Kwa Nini Wanawake Huwakataa Wanaume Flani

Ushawahi kujiuliza kwa nini wanawake wengine ukianza kuwatongoza wanakupa jibu zito ambalo unashindwa kulielewa la: "Mimi na wewe ni kama marafiki"?
Jibu hili hupokewa na wamaume wengi ambao bado hawajakomaa katika nyanja ya kutongoza na kudeti wanawake.
Hili ni tatizo ambalo mara kwa mara hujitokeza iwapo hautaufuata mpangilio stahili ambao unapaswa kuutumia unapoaproach mwanamke.
Unajiona ya kuwa unatongoza mwanamke, kila kitu unachofanya ama unachotaka kutoka kwake anaitikia (isipokuwa muingiliano kimwili), lakini ile siku unapoamua kuufungua moyo wako na kumwambia ya kuwa unampenda anakuzima na kukatiza matumaini yako ambayo ulikuwa tayari umeyaweka katika akili yako.
Kutaka kujua kwa undani swala hili (tayari sababu zake tulikuwa twazijua) tuliamua kukusanya maoni kutoka kwa baadhi ya wanawake warembo kutaka kujua ni kwa nini wanawakataa wanaume ambao wamekuwa wakijaribu kuonyesha upendo wao kwa muda mrefu. Na majibu tuliyoyapata yalikuwa mamoja, yaani walikuwa wakilenga swala moja kuu ambalo lilikuwa likiwachosha.
Nalo ni...
Wanaume ambao hujionyesha kuwa ni watulivu na wasiokuwa na pupa.
Ok mbona wanaume aina hii wanawachosha wanawake na mwishowe kuwakataa?
Kulingana na maoni ya wanawake hawa ni kuwa wanaume aina hii huonyesha tabia ambayo inawafanya automatically kuwaingizwa katika kategoria ya 'marafiki'
Hivyo kutoonyesha matamanio yako kama mwanaume kwa mwanamke ama kuonyesha kuwa wewe ni mwanaume mnyenyekevu kunakuchongea wewe katika azma yako ya kumshawishi mwanamke yeyote.
So makosa ya mwanaume aina hii ni yapi?
Ok hebu tuichukulie mifano ifuatayo...
Je wewe ushawahi kuaproach mwanamke na kumwomba namba yake ya simu kwa kumwambia: "Hello, unaweza kuniazima namba yako ya simu? Labda siku moja tunaweza kuwa pamoja..."
Ama unapomuagiza kutoka naye deti unamwambia: "Hi, kikundi changu kinakutana siku ya Jumamosi, naonelea uungane nasi, itakuwa siku ya furaha..."
So tatizo hapa linajitokeza kivipi?
Wanawake wanapenda mwanaume mwenye nishati, nguvu na uwezo wa kuamua haraka haraka, mwanzo akiona mwanaume aina hii huwa anasisimka papo hapo. Unamuacha na maswali ya kutaka kujua zaidi kuhusu maisha yako ya undani.
So kuonyesha nishati aina hii utafanyaje?
Wakati mwingine ambapo utakutana na mwanamke unamwomba namba yake, toa simu yako, mpatie na umwambie hivi: "Shika. Niwekee namba yako kwa simu yangu. Ntapenda nikutoe out siku moja."
Kufanya jambo hili moja pekee kutakuwa kumekufanya ujitokeze kama mwanaume mwenye kujiamini, mwenye nguvu, na nishati ambaye anapigiwa upato na wanawake wengi. Na kamwe hatakuweka katika kategoria ya 'friend zone'
Ni rahisi ama?
Ok wakati mwingine unapoaproach mwanamke nataka uonyeshe nishati yako kama mwanaume, nataka uonyeshe kuwa wewe si mwanaume wa kuingizwa katika kategoria ya 'urafiki'. Mwanzo nataka uonyeshe ushupavu wako kwa kuzitumia mbinu tatu ambazo zitamfanya mwanamke akuheshimu sehemu yeyote pale ambapo atakuona. Nataka udhihirishe ya kuwa wewe ni mwanaume alpha ambaye hatikishiki na jambo lolote lile.


0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post