Kuna mambo mengi ambayo wanawake huona kama ni mambo ya kawaida, huyafanya kwa nia nzuri tu bila kujua kua yanawakwaza waume zao na inawezekana ikawa ni kigezo kikubwa cha ugomvi na kuvunjika kwa ndoa. Wanawake wengi huona kua ukishakua muaminifu, ukamjali mume wako na kumsikiliza inatosha.
Wanaona kuwa kosa kubwa la kukufanya kuachika labda ni uzinifu na dharau kwa mume. Ndiyo haya ni makosa ya kuonekana, lakini kuna makosa ambayo hayaonekani kama makosa ila ukichunguza ni kama mdudu ambaye hutafuna ndoa nyingi. Huleta matatizo makubwa katika ndoa, haya unaweza usiyaite makosa ukasema ni tabia ambazo kama unazo basi badilika.
(1) Kwenda Nyumbani Kwenu Mara Kwa Mara; Umeshaolewa, inawezekana unakaa karibu na kwenu au na ndugu zako, kwakua umeingia kwenye familia mpya una kaupweke flani, hujawazoea au kwakua mume anafanya kazi na wewe upo tu nyumbani unaboreka unaona bora uende kusalimia kwenu, si ni karibu wakati mwingine huna hata haja ya kuomba ruhusa.
Kila wiki uko kwenu, kila ukitoka kazini upitie kumsalimia Mama na Mama naye ukikaa siku mbili tatu utasikia kuwa mbona huji kuniona. Huwezi amini Dada yangu wanaume wengi wanachukia hii tabia, hata kama hakuambii au haonyeshi kuchukia basi jua kuwa ni mbaya. Unapokua unaenda kwenu mara kwa mara inakua ni kama hujaolewa flani hivi.
Unaweza kuona kama kitu cha kawaida lakini unamfanya mume wako ajihisi kama vile anashindana na ndugu zako, kwamba kila wakati unataka kwenda, unaenda peke yako na wala hajui huko unakoenda unaenda kufanya nini? Hata kama ni kusalimia tu lakini mumeo hajui, kuna mambo mengi ambayo mwanaume atawaza na yote yanamfanya ahisi wewe ni mbinafsi.
Kwanza atawaza kua labda unaenda kuwaambia siri za nyumbani kwenu, anawaza kuwa labda hufurahii ndoa ndiyo maana unaenda kwenu kupumzika, atawaza kuwa wewe ni mbinafsi unawapenda watu wa kwenu kuliko watu wakwako, mwanaume hatakuamini kwani atahisi kuwa hata siri za kwake unapeleka kwa ndugu zako.
Lakini mwanaume atawaza kuwa labda unataka mumkalie, ataona kama unataka kumdharau kwani si kila wakati utaomba ruhusa na hata ukiomba akikuruhusu basi ni kwa shingo upande kwakua hataki maneno. Ndiyo ni ndugu zako unawapenda lakini kumbuka sasa umeolewa, unahitaji muda na familia yako mpya, kuna kitu gani umekisahau huko, miaka yote hiyo uko nao mbona ulitaka kuolewa.
Kwa wazazi wa zamani wanajua kua mwanamke haendi endi kwao mpaka apelekwe na mume wake, wanajua kua ile kuendaenda inamfanya ajali ndugu zake kuliko ndoa yake. Unapaswa kubaki na mume wako kutumia muda mwingi nayeye, sasa wewe unafanya kazi, mume naye anafanya kazi lakini mwisho wa wiki watoto mgongoni unaenda kwa Mama.
Hata kama hufanyi kazi ila mume anafanya mwisho wawiki badala upumzike na mumeo umeenda kwenu, ndugu yangu unavunja ndoa yako na ni wanaume wachache sana ambao huamini wanawake wenye tabia hii kwani huwaona kama hawajali ndoa. Sasa najua unajiuliza unatakiwa kutembelea kwenu angalau mara ngapi?
Binafsi naamini kama mko karibu sana sana mara moja kwa mwezi au mara moja kila baada ya miezi miwili. Kwanza kuna simu hivyo unajua hali zao, labda kama kuna ugonjwa ila kama ni wazima basi ikizidi sana mara moja kwa mwezi ila wastani ni mara moja kila baada ya miezi miwili. Narudia mume wako hakuambii tu lakini haipendi hiyo tabia kila siku kwenu!
Unaweza kujiuliza hivi ni kwanini mume wangu hanishirikishi katika mambo yake, hivi ni kwanini anafanya mambo yake kimya kimya, lakini jibu likawa nikwakua tu hakuamini. Unatumia muda mwingi kwenu na unamuonyesha kuwa unawajali ndugu zako kuliko unavyomjali yeye, anaogopa kukushirikisha kwasababu ile kila siku kwenu anahisi labda mnapanga kumfilisi hata kama hana kitu cha kufilisi.
(2) Kushikiwaa Kili Na Ndugu Zako; Rafiki yangu mmoja alikua anafanya kazi katika mkoa flani, ni Kijijini anaishi na mume wake huko na wako vizuri tu. Lakini ndugu zake kwakua wana uwezo wakaona kuwa ndugu yao hawezi kufanya kazi Kijijini hivyo wakamtafutia kazi Dar, wakamuambia ahamie huko na kumuacha mumewe huko huko Kijijini.
Rafiki yangu yule aliniomba ushauri kuwa afanyeje, amuache mume aende Dar au abaki na mumewe kwani huko anakoishi mumewe kashawekeza na hawezi kuhama, maisha yao ni mazuri tu ila yeye hapapendi na ndugu zake kwakua wana uwezo wamemtafutia nafasi Dar. Nilimuambia kama mume wako ana akili siku ambayo utahamia Dar kuwafuata ndugu zako angepaswa kukukabidhi na talaka yako.
Alishangaa lakini nilimuambia kwangu ishu si wewe kukaa Dar, ishu si wewe kutaka kuishi mjini, lakini pale tu ambapo ndugu zako walipoamua kuingilia ndoa yenu, walipoanza kukupangia namna ya kuishi na mume wako ndiyo ambapo umeanza kuiharibu ndoa yako. Ndoa ni ya watu wawili, haina uhusiano wa ndugu wa mume au ndugu wa mke.
Kuna wanawake ambao hawawezi kufanya kitu bila kumuambia Mama yake, Baba yake au Kaka yake, mwanaume hawezi kuamua kitu na mke we utasikia “Ngoja nikaongee na Mama kwanza, Baba alisema nisifanye hiki na kile, sijui nasubiria mpaka Kaka afanye hiki…” Hapana, unapokuabali kuolewa unatakiwa kukubali pia kuwa ndugu zako si sehemu ya ndoa yako.
Labda kama unaonewa unanyanyaswa na kupigwa ndiyo hapo ndugu wanapaswa kuingilia lakini si katika maamuzi ya kawaida ya kifamilia. Kama mwanamke una hii tabia ya kila kitu kuwashirikisha ndugu zako kabla ya kufanya maamuzi acha kwani mumeo anaona kama hana nguvu kwako, anaona kama vile kaoa famila nzima.
Ndoa za mabinti wengi ambao wazazi wao wana uwezo wa kifedha kidogo huvunjika kwasababu hii, wazazi wanakuamulia kila kitu na kama mumeo akisema utasikia “Kama hataki nnjoo utakaa hapa kwani yeye ndiyo anatoa pesa… kwani umekosa nini mpaka kuhangaika na huyo mwanaume!” Wazazi wanakuona bado mtoto na wanataka kuingilia ndoa yako.
Achana na hii tabia kwani kama ukirudi hapo nyumbani ni mwaka tu watakua washakuchoka na kukuona mzigo. Unapaswa kufahamu kua ukiolewa ndugu zako si sehemu ya ndoa yenu hivyo hata kama utaomba ushauri jifunze kufanya maamuzi yako, inakera ndugu wakiingilia ndoa iwe ni ndugu wa upande wa mwanamke au mwanaume.
(3) Kuruhusu Marafiki Waizoee Ndoa Yako; Kuna yule shoga yako ambaye kabla ya ndoa mlikua mnafamya kila kitu kwa pamoja, mlikua mnadanga pamoja, mnaongea kila kitu, kwako kwake na kwake kwako, mnazungumza kuhusu wpaenzi wenu na hata kuvaliana au kuazimana vitu kwenu ilikua kama kawaida, mlikua kama mapacha.
Umeolewa unataka kuendeleza urafiki wa namna hiyo, hapana shoga yako si sehemu ya ndoa yako tena. Si sehemu ya maisha yako mapya, hutakiwi tena kumuambia kila kitu na anapaswa kuwa na mipaka na nyumba yako, hakuna tena kuazimana vitu na mambo kama hayo. Labda nifafanue kidogo ndiyo mtanielewe, sisemi umchukie shoga yako hapana, bali kuwe na mipaka.
Kabla ya ndoa ulikua unamuambia shoga yako kila kitu kuhusu wewe, yalikua ni maisha yako, lakini sasa umeolewa, maisha yako hayawi yako, siri zako haziwi zako, matatizo yako hayawi yako bali ni yako na mume wako. Kwa maana hiyo unapomuambia shoga yako siri zako humuambii zako tu unamuambia na siri za mume wako bila idhini yake.
Wakati hujaolewa ulikua unamuazimisha nguo na vitu vingine, zilikua nguo zako vitu vyako. Lakini sasa umeolewa, si nguo zako tena, si vitu vyako tena, ni vitu vyako na mume wako, hata kama hajakununulia yeye lakini ulinunua wewe yeye akanunua chakula, ni vyenu, nguo zako si zako ni zenu, sasa iweje nguo ambayo anakuvua mumeo umpe na rafiki yako naye avae?
Kabla ya ndoa alikua huru kuingia chumbani kwako, akakaa na khanga moja na kupiga stori lakini umeolewa, si chumbani kwako tena ni chumbani kwenu, hana uhuru huo kwani ukishampa uhuru huo basi unamnyima uhuru mume wako wa kujidai chumbani. Nilazima kuwe na mipaka, shoga yako aishie sebuleni hata jikoni haruhusiwi.
Narudia haya mambo ya shoga yako anakuja kwako mnaingia jikoni kupika yaache huko huko katika uchumba, ushakua mke wa mtu si jikoni kwako tena ni jikoni kwenu. Sijui kama mmenipata, ni mambo ya kawaida lakini yanavunja ndoa, tena katika hili kuwa makini sana kwani nirahisi shoga yako kukugeuka na kukuchukulia mume.
Kama unavyojua sisi wanaume kuchukuliwa nako si kazi sana, unapomambia shoga yako kila tatizo la ndoa yako unakua unampa silaha, unamuambia kwa huna furaha una matatizo hivyo mumeo nirahisi kuibika, anajua udhaifu wa mume wako hivyo unampa vitu vya namna ya kumteka, trust me shoga yako anamtaka na mumeo hatajivunga akitakwa.
Lakini unapomuambia kila furaha, kila kudekezwa na starehe basi ni kama unampa wivu, unamuambia vitu ambavyo yeye anavitamani lakini havipati hivyo unamlazimisha kufanya juu chini ilia avipate na si kwa kufanya kingine bali kwa kumtafuta huyo huyo mume wako.
Sijui kama mmenipata Dada zangu, hembu jifunze kutenganisha urafiki na ndoa, shoga yako ni rafiki yako lakini si rafiki wa ndoa yako. Usiruhusu awe sehemu ya ndoa yako na hata kama ikilazimika kuongea basi hakikisha unayemuambia anaweza kukusaidia, usiruhusu akajua kila kitu katika ndoa yako kwani wewe hujui kila kitu katika maisha yake.
KAM AUMENIELEWA BASI #SHARE UNAWEZA SAIDIA NA MWINGINE
Post a Comment