MAISHA SI MAGUMU KIASI HICHO, MACHOZI HAYAWEZI KUMBADILISHA HUYO UNAYEMLILIA!
Kisaikolojia mume wako akishaanza kujiona kama Bosi au Baba yako basi anakuona kama unaboa, anachoka misamaha yako na atahitaji kutoka nnje kwani mwisho wa siku hata kama mumeo ni mkali vipi lakini anahitaji mwanamke ambaye atakua mke kwake na si mtoto au mfanyakazi. Sijui kama hata mananielewa nyie dada zangu maana mmekaririshwa kua ndoa ni unyenyekevu hivyo mnajikuta mnaigiza kila siku.
Unyenyekevu sawa lakini nyenyekea basi ukiwa umefanya kosa wewe, kama mtu akikukosea ukanyenyekea basi unakua ni uigizaji na ndoa si uigizaji, kama unajiafanya umekosa wakati hujakosa, kama unaomba msamaha wakati huna cha kuomba msamaha wewe una tofauti gani na Bongo Movie? Hembu niambie kweli si mtu yeyote mwenye akili anajua kabisa unaigiza, maana kuomba msamaha ni kujutia sasa wewe unajutia nini wakati hujakosea?
Jifunze kuheshimu na si kunyenyekea isipokua pale unapofanya kosa wewe basi nyenyekea, jifunze kuwa mkweli na si kuigiza. Huwezi kuwa na furaha wala mume wako hawezi kuwa na furaha kama unaigiza katika ndoa yako, lazima atatoka kutafuta mke wa kweli na kukuacha wewe muigizaji unalia tu ukiwa hujui hata umekosea wapi. Hata katika mahusiano ya kawaida ni lazima uache kumnyenyekea na kuanza kumheshimu!
Acha kukaa na maumivu na kuendekeza kulialia kila siku, tafuta suluhu ya matatizo yako. Maisha si magumu kiasi hicho, machozi hayawezi kumbadilisha huyo unayemlilia.
Post a Comment