KWANINI WENGI WANADUMU KWENYE MAHUSIANO KULIKO WAKIINGIA KWENYE NDOA?

Iddi Makengo - Najua una hamu sana ya kuolewa lakini hembu ...
Kwanza ifahamike kwamba MAHUSIANO ndiyo njia sahihi ya kuelekea kwenye NDOA.
Hapo ni rahisi kujua ikiwa mwenza uliyemtarajia ni yeye ama mtarekebishana kuliko zile ndoa watu wanaingia bila kufahamiana ndani yake Kuna VITA KUBWA kuliko hata wale waliofahamiana!
Nirudi kwenye maana ya MADA hii;
KWANINI MAHUSIANO YANADUMU KULIKO NDOA?
Unajua wengi hawajui kwamba MAHUSIANO ni uwanja wa ujana ama ni mahala pa kutakatisha Mapenzi, Uongo ama usaliti ni mahala pake, Kila mmoja kujaribu kuhakiki ni YUPI na ni nani hasa ndiye chaguo lake, Kwenye Mahusiano hata ukisalitiwa ama kudanganywa haiumi sana kama Mtu anapokuwa kwenye NDOA akayaona hayo.
Kwenye MAHUSIANO sarakasi zote ufanye ila ukiishakuwa umetamka neno NDOA acha mara moja ujinga wote, Kwa sababu MAHUSIANO ni UZINZI ndo maana MUNGU akaagiza kila mmoja na awe na MKE/MME WAKE.
Ukiishakuwa umetamka neno NDOA Basi umemkaribia MUNGU huna budi kuachana na UJINGA wako na utubie ili utakapokuwa UMEKANYAGA MADHABAHU YA MUNÄ¢U basi usiwe na hila MOYONI mwako
Ulimdanganya Mwenza wako wakati wa MAHUSIANO na ukabaini ndiye anayepaswa kuwa MKE/MME wako Basi tubia kwake na kwa MUNGU wako ili mnapokuwa mnakwenda kukanyaga MADHABAHU YA MUNGU msipatwe na LAANA kwa sababu MUNGU hadanganywi wala kufichwa kitu bali bin adam tunaweza kudanganyana ama kufichana
Ukikanyaga MADHABAHU YA MUNÄ¢U na Uko na siri zako MOYONI automatically MUNGU ANA DISCONNECT UMOJA WENU kwa sababu hajaukubari japo mnawadanganya MASHEKHE/WACHUNGAJI na MAPADRI
Madhabahu ni mahala penye HUKUMU YA MUNĢU kwa sababu ni sebure ya MUNGU usikanyage na uchafu wako unaohitaji uendelee kuishi nao LAANA inakuhusu ila kama unataka uchafu wako ukuondoke hapo UTAPOKEA TAJI👑
Yaogope MADHABAHU kuliko chochote, Ndo maana mnaingia kwenye ndoa MNAANZA VITA kwa sababu mlikanyaga madhabahu mkiwa na UCHAFU WENU wewe unaolewa ama kuoa kwa sababu zako ni MUNGU YUPI ATABARIKI NDOA YAKO?
Ifahamike kwamba NDOA NI TAJI YA USHINDI KUACHANA NA UKAHABA PAMOJA NA UZINZI lakini wewe Bado unataka ndoa eti ili ushuhudiwe na marafiki ama kumuumiza  wako, Mwanangu IMEKULA KWAKO tarajia VITA vikubwa wala hutafurahia NDOA HIYO.


0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post