KILA TATIZO UNALOKUTANA NALO KUMBUKA KUNA NJIA IMEWEKWA KWA AJILI YA KULIMALIZA


Kwenye maisha tunapitia chagamoto nyingi sana, wengine wanapita kwenye magonjwa, wengine elimu, wengine kazi, wengine ndoa, wengine biashara, wengine Watoto na baadhi ya changamoto nyingine nyingi (ambayo hayo ndio majaribu)
_
Sikia hakuna jambo likapita kwako, Mungu asijue kwasababu Mungu anatabia kabla ya kuruhusu uzaliwe anaenda mpaka mwisho wa maisha yako anatazama wapi utapita na nini utapitia alafu anarudi mwanzo anaruhusu uzaliwe, ndio maana ukiona kuna jaribu unapitia ujue Mungu ameweka mlango wa kutoa yani ameweka njia za kutatua hilo tatizo moja na njia ni watu ambao watashirikiana na wewe kumaliza hilo tatizo
_
Ndio maana hakuna jambo gumu mbele za Mungu kwa hao walio na imani, ndio maana hakuna taharuki wala kukata tamaa kwa wote wamwinio Kristo, haijalishi unapita kwenye shida gani hata kama mambo ni magumu, jua kwamba ipo njia ya kumaliza hilo tatizo na Mungu hawezi kuruhusu ubebe jaribu ambalo huwezi kulitatua, ukiona ameruhusu ujue uwezo unao
_
Unapoona unapita kwenye hali ngumu, muombe Mungu akupe uwezo, akupe watu wataopita na wewe kwenye hilo jaribu, usilie mwambie Mungu najua umeruhusu hili litokee ila naomba unipe nguvu za kupambana nalo, yote mkabidhi Yeye, wakati mwingine Mungu anataka Imani yako tu

_
Unakumbuka wana Israel walipofika bahari ya shamu, walijua huo ndio mwisho wao maana nyuma farao alikuwa anakuja na jeshi lake, na Musa akamlilia Mungu na Mungu akafanya njia pasipo na njia
_
Biblia inatufundisha nini, unapoona imefika mahali hakuna msaada usikate tamaa aliye juu anao msaada, anajua atafanya nini, usikimbie huku wala kule wala usijaribu kumuacha huyu Mungu aliye hai katika Kristo, Muombe kadri uwezavyo kisha acha mapenzi yake yatimizwe
_
Nakuhakikishia Mungu hatakuacha uaibike hata kidogo kama ni watesi wako utaona wanavyokanyagwa mchana kweupe, yani utashanga namna Mungu atasimama upande wako, kinachotakiwa ni kuomba bila kukata tamaa na imani tu


0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post