Moja kati ya maamuzi ya kipuuzi ambayo utayafanya baada ya kuachana na mwanaume, halafu huyo mwanaume akaenda kuoa mwanamke mwingine ni kutaka kumkomoa huyo mwanamke aliyeolewa. Inawezekana kakunyang’anya, alikupindua au uliachwa vibaya na unahisi kuwa yeye ndiyo sababu ya wewe kuachwa, lakini kuendelea kuwaza kulipa kisasi ni kuendelea kujipa maumivu na kumpa ushindi.
Mbaya zaidi ni kwa wewe kutaka kulipa kisasi kwa kulala na huyo mwanaume. Kwamba unaona kwamba kwa kutembea na X wako labda utamkomoa huyo aliyeolewa, hakuna kitu cha kujidhalilisha kama hicho. Najua unahasira na kwa wakati huo unaweza kuona kama ndiyo njia muafaka ya kulipa kisasi na kumuumiza huyo mwanamke mwingine lakini mwisho wa siku utaishia kujiumiza mwenyewe na si huyo unayelenga kumuumiza.
Nilazima ujue kwamba kila mwanamke anapoolewa anajua mwanaume wake alikua na mtu kabla, alikua na X na mara nyingi mwanamke kama alikunyang’anya mwanaume alishajiandaa na mapambano na hata hajali kitakachotokea. Yaani hiyo ni sawa na kumwagia mlenvi Pombe ukitegemea atakasirika, hapana atakuona fala tu na wewe utapata hasara ya Pombe yako hivyo kuwa makini unapoachika.
Kisasi kizuri hapa ni kwa wewe kumuacha aende, kwamba kuonyesha kutokujali na kuona kama umetupa takataka. Ona kama vile umetupa chakula kilichochacha jalalani. Halafu vuta picha hivi mfano ukatupa wali wako, wali kuku ulikua mtamu lakini umechacha ukautupa jalalani, mbwa akauokota na kuanza kuula, hivi utaenda kuumfukuza mbwa na kuanza kugombania naye mfupa wa kuku ulikwisha utupa?
Labda kama wewe ni kichaaa, kwa wenye akili hawafanyi hivyo naamini hata wewe hutafanya hivyo. Jithamini na tambua kuwa kama likitoka limetoka halirudi tena hivyo acha kujidhalilisha kwa kushindana na mbwa jalalani? Kama ameshaoa asikudanganye kwmabaa likosea bado anakupenda, hapana hakupendi, inawezekana kuna vitu anavimiss kwako lakini hakuwahi kukupenda kwani angekupenda angekupigania mpaka mwisho!
Post a Comment