Tuliandikiana barua za mapenzi na mwenye muandiko mzuri alikua anaonekana atakuwa na sura nzuri.
Walioenda shamba wakati baba analeta ndizi mama alikua ameenda kuchota maji.
Walioenda shamba wakati baba analeta ndizi mama alikua ameenda kuchota maji.
Simu zenye pattern na password hazikuwepo kwani hata wenye simu hawakuwepo na hata walioanzakuzitumia zilikua za mkonge za TTCL
Hata zilipoanza za mkononi zilikua mshindi, dole gumba na hazikuwa na password.
Tulifurahia kuwa pamoja bila kujua kwenye insta kuna nini jipya. Tulikusanyika tukila wali na maharage yenye mchuzi mwingi kwenye sinia na sahani moja kubwaa.
Tulienda wote kanisani. Tuliiheshimu jumapili na siku za ibada kwa wanaoenda madrasa.
Hatukukua na migogoro ya mtoto huyu baba yake nani kwani mke alikua na mwanaume mmoja tu aliyemheshimu sana. Najua utandawazi unavuruga amani kwa njia nyingi. Haki sawa ikichukuliwa na mashoga wakishauri mumeo akitoka nawe toka, mwaga mboga nimwage ugali, huku tukisahau ndoa huvunjwa na mwenye ndoa (mwanamke).
Ushasikia mke mpumbavu huivunja nyumba yake kwa mikono yake mwenyewe. Na mwenye nyumba (mkuu wa shughuli za nyumbani ni mama). Sababu tumesahau asili yetu basi hata wanaume wameona ni sawa wanawake wakahangaike kutafuta pesa ya kulisha familia huku wao wakilala ndani. Bila kuelewa watoto wanajifunza nini kwenye hili.
.Uko wapi furaha ya baba kurudi na mkungu wa ndizi nyumbani??? Hata hivyo wamama hawataki chakula tena wanataka simu kali na wigi kali tu. Si tunajenga nyumba ya mawigi kwenye familia.Hata zamani basi ilikua si rahisi kuona mashoga barabarani japo walikuwepo sasa mashoga wanadai haki zao.Dah, Sijui FUTURE bali naogopa nikijua tunazidi kukosa upendo na umoja.Na ndoa hazidumu tena.zamani mtoto alimuheshimu mkubwa wala hakumgusa hata upinde wa kanga yake..
siku hizi mambo yameharibika kuna vibenteni wala haviona haya kupalamia milima iliyowazidi umri!!!heshima hakuna!!....eti wanasema mapenz hayana umri!!!daah na miss sana enzi za zamani ukimpenda nwanamke munaishia kucheza mdako na komborela hatukuzijua guest..lakini leo kitoto cha form one kinajua bei za guest zote za mtaa!!daaah!!!!....!
nachoka Jamani mimi!!!..zamani hakukuwa na simu lakini wazee wetu hawakuwa na hofu ya kujua mke yuko wapi maana hakukuwa na maslya queen wa kuiba waume za watu !!siku hizi daah!!...zamani tulitumia simu ya baba kucheza game wala hatukuona text ya mchepuko wala ikiita hovyo..siku hiz daah simu inaingia mpka bafuni!!!mke hajui password ya mume na mume hajui Pasword ya mke !!mwendo wa kuviziana tu!!!dah sijui huko nje wanatafuta nini!daah...acha niishie hapa !!nshachoka mimi
Post a Comment