ni Keki sana na waop ndiyo wapishi wa hiyo Keki. Wanadhani kuwa mwanamke aliyeolewa kwao hana haki yoyote na kuona kuwa wao wana haki nyingi kwa Kaka yao kuliko wewe. Nikuambie tu kwamba, kama una shangazi kamuangalie leo, lakini kama huna basi angalia wa jirani yako, yuko wapi? Jiulize hivi wewe unampenda na upo karibu na nani, Mama yako au shangazi yako? Kama upo karibu na Mama yako basi jua kuwa wewe ndiyo utakua Mama wa watoto wako.
(4) Kwa maana kuwa, mwisho wa siku, wanao na mumeo watakuheshimu na mtakua familia moja. Lakini dada wa mume wako, atakua shangazi, wanao hata hawatamjali na baada ya muda utaona kuwa hata mume wako atampuuza hasa majukumu yakizidi. Najua kuna wanaume ambao bado wanajali dada zao hata uzeeni kuliko wake zao ila ni wachache. Lakini cha muhimu kumbuka, wanao watakupenda wewe na huyo wifi atabaki kuwa shangazi apende asipendi. Kwa maana hiyo muangalie tu kwa dharau na muambie shangazi utaniambia nini?
(5) Wapuuze na acha kulalamika kwa mume wako; Watu hawa wanakua hawana maisha, kwakua wao hawana furaha basi hujipa kazi ya kuiba furaha za wengine, anachotaka akigombana na wewe ni wewe kwenda kulalamika kwa mume wako ili usiwe na amani na mume wako. Sasa kama wifi hakupigi, ni maneno tu anaongea mbele yako au kwa watu wengine jifunze kanuni hii. “Tutamalizana wenyewe!” Kamwe! Narudia kamwe! Sijui kama unenielewa Kamwe usilalamikie mambo ya kijinga kwa mume wako, umemsikia anakusangenye! Umemsikia anakutukana huko, mmegombana na kutukanana huko!
(6) Wakati mwingine hata kama mmepigana kabisa, usiende kulalamika kwa mume wako, kwanza mara nyingi haitasiadia, mumeo anawajua dada zake, lakini pili ndiyo kitu wanachotaka kuwa na wewe usiwe na amani. Acha kuwa mtu wa kulialia, watui hawa wanapenda kuonea wale wanawake wanyonge, kama huamini hembu chunguza, yule mke mwenza wa shemeji yako, yule bandidu, mbona hawamsumbui? Nikwakua halalamiki lalamiki na haonekani mnyonge.
Wakikutukana nyamaza, mume akija jifanye mko sawa, hata kama mmetukanana akija usiseme kama wakisema wao mume akikuuliza wewe muambie “Mbona vilikua vitu vidogo vya kike nishamalizana nao, mimi sina shida na mawifi zangu!” jifanye hayo mambo kama hayakuumizi! Yaani hapo watavimba, usionyeshe kama maneno yao yanakuumiza, hapana, onyesha kama uko sawa na hakuna kitu wanachofanya ambacho kinakukera. Ukiwa mtu wa kilalamika lalamika, iwe ni kweli au uongo hata mume wako atakuchoka!
(7) Tafuta kazi; Kama mume wako anaruhusu dada zake kukupanda kichwani basi jua na mume wako ana matatizo. Mwanaume kamili anayejielewa anadili na mke wake na hata kama mke wake ana matatizo haruhusu ndugu zake kumpanda kichwani, anachofanya ni kukomaa na mke wake tu kama ni kmshikisha adabu amshikishe yeye. Sasa unachotakiwa kufanya hapa ni nini, kama unaona mumeo anaacha ndugu zake wanakukalia kichwani basi jua kuwa ipo siku anaweza hata kukuacha kwakua ndugu zake wametaka.
(8) Hakikisha unakua huru kikipato, hakikisha kuwa unakua na kazi na unaweza kujitegemea. Narudia kwako kufanya kazi ni lazima, lakini si kufanya kazi tu hakikisha kuwa unawekeza na wewe unakua na kitu chako. Kama una kazi na mnachuma vitu na mume wako basi andika majina yenu wawili, mume wako asije kukuambia kuwa tunanunua mimi ndiyo mwanaume anandika jina langu, hapana usikubali. Wanaume wa namna hii unaweza kujikuta siku umechukua mkopo mmejenga kabadilika kaandika jina la dada yake.
(9) Kama huna kazi mwanaume wa namna hii kumuambia mali muandike majina yenu wawili atakataa, hivyo kama mna watoto komaa mali zie na majina ya watoto. Hili ni muhimu sio kwakua unamuwazia mume wako kifo, hapana nikwakua anaweza siku akabadilika na kumuandika mali dada yake. Lakini cha muhimu kwa mwanaume kama huyo hakikisha una kazi, kwanza itakusaidia kujitegemea kikipato mwenyewe, kuwa huru na maisha yako, lakini pili itakupunguzia mawazo.
(10) Unapokua na kazi kwanza hao ndugu watakuheshimu hata kama si mbele yako lakini kimya kimya kwenye mioyo yao. Lakini pia muda wa kuwaza maatizo yao utakua mchache, kutwa uko kazini, kwenye biashara au kazini, kuoanana nao hata kama wanaishi kwako ni usiku sasa mtagombana saa ngapi, labda kwenye simu ambayo mara nyingi unawakatia. Hapa ndiyo namalizia kwa kusema, acha kuishi nao, kama unaishi nao labda nyumba ya familia pambana mhamie kwenu hata kwa kupanga itapunguza sana kugombana kusiko na maana.
Post a Comment