MWANAUME FAHAMU CHOZI LA MWANAMKE JUU YA ARDHI NI LAANA:

CHOZI LA MWANAMKE MGUMBA: IPO SULUHU YA... - Personal Care Forever ...
Nikweli unaweza ukawa unamfanyia mwanamke wako mambo mengi ya maumivu na ya kumtoa machozi, lakin kwasababu ana moyo wa uvumilivu akawa anavumilia tuu. Huenda ukaona ni jimbo rahisi sana mkeo kulia ila ujiulize hivi nilimueka ndani kwaajjli ya kumtesa.
👉Moyo wa mwanamke ni moyo ulioumbiwa uvumilivu, atavumilia mateso yote unayompa, vipigo vyote masimango atavumilia atalia lakin chozi lake juu ya ardhi ndio jibu la maisha yake, Mwanaume unaona ni sahihi tu kumpiga mkeo bila hatia lakin ni laana iliyo na msamaha wa gharama.
👉Mkeo unamfanya kama mtoto mdogo, mtu unalala nae kitanda kimoja lakin unampiga kama unavyowapiga wanao, mama alie na watoto walie ndio fahari yako, kumdhalilisha mzazi mwenzio kwa watoto na majirani unaona sifa kweli, hasira zako binafsi unaamua kuzimaliza juu ya mkeo.
👉Mtu mzima analia kama mtoto anatoa machozi yasiyo na hatia lakin wew unaona ni sawa sawa, lakin laiti ungalijua hilo chozi lake ni laana kweny maisha yako, moyo wa mwanamke unaposononeka huwezi kuendelea mbele kamwe.
👉Unapouchubua moyo wa mzazi mwenzio, ukaona ni sifa au unamkomoa kumbuka wew huwez kupiga hatua kabisa, mwanamke anapodondosha chozi lake juu ya ardhi kwasababu yako huwa anakufungia baraka zote huwez kufanikiwa kabisa.
👉Ebu litafakari hili mwanaume kwann unafikia hatua ya kumdharau mwanamke wako, unamshughulikia kama mwanao, unapata faida gani kuona mwenzio anakosa raha kwaajili yako, moyo wake umejaa huzuni na hofu saa zote anaishi maisha ya woga.
👉Mpende mkeo, mheshimu, mtamini, mjali huyo ni ubavu wako ebu ona ukimuumiza ni ww umeumia, suala la kupigana kama watoto wadogo acha. Kama mmekosana kaeni chini msuluhishe sio kuaibishana.
SHARE SOMO HILI, USIPUUZE SHARE


0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post