Mwanaume yoyote anapofikia umri wa kuoa na kuamua kuoa anakua tayari anajua majukumu ya mwanaume kama kuhudumia familia na kujiandaa nayo. Wanaume hubadilika na kuacha kubeba majukumu yao kwa sababu kuu mbili. Sababu ya kwanza ni kuwa na mchumb kiherehere, kwamba wakati wa uchumba mwanaume alikua hajawa tayari kuoa au lakini mwanamke akalazimishia na kuwa anabeba majukumu, yaani kipindi hicho mwanamke anampa pesa mwanaume.
Mwanamke anamhudumia mwanaume, mwanamke anafanya mambo ya maendeleo kwa jina la mwanaume na pesa za mwanamke anakua nazo mwanaume. Mwanaume wa namna hii akioa anageuka kabisa ile kanuni na wajibu wa mwanaume kuhudumia familia, anaweza kutegea akijua kuwa mwanamke wake ni jiherehere asipofanya naye atafanya. Sababu nyingine ya mwanaume kubadilika ni pale ambapo mke anabeba majukumu ya mume baada ya ndoa.
Kwamba mwanaume ameoa mwanamke ndiyo hutafuta nyumba na kulipa kodi au mwanamke ana nyumba wanaenda kuishi kwa mwanamke, huyu mwanaume lazima atakwepa majukumu, mwanzo tu wa ndoa mwanamke anaanza kununua chakula na vitu vyote vya ndani, huyu ni kiherehere. Mwanamke anataka maisha flani ya juu, anaanza kununua vitu vingi vya ghali ambavyo si vya muhimu kwakua tu ana pesa anaona kwanini niteseke! Mwanaume akiona kuwa mwanamke wake ni wanamna hii basi huanza kumtegea majukumu na akiona anayafanya basi humuachia kabisa majukumu.
Mwanamke jifunze kunyamaza, umeolewa wote mnafanya kazi mwanaume akisema huna wewe ni nani useme unacho, mwingine anaenda kukopa kabisa ili tu ahudumie familia. Mara nyingi wanaume wa namna hii wanaposema hawana haimaanishi hawana, wanapima upepo kuona kama utatoa, ukitoa basi hatoi lakini kwakua anajua ni majukumu yake basi atatoa. Kama ndiyo unaingia kwenye ndoa fanya hivi mapema, ajue kabisa kuwa huyu mke si wa kutegea, ukimzoesha akisema huna unatoa subiri mtakua na watoto, kwamba ndiyo hatatoa kabisa kwani anajua kuwa huwezi acha wanao washinde njaa utakopa.
Mwanamke upo kwenye ndoa badla hata unukie Udi unanuka madeni kama vile huna mume! Kuna wakati sawa hana na unaona hana, lakini kama ni kila siku hana na bado unatoa basi jua anakuchora. Kumbuka tu kuwa pesa ya mwanaume lazima iliwe na mwanamke hivyo kama wewe mke wake huli basi itaenda kuliwa na mchepuko! Ukiona wewe hakuhudumii jua kuna sehemu nyingine anahudumia, pesa ya mwanaume haiwi tamu kama haijaliwa na mwanamke.
Post a Comment