Ni kweli wewe ni Mwanamke mzuri, Nikisema mzuri namaanisha kwamba "HAKUNA MWANAMKE ALIYEUMBWA MBAYA" kinacho wachanganya wanaume juu yenu ni kwamba MITAZAMO YAO KWENU NI KWA MAUMBILE NA SIO KWA UHITAJI WA KI JINSIA! Kosa kubwa ambalo utalifanya mbele ya NAFSI yako ni moja tu "UTAKAPOJUA UNAPENDWA NA KUJIONA WEWE NI ZAIDI YA WENGINE" Mwanaume anaweza kubadili wanawake 10 kwa siku na wala asijue yupi Mtamu na yupi Mwenye Radha, Naomba unielewe vizuri katika hilo la RADHA NA UTAMU... Maana yake ni mbili kama yalivyo maneno yenyewe;
1. Radha ni ujumlishaji wa vionjo.
2. Utamu ni uhalisia wa kitu.
Kwa mfano mdogo tu "APPLE UKILILA KAMA LILIVYO NI TAMU LAKINI UKILISAGA LIWE JUISI UTATAKIWA KUONGEZA KITU ILI KULETA RADHA"
Kwa uchache huo utakuwa ushaanza kuifungua akili yako, Unapokuwa umeona Mwanaume kakupenda SHIKAMANA MAMAANGU maana hiyo ni bahati hasa ukizingatia wanaume BY NATURE SIO WATU WA KUTABIRIKA KATIKA UPENDO kutokana na ukweli kwamba wao hutumia MATAMANIO KUMPENDA MWANAMKE tofauti na ninyi Wanawake mnatumia HISIA KUMPENDA MWANAUME! Tofauti hiyo inatosha kumheshimu Mwanaume anayekupenda ili umlinde na MAKUNGURU YA MJINI... Wanawake mna nature moja mbaya sana "KILA MWANAUME AKIKUSIFU UNADHANI AMEKUPENDA" Kuna wakati mama zangu hilo ndilo linawaingiza kwenye UDHAIFU huku ukisahau huyo anayekusifu pengine umependeza ama wewe mzuri hajui uwepo wa Mwanaume wako ni sababu ya muonekano wako, Maana yeye amekuona USO UNA NURU je anajua aliyekupa kuwa na nuru? Maana nijuavyo Stress zikimzidi Mwanamke hata mafuta mnasahaugi kupaka kweli si kweli🤷🏽♂
Unakutana na Mwanaume hajui hata bei ya suruali umevaa, hajui blauz yako bei gani, Wala viatu hajui bei gani n then anakushobokea na kuanza kukupamba kwa maneno na tayari USHAPENDEZA TANGU UNAVAA NYUMBANI KWAKO halafu eti nawe ulivyo mjinga masikio yanakusimama🙆🏿♂
Wacha nikubari Mwalimu wa wanawake alikuwa kipofu ALIWAFUNDISHA KUSIKIA KULIKO KUTAFAKARI maana aonaye hutafakari ajiepushe na balaa lililo mbele yake💃
Chezea mambo yote unaweza kupata tena ila USICHEZE NA MTU ANAYEKUPENDA💪🏽
Sumu ambayo huwa inamiminika kwenye moyo wa Mtu mwenye upendo wa DHATI ni nyingi sana, MAAMUZI yake huwa mawili tu;
▪KULIPIZA
▪KUACHA
Mamaa hayo yote ni hatari kwako, Sasa wewe chezea shilingi ya nauli kwenye tundu la choo UTATEMBEA MPAKA MIGUU IPATE MAGAGA😎
Post a Comment