Mambo hayawezi kuwa sawa kama kila siku umekuwa yule yule na hutaki kubadili tabia yako. Unajua kuna wakati wenza wetu hawana shida ila shida ipo upande wetu.
Unabisha? Umewahi jiuliza kwa nini kila mahusiano ambayo unaingia yanavunjika? Kibaya zaidi yawezekana kila anayekuacha anakwambia sababu lakini ulivyo hauko serious utairudia tena hiyo tabia kwenye mahusiano mengine.
Sasa hapo unadhani unamkomoa nani? Anayechezewa na kupotezewa muda si wewe? Wewe mwenyewe ndo mchawi wa maisha yako na hakuna anayekuroga.
Tabia yako ndo tatizo na wanaokwambia ukweli ukiwaona wabaya ukabaki kama ulivyo basi usije tegemea kudumu kwenye mahusiano yoyote.
"ITUNZE NDOA YAKO"
Post a Comment