*➖Mzazi siku zote hufurahia mafanikio ya mwanae kuliko mtu yeyote yule*
*➖Mzazi ni ngumu sana kumlilia shida mwanae kwa sababu anahisi kuwa anaweza kumsumbua au kumuharibia mipango yake.*
*➖Mzazi ni mtu pekee anayeweza kufurahi kulala njaa ili hali mwanaye ameshiba*
*➖Ukiona mzazi anataka msaada toka kwa mwanae ujue anayo shida haswa na siku zote hujitahidi kupunguza ukubwa wa shida yake kwa mwanae ili asimpe usumbufu*
*➖Mzazi akikwambia ànashida ya elfu 5000 jua shida halisi ni 20000 au zaidi ila atafurahi kwa kuipata hiyo elfu tano*
*➖Mzazi akikwambia anaumwa kidogo, jua kuwa kweli anaumwa, huwa hawahitaji kabisa kuona mwanae akisumbuka kwaajiri yake.*
*➖Mzazi akikwambia mkono unauma, inaweza kuwa amevunjika kabisa ndio maana kakwambia, akisema amevunjika jua hali ni mbaya sana*
*➖Mzazi amebeba baraka za moja kwa moja kutoka kwa Mungu*
*➖Mzazi akifurahi moyoni mwake kwa mtoto wake, jua mtoto huyo lazima abarikiwe, na akihuzunishwa inakuwa kinyume chake yaani zinatoka laana*
*➖Katika amri kumi za Mungu, ni amri ya kumhusu mzazi pekee iliyowekewa ahadi kuwa mtoto atakayemheshimu mzazi atapewa umri mrefu zaidi wa kuishi*
*➖Siku zote mzazi ni ngumu sana tena sana kutoa laana kwa mtoto, lakini hii haimaanishi kuwa laana hazitoki , laana na baraka hutokana na mapokeo ya ndani ya mioyo ya wazazi juu ya kile anachotendewa na mtoto wake*
*➖Epuka kumfanya mzazi ahuzunike moyoni mwake, siku zote mtafutie jambo la kumpendeza, na uzuri ni kuwa huwa hawahitaji vitu vikubwa toka kwa watoto wao.*
*➖Mzazi anaupendo wa ajabu sana usio bagua, ata muwe watoto 20, na mmoja akawa msaada mkubwa sana kwake, kamwe hawezi kumbagua au kumdharau yeyote kati yao, tena unaweza kushangaa akampenda yule ambaye hawezi kumsaidia chochote, lakini maana yake kubwa ni kuwa anaupendo sawa kwa kila mmoja na anataka wote mfanikiwe na kubarikiwe sababu wote ni uzao wa tumbo lake*
*➖Mtoto mwenye busara huchota baraka kwa mzazi wake angali yupo hai, hizo baraka ni za pekee na haziwezi kupatikana kwa mtu YEYOTE*
*➖wengi wamehisi kurogwa na kuhangaika huku na kule kutafuta mafanikio huku wameiacha funguo ya maisha yao ambayo ni mzazi*
*Ubarikiwe*
*Nikutakie siku njema mpendwaa🙏🏽🙏🏽🙏🏽
Post a Comment