Mwaka 2017 nilinunua Kitabu chako, nilishidwa kukisoma kwakua nilikua na mawazo mengi sana, nilimfumania mume wangu na mwanaume mwingine. Kwa maana kuwa mume wangu alikua anafanya mapenzi na Shoga. Nilikua nimechanganyikiwa, kila mtu niliyeongea naye aliniambia vumilia, kama mume wako kakuomba msamaha basi ipo sikua tabadilika mpe nafasi nyingine. Niliumia zaidi kwakua watu wengi walikua wanajua tabia za mume wangu lakini hawakuniambia.
Nilipoongea na wewe uliniambia maneno ambayo yalinichoma lakini yalikua kweli. Uliniambia kubadilika kwa mume wangu ni mpaka amue yeye na mimi kama mke sitaweza kujua kama kabadilika au la? Kama nikiamua kubaki naye nisibaki kwakua nina mawazo kua atabadilika bali nibaki kwakua nataka na pia niwe na malengo yangu. Uliniambia kuwa kwa sasa sina kazi ndiyo maana ndugu zangu hawataki niondoke kwani naenda kuwa mzigo kwao. Nitafute kazi na kama mume akikataa nimuambie bora kuachana kuliko kubaki naye bila kazi kwani ubaya nikuwa nikishamsamehe nakubaki kwakua nishajua hataficha tena.
Kwamba asipobadilika naweza kuchanganyikiwa kwani hata kufanya mapenzi na mimi itakua shida na wakati mwingie hao mashoga wake wanaweza kunipigia na kunitukana. Uliniambia wakati huo sikua na kazi hivyo hata nikiondoka siwezi mnunia mume wangu kwani njaa ikizidi nitarudi na ndugu zangu washanikataa. Nilikusikiliza kaka, nilianz a kupika vitumbua mwaka 2017 mwishoni, mume wangu alikasirika lakini nikaja kusoma Kitabu chako cha Biashara 2018, nilipata ujasiri na kuona kuwa naweza kufanya kitu kingine.
Nilianza kupika nyumbani nazungusha chakula kwenye maofisi na pia nikawa natengeneza juice. Nimeenda na hii Biashara tunagombana na muem wangu mpaka mwaka jana nimeanza kupika kwenye shughuli na napata tenda. Mume wangu hakubadilika bali kila nikipata pesa anadzidisha saharau, ilifikia hatua anawaleta hao mashoga mpaka ndani watoto wanaona, nikaamua isiwe tabu nimehama nyumbani na sasa hivi tupo mahakamani tunataka kugawana nyumba. Ananiambia hataki kuniacha lakini Kaka hivi kweli mtu analeta wanaume ndani na kuna watoto anajifanya marafiki zake hata kama ni uvumilivu ndoa ni haki kweli?
Haoni hata aibu kuongozana na hao vijana ambao wanafahamika kuwa ni mashoga eti kwasababu ana pesa kila mtu ananiambia vumilia. Nakushukuru kaka uliniambia ukweli na naashukuru kwa kunisimamia biahsara yangu kwani nilishakata tamaa ya maisha.
Post a Comment