Kuna wakati MAPENZI yanatakiwa kuachwa kama yalivyo ili kuruhusu VITA ZA UPENDO WA KWELI NA UPENDO WA MPITO vipigane💊

FAHAMU TABIA ZA MWANAUME MWENYE NIA YA... - Mwalimu Bemasha ...
Kuna wakati watu wanahitaji MAPUMZIKO japo kwa muda usiojulikana ili kuileta maana ya UPENDO MBELE YAO💏
Kuna wakati kukaa muda mwingi au mrefu mkiwa pamoja Kuna hali fulani ya UCHOVU hujitokeza, Kwamba Mtu anaweza kukuchoka bila sababu, Na hapo ndipo viji maneno vya dharau, Kebehi hujitokeza na ukiona hivyo huna budi kuipisha hali hiyo, Haimaanishi kwamba UMECHOKA laa hasha ila unajitenga na ile hali ya kutengeneza UGOMVI unaosababishwa na HASIRA kutokana na mwenza wako kuzidi kukukwaza, Lakini pia haimaanishi kwamba MWENZA WAKO HAKUPENDI ila mnahitaji muda wa kujua DHAMANA YA PENZI LENU IMEFIKIA KIWANGO GANI🔬
Umbali ni shuhuda wa UPENDO kwamba ule ukaribu haupo tena kutokana na KUTOELEWANA KWENU😭
Na hapo ndipo ile sura ya PENZI LENU LA AWALI INAWEZA KURUDI ili kuwajenga upya namna ya kuishi bila migogoro, Kwa sababu UMBALI ambao mtaupitia bila kuwa na mawasiliano mazuri ama kutowasiliana kabisa Kuna uhakika wa 75% kila mmoja atakuwa analia ki vyake.
Mapenzi yanajengwa kwa MARIDHIANO baada ya kutokea kutoelewana, Lakini naoongelea PENZI LA DHATI hilo ndilo linaweza kuishi hata kwenye MIGOGORO
Jifunze kuruhusu UMBALI ikiwa Unajua kwamba MNAPENDANA💑
Kwa kufanya hivyo utaboresha upendo na kujenga DHAMANA kubwa ndani ya Mwenza wako, Kwa sababu KAMA MKO KWENYE KUTOELEWANA NA UKABAKIA KUPAMBANA ILI KUJITETEA Kuna nafasi kubwa sana ya kuharibu UPENDO ulioujenga kwa mwenza wako, Kwani atakuona UMEBADILIKA ama Una DHARAU kitu ambacho kitamvunja MOYO mwisho wake ni kuanza kuhesabu makosa yako, Taratibu PENZI lenu litakuwa REHANI👥
Ipishe gadhabu ya ki bin adam Kwani hiyo huleta MAUDHI na ukiona MAUDHI utaingiwa HASIRA kama sio UGOMVI basi MTAUA UPENDO WENU
JIBU LA UKIMYA NI MWIBA KWA MKOSAJI Jifunze kuwa mshindi hata kama unaumia, Jipe muda kuumia ili umjenge mwenza wako KUTHAMINI PENZI LAKO💪
Lakini ikiwa ni wa kwako MKIRUDIANA itakuwa ilipangwa ninyi kuwa WAMOJA💝
Na kama ikitokea UMBALI ukaua PENZI lenu ujue huyo hakuwa wako ila mlishiriki mambo ya KUPITA.


0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post