Kama wewe ni mwanamke, upo kwenye mahusiano, una mtu wako siriasi hembu anza kujiheshimu, anza kupunguza wale marafiki wa kukushikashika kila mara, anza kupunguza wale marafiki ambao wamekuzoea kiasi kwamba unaweza kujiachia tu mbele yao na wao kuona mwili wako hovyhovyo kwakua tu ni marafiki, anza kuondoa mazoea na mitoko isiyoeleweka na marafiki, mitoko ambayo inatia shaka.
Si kwamba usiwe na marafiki hapana, lakini kuwa na heshima, kwa maana kuwa, hakikisha marafiki zako wanakuheshimu na hawakufanyii mambo ambayo mpenzi wako akiyaona anahisi unachepuka. Unaweza usiwe unachepuka, lakini ukiwapa uhuru sana marafiki zako wakiume jua kuwa atautumia na wanaweza kuvuka mipaka, ipo siku watajisahau na kukushikashika mbele ya jamaa yako, ipo siku watakutumia mameseji au mapicha ya ajabuaajabu na kuweza hata kuvuruga mahusuano yako! Badilika kuna mambo mengine si ya lazima sana!
Sio kila mtu anaeku-treat vizuri anastahili nafasi katika moyo wako. Baadhi ya watu ni mbwa mwitu waliojivika ngozi ya kondoo, na wako vizuri sana katika mikakati yao.
Hivyo, kuwa makini sana na watu unaowakaribisha moyoni mwako. Usiwe na haraka ya kuamini watu. Usiharakishe kufanya vitu ambavyo utakuja kuvijutia punde kidogo. Chukua muda wa kutosha kumjua mtu kuhusu interest yake, tabia yake, malengo yake kuhusu wewe na mahusiano yenu.
Kama mtu anakung'ang'aniza kuharakisha jambo ambalo kwalo, wewe hauko tayari au hauko comfortable nalo, hiyo iwe alama ya mapema kwamba, wako kwa muda tu na sio lifetime commitment.
Kuwa makini sana na watu na jifunze kuepuka mambo yatakayokuletea majuto mbeleni. Maisha ni zawadi tuliyotunukiwa na MUNGU, si sawa kwa wewe kuendelea kuwa mtu wa kuumia, kuwa disappointed na stress kibao mara kwa mara. Unatakiwa ujifunze kupitia makosa, na kulitumia funzo ulilopata.
Maisha yako ni bora na yenye thamani kubwa sana, furaha na amani ya moyo ndio chachu ya kufanikisha kusudio la uwepo wako.
Licha ya maumivu tunayosababishiwa na wale tuliowaamini, tusichoke! tujifunze kujithamini na kufurahia maisha yetu Pasina kutamani maisha ya wengine, maana, hatufahamu na wao wanapitia magumu yepi.
My sister, mwanaume bora na sahihi kwako hua hata ha-propose relationship. Siku zote hukukuta ukiwa busy na mambo yako na hukusaidia kufanya vizuri zaidi kwenye hayo mambo yako.
Ni mfano kama wa bacteria, huwezi jua ni lini wameingia mwilini mwako, nae huingia katika maisha yako from nowhere, utajikuta tu unamiss kuwa karibu nae. Mwanaume alie bora hua haingilii na kuharibu chochote katika maisha yako..iwe kiroho, kimwili na hata kiuchumi!
Huwa haji kama Boyfriend, huja kama rafiki tu na mwishoe hujikuta mmefika milestone katika mahusiano!
Hata siku moja hua hatangazi kusudio lake la kukuoa, hua haji na bango kichwani lililoandikwa "NIMEKUJA ILI NIKUOE". Wanaume waoaji huwa hawana mbwembwe kabisa.
Uliza yeyote yule aliyepo kwenye ndoa iliyo na furaha, atakueleza namna walivyofahamiana na huyo mume wake....
Mwanaume sahihi ni yule ambae unamiss uwepo wake..ni yule mwanaume ambae ukiwa peke yako unawaza kwamba "I wish he was here, he would have..... " My beloved black sister huyo ndio mwanaume sahihi kwako!
Sio yule ambae ukiona anakupigia simu mapigo ya moyo yanaenda kasi kwa hofu, sio yule ambae kila mkiwa pamoja lazima mgombane kwa issue ya usaliti, sio yule ambae kila mkigombana kidogo anatishia muachane, sio yule ambae kila siku unalilia na kubembeleza mahusiano...that's not your man. Huyo ni mwanaume wa mwanamke mwingine.
Mwanaume sahihi kwako huja na impact chanya kwenye maisha yako, huacha alama katika maisha yako ambayo hauwezi kuisahau, sio kuisahau kwa maumivu, la hasha..ni alama inayoakisi mapenzi, faraja, na matumaini!
Look around your circle and you will see this guy. He is already within reach.
Post a Comment