Mwanaume anapokuambia hapana, anapokuambia sitaki, anapokuambia nina mtu mwingine hembu kubaliana na hiyo hali, acha kuendelea kufanya vitu vingine kwa lengo kuwa labda utamshika, utambadilisha mawazo. Dada zangu mnajitafutia matatizo bure, mpaka anakuambia kuwa sikutaki inamaanisha kuwa tayari ashatafakari na kufikia uamuzi.
Najua mara nyingi mnawasingizia hao wanawake wengine, kwamba labda kamteka, labda sijui kamuwekea dawa, labda hiki na kile. Unatakiwa ukumbuke tu kuwa hata kama ni dawa lakini huyo mpenzi wako hakuiruka Barabarani, alimfuata na kumtongoza ndiyo akawekewa. Najua unataka sana kuolewa lakini wewe kuzidisha kukata viuno au kumbebea Mimba haitasaidia.
Wanaume ni walafi, hula hata vyakula walivyovikataa lakini haimaanishi kua wataviacha vilivyoko mezani. Hivyo usione bado anakutumia kimapenzi, ukijipeleka bado anapiga shughuli utadhani kama bado anakupenda, hapana, kama kashakuambia sikutaki au kukuonyesha dalili hakutaki basi jua kuwa anamaanisha hakutaki.
Ukienda kwake mechi atapiga na kesho huyo mwingine atapiga, najua ushaziona dalili kua hutakiwi, hakupigii simu, hakutumii SMS, kashakuambia kabisa nina mtu wangu au kakuambia usinipigie muda flani. Kakuambia kuwa anataka kuoa au kashamtambulisha mtu kwao lakini bado unajipeleka eti unataka umbebe mimba kumkomoa huyo mwingine.
Dada yangu unapombebea mimba mwanaume wa namna hii jua unajiandaa kuwa ‘Single Mother’ wanaume wa zamani ndiyo walikua wakikoa sababu ya mimba ila sasa hivi mtu ataoa wangapi kama kila anayempa ujauzito anatakiwa kumuoa, siku hizi wanakwepa majukumu anakuacha ulee anarudi kwako mtoto ashakua mkubwa.
MIMI NISHAMALIZA WEWE NENDA KAMBEBEE MIMBA UKIOTA NDOA!
Post a Comment