MOJA YA WAKATI MGUMU SANA KWA MWANAUME NI PALE AMBAPO...!

UTAMUZAIDIAPP

Moja ya wakati mgumu sana kwa mwanaume ni pale ambapo huna kazi, huna kipato chochote na huna mchongo kabisa, kila unachojaribu kukifanya kinakwama halafu mke wako anatimiza majukumu yako tena bila manyanyaso, kwa mwanaume kamili ukiachana na wale wakiume lazima utajinyanyasa na kujisikia vibaya.
Kwa mwanaume kamili pia utamshukuru mke wako na pale mambo yako yakitiki basi hutasahau kuwa mke wako alikua na wewe bega kwa bega kipindi ambacho hata ndugu zako hawapokei simu zako, marafiki nao ukiwapigia wanakumbia “nitakucheki baadaye” kisha hawaoatikani tena, utakumbuka thamani ya mwanamke wako na hutaruhusu mtu kuchezea mafanikio yako.
Lakini kwa wale wanaume ambao bado hawajavunja ungo vizuri basi wakipata wanasahau kila kitu, tena kama walisaidiwa hunza kujiona kama wao wana akili sana, huanza matusi, dharau na kuthamini marafiki na ndugu ambao kipindi hicho hata namba yako walikua hawana. Utataka wakusifie na kukuona wamaana wakati katika akili zao wanakuona takataka.
Mwanaume kama una mwanamke kama huyo ambaye alikubeba kipindi ambacho unaweza kaa wiki bila kuingiza hata Buku basi mheshimu sana na mara kwa mara mkumbushe kuwa yeye ni jembe na unajisikia raha kuwa na mwanamke kama yeye. Kwa mwanamke kama ulishapitia hali hii, ukamsaidia mwanaume, ukabeba majukumu mpaka pale ambapo naye alipata na kufanikiwa.
Baada ya maisha kumnyookea akabadilika na kuanza kukunyanyasa basi kuanzia leo sema sinyanyasiki tena, akirudi nyumbani akitukana muangalie, usiseme chochote kumbuka ulipomtoa kisha waza binti wa miaka 12 ambaye bado hajavunja ungo namna ambavyo anaringishia underskirt ‘anasketi’ au shumizi mpya, kisha tabasamu na sema “Ni utoto tu akikua ataacha…”
Anza kujipanga kivyako na weka ahadi kuwa kama niliweza kumtoa huyu asiyenashukurani na mimi naweza kujitoa, anza upya kutafuta, uza chochote hata vitumbua hata kama yeye anaendesha Ranger Rover na akikukataza muambie “Tulia niangalie nikifanikiwa…” acha kulialia na fanikiwa kweli kwani wewe ni jembe na mpini wake hivyo unaweza kulima peke yako!
Kama nimekukwaza basi badilika kwani huna lolote wanaokuona wamaana kwa kumdharau mwanamke aliyekutoa wanajua kuwa huna kitu ulisaidiwa tu wanakuchora tu pole


0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post