MPE NAFASI MPENZI WAKO KWA WANAUME WANAOKUSUMBUA KINGONO


Kimsingi hili ni tatizo sugu ambalo linaepukika lakini kuna ugumu kidogo katika kuliepuka moja kwa moja. Mitaani tunakoishi wapo wanaume ambao wasione msichana mrembo akipita, lazima wataanza kumsumbua kwa kumuita na wengine kufikia hatua ya kuwashika sehemu zao nyeti bila ridhaa yao.
Mbaya zaidi ni kwamba wanaume hao hufanya hivyo hata kwa wanawake ambao ni wake za watu au wenye wapenzi wao. Tabia hii huwakera sana baadhi ya wanawake hasa wale wanaojiheshimu na kuziheshimu ndoa na uhusiano wao.
Hata hivyo, kuwaepuka wanaume wakati mwingine huwa ngumu kwa kuwa wengi wao hawana akili timamu, muda mwingi wao huwaza kufanya ngono tena na kila mtu watakayemuona bila kufikiria madhara wanayoweza kuyapata baadaye.
Niseme tu kwamba, wanaume wa aina hii wapo wengi tu huko mtaani ila kwa mwanamke anayeiheshimu ndoa yake au uhusiano wake na akaweka nia ya kuwaepuka, inawezekana!
Niseme tu kwamba, wanaume siku hizi wametawaliwa na tamaa zisizokuwa na msingi. Ukitaka wakusumbue watakusumbua kweli na wakati mwingine wanaweza kukushawishi ukamsaliti mpenzio wako.
Kikubwa ni mwanamke kuwa na msimamo. Kutokukubali kugeuzwa kiti cha daladala kwamba kila mtu anaweza kumchezea.
Lakini mbali na hilo, unajiwekea mazingira ya kuwafanya wanaume wakuheshimu na kugwaya hata kukutamkia maneno ya kijinga.
Vaa kiheshima, acha utani wa kijingajinga na wanaume na hakikisha unakuwa na tabia ambazo zitawafanya wanaume wajue kwamba wewe ni mtu mwenye ndoa yako usiyetaka kuutia doa uhusiano wako.
Hata hivyo, huko mtaani unakopita unaweza kukutana na mwanaume anayejua fika wewe ni mtu ulie kwenye uhusiano wako lakini anakusumbua kila siku huku akikushawishi kwa njia mbalimbali.
Huyu hutakiwi kumchekea na kumpuuzia, una kitu cha ziada unachotakiwa kukifanya. Nasema hivyo kwa kuwa kuna wanaume vinga’nganizi. Unampa maneno makali ili akukome lakini bado anaendelea kukusumbua.
Inapofikia hatua hiyo jaribu kumshirikisha mpenzi wako au mumeo.
Hiyo itasaidia sana kwani mumeo anaweza kuchukua hatua zinazostahili dhidi yake na hatimaye kuweza kupunguza kasi ya usumbufu huo. Kamwe usithubutu kukaa kimya.
Mbaya zaidi ni kwamba unaweza kukuta shemeji yako ambaye ni rafiki wa karibu wa mpenzi wako ama mwanaume anayemfahamu vilivyo mumeo akakutongoza. Huyu ni hatari sana na wala usisubiri akutongoze mara mbili. Siku ya kwanza tu atakayokutamkia maneno yake ya kipuuzi, kwanza geuka mbogo, mkaripie kwa ukali kisha mpe taarifa mpenzi wako.
Baada ya hapo, mwanaume huyo hutakiwi kumheshimu, mchukukulie kama mjinga mjinga fulani. Nasema hivyo kwa kuwa mwanaume wa dizaini hiyo akikutokea kisha ukawa unamchekea ipo siku anaweza kukulazimisha kufanya naye mapenzi.
MWANAMKE MCHA MUNGU NI ZAIDI YA MGODI WA MADINI.
Kwa nyakati tulizonazo kila kijana atakwambia cha muhimu kuwa na mwanamke mwenye hofu ya Mungu cha ajabu sasa huyo mtu anayesema hivyo hana hofu ya Mungu na hakumbuki aliingia lini kwenye nyumba ya sala, nikatambua kumbe kumjua Mungu ni zaidi ya Uzuri wa nje unaoweza kuharibika, binti tunza mahusiano yako na Mungu hayo mengine yatakutafuta , nikukumbushe tu madini hufuatwa porini na chini sana kwenye miamba ila kuwa makini na wachimbaji haramu wasio na ujuzi.


0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post