MWANAUME USIMWACHIE MKEO HELA CHUMBANI MWACHIE MBELE YA WATOTO NA UMWAMBIE NA MATUMIZI YAKE, NA WATOTO WASIKIE USIJE KUISHI MAISHA YA UPWEKE UZEENI


MWANAUME Unamwachia mkeo hela ya chakula chumbani, Mke anatoka na kapu anaenda kununua chakula, anapika, anawaambia watoto, njooni Wanangu
mle nimewapikia chakula kitamu, watoto wakishakula wanasema Asante Mama.
MWANAUME Unamwachia mkeo hela ya nguo za sikukuu chumbani, kesho yake mkeo anatoka kwenda kununua nguo, akirudi anawaambia wanangu nimewanunulia nguo za sikukuu njooni mjipimie, watoto wakishajipima, anawaambia wanangu mmependeza eeee, simnaona ninavyowapenda watoto wanafurahi na kusema asante mama.
MWANAUME Kila aina ya pesa ya matumizi unamwachia mkeo hela chumbani.
MWANAUME Ukifika muda wa kutoa ada unamkabidhi mkeo hela chumbani, kesho yake mkeo anawaambia watoto kuwa anaenda kuwalipia ada ya shule, akirudi anawaambia ananhu nimeshawalipia Ada, na gari za shule zitakuwa zinawapitia, nataka msome wanangu ili baadae mje mnitunze, watoto wanasema Asante Mama.
KIBAYA ZAIDI
Ukifika muda wa kutoa adhabu, mkeo yeye hatoi adhabu, anawaambia watoto, ngoja baba yenu arudi, na wewe ukirudi unaelezwa na mkeo matatizo ya wanao, unachukua bakora unawaadhibu watoto, bila kujua kuwa unazidi kujenga uhusiano M'BAYA na wanao.
Ukifika uzeeni, watoto wako hawana KUMBUKUMBU yoyote ya mema uliowafanyia na kama bado utakuwa hai watazidi kukuchoma zaidi na kale ka msemo kao ka *NANI KAMA MAMA*
WANAUME TUWE MAKINI SANA.
Share
Like Page


0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post