MBINU AMBAZO ZITAMFANYA MPENZI WAKO AKUONE WA KIPEKEE KILA SIKU!

Index of /wp-content/uploads/2020/04/

Kwa mara nyingine tena napata wasaa  mzuri wa kukuandikia wewe mtanzania mwenye lengo la kukuza na kujifunza mengi juu ya swala la mahusiano 

Leo nitakujuza baadhi ya njia ambazo utazitumia ili siku zote ubaki kuwa wa kipekee kwa mpenzi wako 
1.PENDELEA SANA KUMUULIZA MWENZI WAKO ANATAKA NINI.
Penda sana kujua mwenzi wako anapenda nini na anachukia nini na ni kipi apendi  njia hii itakusaidia sana kufanya yale yatakayokuwa mazuri kwake——— ukiangalia ndoa nyingi  zinavunjika na kusababisha vijana kutopenda kuoa wala mabinti kutopenda kuolewa hii ni changamoto kubwa sana duniani kwa ujumla . Moja ya vitu nilivyogundua ni kuwa ndoa au uchumba au uhusiano wa mapenzi kutokudumu ni kuwa   wengi wameshindwa au hawana utaratibu wa kuwauliza wenzi wao ni nini wanachopeda na nini wasichopenda

Nataka wewe uwe wa pekee kuanzia leo anza sasa kumuuliza mpenzi/mke/mme, wako kwa utaratibu na upole mwendee npenzi/mke/mme wako mf: “kipenzi cha moyo wangu ningependa tudumu  katika mahusiano yetu sitopenda nikukose ata dk 1 ya uhai wangu naomba nijue kutoka kwako ni kitu/vitu gani unavyopenda nikutendee na ni kitu/vitu gani usivyotaka nikutendee  naamini atakujibu.
2.FANYIA KAZI YALE ULIYOAMBIWA.

Baada ya kutambua yale anayotaka na asiyotaka sasa ni wakati wa kuyafanyia kazi hapa kuwa mwangalifu sana usipende kumuudhi mpenzi wako wala kufanya asiyoyapenda mara kwa mara unapouliza nia uwa ni kutambua hivyo ukishatambua ni vyema ukafanyia kazi.
3. THAMANI

Je wajua njia gani ya kuonyesha thamani ili uendelee kuwa bora kwa mwenzi wako  hapa nitakuorodheshea baadhi ya njia ya kuendelea kuwa wa pekee

 

¹ ZAWADI ndiyo zawadi wapenzi wengi upenda zawadi kutoka kwa wenzi wao  hasa kwa wewe wa kipekee.  Pendelea sana kumletea mwenzi wako zawadi ata kama ni “BIG BOM” nayo inakufanya uwe wa kipekee aijalishi utaiona ni ndogo ila thamini kile kidogo najua atakipokea tena kwa furaha zaidi. si lazma zawadi iwe ni gari,au nyumba au piki piki zawadi ata nguo nunua mpe kwa  furaha na tabasamu la upendo. Naamini utakuwa wa kipekee

 

²KUMJULIA HALI 

wapenzi/wanandoa  wengi uwa wanazembea sana swala hili la kuwajulia wenzi wao hali  rafiki nakuambia utaendelea kuwa wa kipekee zaidi  pindi utapokuwa na mazoea ya kumjulia mwenzi wako hali 

Uamkapo asubuhi  aijalishi mmelala kitanda kimoja au kas na kus  muulize “mpenzi/mke/honey/sweet/ hubby. N.k  “UMEAMKAJE!!!  vipi hali yako!! Umelala vizuri!! Nakadhalika  najua ni watanzania wachache sana wenye tabia hii ila nataka wewe uwe wa kipekee zaidi   

Mda wa breakfast, mda wa lunch, mda wa dinner.  

Kama mko mbali mkaribishe mwambie nini unakula mwambie unatamani  siku moja muwe baba na mama mkae pamoja mle pamoja n.k  ata kama mnaishi pamoja penda kumwambia mkeo / mmeo maneno mazuri  “mke/mme wangu  natamani nisikukose ata siku moja wakati wa chakula”  ni maneno madogo sana ila yana nguvu kubwa sana  hii itamfanya mmeo/mkeo/mpenzi wako ata kama yupo kazini itamfanya akujali ata kwa kukupigia simu mda  ambao anakuwa kapumzika akitaka kujua hali yako na natumaini mwenzi wako ataongeza mapenzi kwako.
TAMBUA WAKATI 

ni kweli kuna wakati ambapo mpenzi wako anakuwa na hasira kwa mambo tofauti au msongo wa mawazo  ningependa pia uwe wa pekee kwa kumfuata mpenzi wako tena kwa upendo na tabasa muulize kwa upole. mpenzi wangu nini shida?!!! Kama atokujibu vizuri basi ondoka hapo  kwa mda muache kidogo kwa mda ambao utaona ameanza kupunguza hasira/mawazo. Kisha mpe ata glass ya maji na muache mpaka atakapo acha  mawazo/hasira kisha muulize tena kwa upole na akikujibu mpe ushauri wa busara .
 ❌❌❗❗usimlazimishe wala kumkasiriki.
Kwa leo naomba niishie hapa natumaini somo ili litakusaidia na tena utakuw mtu wa kipekee.


0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post