Utavumulia maumivu na manyanyaso mpaka lini ? Utaendelea kuvumilia usaliti na dharau zake kisa tu yeye ana pesa au kisa tu ye ni mrembo sana au handsome??
Mwonekano wake mzur au pesa zake vinakusaidia nini kama hakuheshimu wala hakujali ?? Unahis ukimuacha utapoteza maisha na furaha au vipi??
KAKA/DADA epuka kuwa mtumwa wa penz kwa mtu asiye jali uwepo wako kwake. Usiogope kumpoteza hata kama bado unampenda. Kwan wangap uliwah kuwa nao ila sasa umewasahau ?? Kumbuka ulimchagua awe taa ya kuangaza maisha yako sasa kawa fisadi wa mapenz hakufai.
Ktk maisha yako jifunze kuwaruhusu wanso taka kukaa mbali na maisha yako. Huwez wazuia watu wanao kukimbia bali jifunze kuishi bila wao na kuamin kesho utapata bora zaid yao. Machozi yako hayatoshi kufuta kumbukumbu mbaya ko kaa chin kisha inuka kishujaa. Leo anakuona Taka Taka kesho atakuona Almasi baada ya kukupoteza na ukaokotwa na wengine
Epuka kuishi kwa historia kila kitu kinatokea kwa mipango ya Mungu. Shida zinapo kuzidia ujue Neema inakaribia. Simanz yako ina mwisho wake. Usiruhusu aendeshe maisha yako sababu ya pesa zake au mvuto wake. Hapo ulipo Bado unathaman kubwa jitunze siku utathaminiwa
Wa kuja kukupa faraja humjui na hujui wap na lin utampata kwa sasa endelea mwomba Mungu. Umekutana nae ukubwan bas asikufanye ujute kuzaliww. Kumbuka Mwanajeshi huenda vitan akiwa hajui kesho yake..nawe ishi kwa kumuomba Mungu zaliwa upya na akili mpya. Wewe ni MAMA/BABA...MKE/MUME wa kesho. Usikate tamaa kisa umri
KILA la HERI
Jikomboe mwenyewe
Jikomboe mwenyewe
Share na rafik yako
Post a Comment