KUA MAKINI SANA NA MTU HUYU, ANATAKA WEWE UMUAMINI LAKINI YEYE HAKUAMINI!

SIMULIZI: Jamani Unaniuaaaaaa (Sehemu ya 22) - Linda Penzi Lako
Mara nyingi hutokea kwa wanawake, lakini wapo wanaume pia. Una mpenzi wako, unampenda sana na kweli anaonekana na yeye kukupenda, mmekua mkishirikiana katika mambo mengi ya kikawaida tu, labda wote mnafanya kazi hivyo akikwama unamsaidia na wewe ukikwama anakusaidia. Lakini sasa hamjafikia kuoana, labda kuna sababu za msingi zinawazuia kufanya hivyo na pengine hata hizo sababu hakuna.
Lakini tu hamjaoana, kwakua una kazi na pengine mnafanya mambo kwa pamoja na hata kuishi pamoja kama mke na mume anakuambia mfanye mambo ya maendeleo kwa pamoja. Labda kununua kiwanja na hata kujenga au kununua gari. Unamuambia sawa na kwakua kunampenda na una mipango ya kuingia naye katika ndoa unaona haina shida unamuamini unakubaliana naye.
Lakini katika kufanya hicho kitu cha maendeleo unamuambia kuhusu kuandika majina yenu, kwamba si mnataka kujenga, kununua kiwanja au gari, unamuambia katika mkataba basi muandike majina yenu. Anawaka! Anataka uchangie lakini hataki jina lako liwepo. Labda anakumbia mimi ndiyo mwanaume jina langu linapaswa kuwepo, lakini haiiishii hapo unasikia “Kama huwezi kuniamini kwa kitu kidogo kama hiki basi hata kwenye ndoa sijui kama tutawezana!”
Haya ni maneno ambayo wanaume wengi hutumia wakitaka kuwaonea wanawake. Narudia mara nyingi hutokea kwa wanawake ingawa kuna wanaume pia hufanyiwa hivi. Anataka umuamini yeye kuwa hatakudhulumu, uchangie pesa mjenge lakini hataki kukuamini wewe na kuweka jina lako. Dada yangu kuwa makini wanaume wa namna hii mara nyingi hukufanyia moja kati ya mambo haya mawili.
Kwanza inawezekana hata hana mpango na wewe, ana mpango wa kukudhulumu tu hivyo hataki ushahidi kuwa na wewe ulichangia, inawezekana hajaamua kuoa na hajui kama atakuoa wewe, labda kuna na mwingine na mwingine inawezekana mko wengi na wote mnachangia katika ujenzi au kununua gari, lakini uko peke yako na hajapanga kama atakuoa au la ila anapenda pesa zako.
Jambo la pili inawezekana anakupenda kweli, ana mpango wa kukuoa lakini hajiamini, hajiamini kuwa na wewe kama mwanamke ukiwa na mali utamheshimu. Kwa maana hiyo anataka kila kitu kiwe kwa jina lake ili siku akikuoa na akaanza kukunyanyasa basi akuambie ondoka hukuja na kitu. Si nyumba mlojenga wote iko kwa jina lake, hapa anakua hana mpango wa kudhulumu lakini ana mpango wa kukunyanyasa.
Kwa maana hiyo dada yangu au wewe ni mwanaume, kama mwanaume akianza hivi, anataka mfanye mambo kwa pamoja lakini kila kitu kiwe na jina lake, ni nyumba jina lake, gari jina lake, biashara jina lake basi kuwa makini, ni bora ukafanya peke yako kwani jua kuwa unaweza usiolewe ukapigwa chini na usiambulie chochote na hata ukiolewa basi ukaishia kunyanyaswa kila siku na kutamani kutoka kwenye hiyo ndoa.
MIMI NISHAMALIZA WEWE SOMA KIMYA KIMYA UAMUZI NI WAKO!


0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post