MWANAMKE ACHA KUTAFUTA MUME ATAKAYEKUWA SAWA NA UTAKAVYO WEWE. KWANI WA VIWANGO VYAKO HATAZALIWA📌

Kama una mwanamke wako, ni mke wako, mpenzi au mchumba wako na ...
Nini Maana ya andiko lisemalo;
• HAKUNA MWANA WA ADAM ALIYE MKAMILIFU?
Hauwezi kumpata Mwanaume unayemtaka wewe, Hata shetani alikuwa MALAIKA WA MUNGU tena mwimba kwaya lakini kwa udhaifu wake akaasi ije iwe Mwanaume wa dunia hii?
Mwanamke wakati ukisubiri aje MUME MTAKATIFU Yule aliyeandikwa kwa ajili yako atakuwa amevunjika MOYO na kuendelea kutafuta Mwanamke mwingine, Kisa hukuona kama anavyo vigezo kama unavyovitaka ndo maana mnajikuta mnaolewa na wanaume wanaojifanya kutimiza vigezo vyenu baadaye mnajutia kwa sababu hawakuwa HALISI💯
Upendo unaweza kumgeuza mtu mbaya akawa mtu mwema, Tatizo ni wewe Mwanamke kujaribisha jaribisha MAHUSIANO ili uone atakayekidhi VIGEZO vyako😂
Vigezo anatimiza MUONGO peke yake ila Mkweli utaweza kumsahihisha kwa madhaifu yake na mwisho kabisa ATAKUWA KAMA ULIVYO-WIWA na hapo nafsi yako itatulia.
Kumpata Mtu unayemtaka mwenyewe ni NDOTO ngw'ana wane ikiwa mtoto wako wa kuzaa anakuja kukubadilikia vipi mtoto wa Mwanamke mwenzio?
Ifike mahala Mwanamke usiwazie FURAHA NA AMANI peke yake bali kumbuka hakuna mkamilifu na hapo MUNGU atamtengeneza ulomchagua bila kuzingatia vigezo na utakuwa na FURAHA PAMOJA NA AMANI YA KUDUMU kwani Makosa ndo HUMFANYA MTU KUWA MZURI kuliko kama akija kwa uzuri na kumbe MBAYA utajutia rafiki yangu😭😭😭
Kwa taarifa yako WANAWAKE wanaofurahia MAHUSIANO na NDOA zao mara nyingi ni wale wanaojua kwamba HAKUNA BIN ADAM MKAMILIFU muda mwingine wewe mwenyewe unaingia makosa bila kujua, Maana WANAWAKE mood zenu mnazijua wenyewe JE WEWE UMEKAMILIKA?
Acha UBINAFSI kutaka uwe wewe tu wa kutoumizwa huku nawe ni mdhaifu vile vile😷


0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post